Sabalheri mbunge wangu Gwajima

Sabalheri mbunge wangu Gwajima

kirengased

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2016
Posts
6,818
Reaction score
7,484
Nichukue nafasi hii kumtakia kheri na kumpongeza mbunge wangu wa Kawe Askofu Gwajima.

Ukweli misingi ya siasa zaleo Kwa nchi nyingi Afrika zinahitaji rohonyeusi, uongo,uchawa,mihemuko na kutizama upepo unapoelekea na wakati mwingine ulozi.

Natambua Askofu kujishirikisha na mambo hayo ni kazi ngumu na inahitaji utubu Kila wakati maana unaelewa wazi ufanyacho ni dhambi mbaya.

Vile uliitwa na kuagizwa ugombee na tutapewa ubunge iwe jua iwe mvua ilikuwa huna namna maana agizo la mwenyekiti ningumu mno kulikataa hasa ukizingatia nature ya mtu mwenyewe aliyekutaka ugombee ili kufifisha sakata lako na mwanawe Bashite.

Sasa wamekuambia basi lakini wenye akili tutajua wewe ulikuwa wakwanza KUSEMA kwauharamu huu wewe baaasi.

Ulipata topic nzuri na uliongea ukweli mzuri na kwakuwa kawaida hawatakagi ukweli kwanamna yoyote tulijua watakutoa.

Safari hii wamesema vizuri kwamba Ngoma siyako utakosea stepu! Nidhahiri Ngoma Ile si yakuchezwa na Maaskofu na wewe ulilazimishwa, Ile ningoma ya watu waliopoteza hofu ya Mungu na kuwekwa mnatamanio yao mbele.

Rudi uitetee haki, uitetee kweli lakini sana umuhubiri Mungu akomboaye dhidi ya watekaji, ahuishae dhidi ya wauaji, arejeshae dhidi wa wezi na atengenezae dhidi ya waharibifu!!

Kwa mara nyingine HEKO GWAJIMA wewe ni shujaa wa Yesu🙏🏾
 
Back
Top Bottom