Sabena Bus,yaua!

Sabena Bus,yaua!

Ghiti Milimo

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
5,134
Reaction score
7,651
Basi la Sabena,lililokuwa linatoka Mwanza,kuelekea Tabora,limepata ajali,na kwa uchache watu saba wamefariki papo hapo,maeneo ya Busanda,nje kidogo ya mji wa Shinyanga. Kwa mujibu wa ndugu yangu,aliyekuwepo eneo la tukio,ajali yenyewe,imetokea hivi:-
Basi la Air Time,lilikuwa linafuatwa nyuma na Sabena. Pia,mbele kulikuwa na farasi wawili,wakiendeshwa na wazungu,kila mmoja na farasi wake,wote wakielekea njia ya kuelekea Nzega,kutokea Shinyanga.
Wakati huo huo,mbele kulikuwa na SEMI lililobeba cement,kuelekea Shinyanga. Sabena,bila tahadhari,dereva akaamua kulipita Air Time,ghafla,akaliona hilo SEMI mbele yake! Akalirudisha kushoto,na kuligonga Air Time kwa nyuma,baada ya hapo,likarudi tena kulia,na kukutana uso kwa uso na SEMI,ambalo baada ya kugongana,lilitoka nje ya barabara,na kuiacha Sabena barabarani,likiwa limepondeka vibaya!
Lile Air Time,lilipogongwa nyuma,lilienda kumgonga farasi mmoja,likamvunja mguu,na kumuua mzungu aliyekuwa ameipanda!
Hilo Air Time,hakuna aliyeumia!
Ajali hii,imetokea leo saa 2 asubuhi.

Source: Ndugu yangu,aliyekuwepo eneo la tukio,na kutoa msaada kwa majeruhi!
 
Wapumzike kwa amani hao marehemu, mungu awajaalie nafuu ya upesi majeruhi. Amen
 
yaani inasikitisha sana. Ajali mara nyingi sana inatokana na uzembe wa dereva, na uzembe wa dereva nao unachagizwa na hitaji la kutaka kuwahi kufika destination waendayo.

Too sad. Mungu awapokee roho za marehemu wote na kuilaza mahali pema peponi. Amen
 
Kweli uzembe wa madereva wetu utatumaliza. Ajal ya kizembe kabisa hiyo. Sijui tusafiri na nn?
 
Wakuu kuna haja ya kuhoji HIZI leseni mpya za madereva walisema zitapunguza ajali jamaa wakala tenda ya sh 40000 mara madereva 1.5m,jee mbona AJALI zinazidi kuongezeka?
 
RIP marehemu, hii kampuni ya sabena mwenzi wa 7 au 8 hivi iliua watu karibia 1o ikielekea mbeya, tukaambiwa imefungiwa na mmiliki kakamatwa, hivi ilifungiwa mbeya tu au kote na kama ni maeneo yote iliruhusuwa lini?
 
Ilifungiwa kote mkuu,nafikiri ilifunguliwa mwezi wa kumi.Nafikiri kuna haja ya kuifutia leseni kabisa hiyo kampuni.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Roho yangu inavuja damu kwa uchungu!
Mungu wa Israel turehemu!
 
nyie madereva vilaza mnatumaliza jamaniiiiii r.i.p ndugu zetu
 
Ilifungiwa kote mkuu,nafikiri ilifunguliwa mwezi wa kumi.Nafikiri kuna haja ya kuifutia leseni kabisa hiyo kampuni.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

itakuja na jina lingine
BASENA subiri ifutiwe leseni
 
Mungu awalaze marehemu wote mahali pema peponi na awape nafuu majeruhi wote,amein!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Basi la Sabena,lililokuwa linatoka Mwanza,kuelekea Tabora,limepata ajali,na kwa uchache watu saba wamefariki papo hapo,maeneo ya Busanda,nje kidogo ya mji wa Shinyanga. Kwa mujibu wa ndugu yangu,aliyekuwepo eneo la tukio,ajali yenyewe,imetokea hivi:-
Basi la Air Time,lilikuwa linafuatwa nyuma na Sabena. Pia,mbele kulikuwa na farasi wawili,wakiendeshwa na wazungu,kila mmoja na farasi wake,wote wakielekea njia ya kuelekea Nzega,kutokea Shinyanga.
Wakati huo huo,mbele kulikuwa na SEMI lililobeba cement,kuelekea Shinyanga. Sabena,bila tahadhari,dereva akaamua kulipita Air Time,ghafla,akaliona hilo SEMI mbele yake! Akalirudisha kushoto,na kuligonga Air Time kwa nyuma,baada ya hapo,likarudi tena kulia,na kukutana uso kwa uso na SEMI,ambalo baada ya kugongana,lilitoka nje ya barabara,na kuiacha Sabena barabarani,likiwa limepondeka vibaya!
Lile Air Time,lilipogongwa nyuma,lilienda kumgonga farasi mmoja,likamvunja mguu,na kumuua mzungu aliyekuwa ameipanda!
Hilo Air Time,hakuna aliyeumia!
Ajali hii,imetokea leo saa 2 asubuhi.

Source: Ndugu yangu,aliyekuwepo eneo la tukio,na kutoa msaada kwa majeruhi!

kwa hiyo wamekufa 7 na mzungu mmoja?
 
Ilifungiwa kote mkuu,nafikiri ilifunguliwa mwezi wa kumi.Nafikiri kuna haja ya kuifutia leseni kabisa hiyo kampuni.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

kweli mkuu, ajali za mabasi haziwezi kuisha tanzani kwakua wameliki wameingia mikataba na ushirikina, poleni wafiwa na MUNGU awaguse majeruhi ili wapone haraka
 
Back
Top Bottom