Sababu zilizonifanya niache kuendesha gari kwa spidi barabarani, hakuna nilikokua nawahi zaidi ya ushamba, sifa na kuiga

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Maada hii inahusu spidi za kuzunguka mjini na mitaani sio barabara kuu za safari ndefu

Nikiwa mimi ni moja wapo wa waliostaafu hii tabia nimeona niweke huu mjadala, Nakumbuka nlikuwa napenda sana kutembea barabarani na mitaani kwa spidi ambayo watu walilalamika nakimbiza gari na kuweka maisha ya raia hatarini.

Nikaja kugundua kwamba hakuna sehemu nayowahi zaidi zaidi tu ya ushamba wa gari, sifa na kuigana.


Mwaka 2015 (miaka 23) nilienda driving school na nikapewa leseni ya udereva, baada ya hapo nikawa na gari ya kwanza Carina TI nilyoshauriwa na nafundi kwa bajet yangu, niliipenda niliiwekea rim sport, kuweka tint kwenye vioo, mziki mnene, n.k ili tu nionekane 😁😁

kuanzia hapo kila gari niliyokuwa nayo niliipenda sana kwa kuiremba sambamba na kuipa moto / kukimbiza, Ila nikiri wazi tu huu ushamba umeniisha mwaka huu mwezi wa february nilipokuwa nampeleka dada yangu sehemu fulani akawa analalamika kwani nawahi wapi na spidi yangu inampa kizunguzungu, nilimpeleka hio sehemu asubuhi na kumrudisha jioni kwa muda wa wiki mbili.

Nilianza kuona kwakweli spidi niliyozoea kuendeshea gari ipo juu japo mimi niliona kawaida, Nikaona hakuna sehemu nayowahi na nikaona nahatarisha maisha ya watu wanaokatiza barabara hasa watoto.

Kwa sasa spidi yangu nayopenda kutembelea ni haivuki 40 kph na kwenye barabara ya vumbi haizidi 20 ili nisitimue vumbi na kuwachafua raia.

Kwa spidi hii nimeanza kuona raha ya kiendesha gari, akili yote inakuwa inaweza kumudu gari na mazingira ya barabara na kusikiliza muziki bila wasi wasi.

Uendeshaji wa gari kwa spidi kubwa ni hatari kwako na wengine, chukua hatua
 
mmhh mshukuru Mungu hujakutana na ajali tuulize sie kaka..nilishakutana na gari uso kwa uso mambo yenywe ndo kama hayo hayo ushamba na ujinga klichwani na utoto pia ulitawala sana..tena cha kuchekesha ajali ilikuwa ni road ya mtaani kwetu
 
Speed 30? Ata barabara kuu au ni za mitaani? Kama ni mtaani uko sahihi kabisa ila barabara kuu speed ni 50 kwa 80 ingawa sina gari lakini huwa naona vibao njiani
Mkuu ni kwa huku tunakoishi kwenye makazi ya watu kwenye mitaa, huko barabara kuu ni kufumua tu
 
Speed 30 bado una tatizo. Tatizo utalitatua utakapoelewa wapi uendeshe speed gani na kwann.

Kama utaendasha speed 30 barabara isiyo double road unaweza ukasababisha ajali maana unalazimisha kila MTU akuovatake.

Sehemu nilipo kwa sasa ni mbeya, hakuna double roads na kwa hii spidi ipo poa tu, Sijaona usumbufu wa aina yoyote,
 
Back
Top Bottom