Sababu za uchafu ni pamoja na umasikini

Sababu za uchafu ni pamoja na umasikini

Shoctopus

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
3,435
Reaction score
1,995
Njia nzuri na ya uhakika ya kupambana na uchafu ni kuboresha hali ya maisha ya mwananchi mjini na kijijini.
Na kabla sijaemda mnali nikumbushe maneno ya Mwalimu J. K. Nyerere: "Ili tuendelee tunahitaji Ardhi, Watu, Siasa Safi na Uongozi Bora".
Mwalimu pia alisema: 'Adui wa maendeleo ni Maradhi, Ujinga, na UMASIKINI'
Kwahiyo Serikali ijikite katika kutunga sera na sheria kukabiliana na mambo hayo ya msingi.
Kuna maeneo watu vijijini hawana maji kabisa, achilia mbali maji safi ya kunywa! Halafu unawatoza faini kwa eti kutokuwa na mifuniko ya choo cha shimo! Hata kama ana nyumba lakini hana choo jibu lake ni kumtoza faini tu? Kwanini usijifunze kwanza sababu zinazoweza kufanya watu washindwe kuwa na choo, au wana choo kisichofaa? Wengine hali duni ya maisha inayosababishwa na mambo mengi sio hilo tu unaloona wewe ambalo juujuu au kiurahisi unaona ni ujinga tu?
Ndio maana ya kutaka watu wenye elimu na vyeti halali katika kazi. Na ni lazima iwe pamoja na kazi za uongozi. Bila hivyo baadhi ya watu waliopewa madaraka watadhani uongozi ni kuswaga wananchi kama mifugo.
 
Back
Top Bottom