Title ingekuwa hivi, sababu za marofa wote kufurahi kukamatwa ndege yao..........Sababu za watanzania wengi kushangilia kukamatwa kwa hii ndege.
1- Tatizo lilianzia kwenye Slogan ya hii Ndege “ HAPA KAZI TU” haikuwa sahihi kwa sababu moja kwa moja inahususisha Chama cha CCM wakat hii ndege n mali ya kila mlipa kodi na sio mali ya CCM. Machon kwa watanzania walio wengi hawana hisia wala mapenz na hizi ndege.
2- Shirika hili CAG haruhusiwi kulikaguwa mahesabu yake, hii n kinyume cha sheria and taratibu za matumiz ya fedha za walipa kodi.
3- Hii ndege kwa nyakati tofauti imetumika kuwapiga vijembe viongoz waliopita au wapinzani kuwakashifu au kuonekana hawakufanya la maana.
4. Kwa nyakati tofaut wataalam wa ndan na wanje walitoa ushauri kuhusu uendeshaji wa shirika la ndege lakin walipuuzwa. Moja ya mahojiano J.K alitamka “ ni vyema kuanza kushughulikia na kutatua matatizo ya shirika la ndege kwanza” akaishia kukashifwa.
5. Sababu za ununuzi au kufufua shirika hili zimekuwa ni kitendawili kisichokuwa na majibu sahihi kwa walipa kodi walio wengi kwa sababu miaka ya nyuma shirika hili lilikuwa likijiendesha kwa hasara na kuacha madeni lukuki yanayotakiwa kulipwa.
Ushauri wangu binafsi kama mlipa kodi niliyechangia senti kufanikisha ununuzi huu, ni vyema shirika hili likaingia ubia na makampuni makubwa yenye uzoefu wa kufanya biashara hii au Serikali iache shirika hili lijiendeshe lenyewe kusiwepo na shinikizo la kisiasa. Ugomvi na makampuni mengine kama Fast Jet au Acacia nk ni vyema kutumika diplomasia kuliko nguvu maana hata sisi tunadaiwa huko nje
Nihitimishe tu kwa kunukuu wahenga “ ukitenda wema utalipwa wema, ukitenda ubaya utalipwa ubaya”