Sabasaba na vilio vya wakulima wa pamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sabasaba na vilio vya wakulima wa pamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tocolyitics, Jul 7, 2012.

 1. t

  tocolyitics Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni miaka mingi sasa wakulima wa pamba wamekuwa wakilima kwa taabu na kujituma kwingi lakini serikali inawaachia tu wanunuzi wa pamba ambao wengi ni wanasiasa wa chama hiki hiki cha zamani wapange bei wanayotaka wao. Wakulima hawa takribani milioni 16 wengi wao wakiwa kanda ya ziwa wanavilio na maumivu makubwa baada ya bei kutangazwa kuwa 660 kwa kilo. Inauma sana kwani kila msimu ukifika vikao vinaanza kujadili bei ya pamba na haya ndo matokeo yake. SABASABA miaka za zamani kidogo wakulima wlikuwa wanasherehekea kabla NANENANE haijaanzishwa kwa furaha lakini sasa ni vilio tu. Serikali jamani mbona mnawatelekeza wakulima wenu? Hongera mbunge NCHAMBI kwa kujaribu kututetea na sisi tumekuona ingawa chama chako ndo kimetufikisha hapa tulipo.
   
 2. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Suluhisho la tatizo la pamba na mazao mengine ya biashara ni kutoyauza yakiwa ghafi. Serikali itafute namna ya kutengeneza na kuuza bidhaa zinazotokana na mazao hayo.Vinginevyo kila mwaka tutaendelea kusikia kilio cha wakulima. Mwaka jana bei ya pamba ilikuwa Tsh.1000/= Mwaka huu wakulima walitarajia kwamba itakuwa ama Tsh. 1000/= au zaidi ya hiyo lakini wamepata presha waliposikia bei ni Tsh. 680/=!!!
   
 3. t

  tocolyitics Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakuu mbona mko kimya au wakulima mmeridhika na mmeamua liwalo na liwe.
   
 4. t

  tocolyitics Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu uko sahihi, lakini pia serikali ingefufua viwanda vyetu vya nguo mkulima asingelia hivi coz soko lingeongezeka
   
 5. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hii ni changamoto kubwa sana kwa sera zetu kama kilimo kwanza. Ndiyo kuna mikakati ya kuimarisha kilimo cha mbunga na mahindi katika maeneo ambay mazao hayo yanastawi. Lakini sehemu kubwa ya nchi inastawi mazao ya biashara kama pamba ambayo yanastahimili ukame na hayahitaji mvua nyingi.

  Mwaka huu katika kuvuna Kilo moja ya pamba kibarua alilipwa shillingi mia 200-300 kwa kilo, kulima ekari moja ilikuwa 40,000, palizi 30000 kwa ekari x 2= 60,000 bado gharama za pembejeo kama mbegu na madawa. Kwastani ekari moja iliyostawi vizuri ni kilo 400- 500, ukikokotoa garama zote hizo utaona kuwa mkulima hana alichokipata kwa mwaka mzima endapo atalipwa kwa bei chini ya 1000. Kitakachotokea wakulima wataacha tena kulima zao hilo kama ilivyo kuwa miaka ya nyuma.
   
 6. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Serikali iangalie uwezekano wa kuwa-subsidize ili kuepusha kilimo cha pamba kufa nchini.
   
 7. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Nchi yenyewe imeshakufa!
   
Loading...