Sababu za msingi za kumpiga mwenzi wako!

Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,540
13,438
Wana MMU habari za weekend?
Nimeona nianzishe Uzi huu baada ya The Finest kunitafakurisha kwenye Uzi wake "what make u stay"
Ni mara nyingi sana kwa kwa baadhi ya waume kupiga wake zao naomba tujadiliane ni lini, kwa kosa lipi mke anastahili kupigwa! (ni mara chache sana mke kumpiga mume; naomba tusijadiliane hilo)

Pia naomba tuchunguze kwa undani sababu za kijamii zinazompa uhalali wa mume kumpiga mke kama zipo!

Na mwisho, tuchunguze tabia za wanaume hawa ambao hupiga wake zao (wataalamu wa psychology mtusaidie), je wanamitu kinachofanana (have s/thing in common); huenda hii itawasaidia kina dada wanaotaka kuolewa kutambua mapema!

Karibuni kwa michango yenu ya thamani!
 
ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,770
6,521
kikubwa kinachowapelekea kumpiga mwenza wake ni wivu na sifa za kijinga ndio zinapelekea huko..
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,540
13,438
kikubwa kinachowapelekea kumpiga mwenza wake ni wivu na sifa za kijinga ndio zinapelekea huko..

Nakubaliana na wewe; lkn na wanawake pia si huwa na wivu? Au kwakuwa wengi wetu hatuna nguvu za kupigana?
 
TMK DAR

Member
Jul 27, 2011
46
11
HAMNA WAPIGAJI WAZURI KAMA WANAWAKE!
Ila yao it's like a silence killer,na kwa sababu yy ndie kashika zana zote,she can even kill you, si anakuwekea ka cyanide unajikuta umeondoka na anaedelea na raha?
Kupigana nai mambo ya kizamani na haswa kwa watu wasiondelea(mind),rate imeteremka sana.
Lakini kubwa kwa lote ni tabia,mtu ambaye ni violent mke wake anaweza hata kuwa anamletea chai akampiga kwa sababu hakuileta kwa adabu?*?
Hamna sababu ya kumpiga mwanamke maana visababu utakuta mtu anapigwa kwa sababu ya mwili wake au utumwa wa kununuliwa na viji mahali.e.g mtu amekutwa analiwa uroda anapigwa yeye,mtu amekutwa anazungumza na mwanaume(unknown or known to the fam)anapigwa yeye,chakula hakina nyama -kipigo.
Wapiganaji kuna siku utampiga mtu umuue na wewe ndio adios au Keko ya miaka kadhaa:fencing:
Nakubaliana na wewe; lkn na wanawake pia si huwa na wivu? Au kwakuwa wengi wetu hatuna nguvu za kupigana?
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,735
22,971
hakuna uhalali wa kumpiga mke, ni ujinga na ubabe wa kishamba wa baadhi ya wanaume (ambao mara nyingine wanawake wengine wanauendekeza na kulea maradhi)
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,540
13,438
TMK Dar
Nazungumzia phisical violence. Unasema hakuna sababu ya msingi; nakubaliana nawe. Labda tuangalie wanaume wanaowapiga wake zao, do they have something in common? Malezi/ makuzi yao, je wao ni violent hata maofisini, wanajiamini, utendaji wao kwa ujumla!

Tujaribu kuangalia root cause na influencing factors za tabia hiyo!
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,540
13,438
hakuna uhalali wa kumpiga mke, ni ujinga na ubabe wa kishamba wa baadhi ya wanaume (ambao mara nyingine wanawake wengine wanauendekeza na kulea maradhi)

Kwanini wanataka kuonesha ubabe? Ina maana hawajiamini au? Na kama ndivyo hiyo ndiyo njia pekee yakuonesha wako ontop?
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,735
22,971
Kwanini wanataka kuonesha ubabe? Ina maana hawajiamini au? Na kama ndivyo hiyo ndiyo njia pekee yakuonesha wako ontop?

absolutely na ukimkuta mwenye wivu wa kijinga + kutokujiamini kwake, tegemea kipigo kisichoisha!

Ingawa mara nyingine malezi yanangia, mwanaume alokulia nyumba ambayo baba anampiga mama akili yake inajitune kuwa mume kumpiga mke ni kawaida, na mwanamke anadhani kupigwa na mume ni sawa.
 
MUREFU

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,331
348
unajua tatzo la kumpiga mwandan wako au mkeo hutokana na tabia ila siku zote anaesababsha yote haya ni mwanamke mwenyewe. Kwann anasababsha huwa wanapenda kufanya vitu ambavyo umemkanya au mliongea ili mrad aone utachukuwa hatua gan na hapo ndipo unapokuta mwny kukosa uvumilivu anamshushia kipigo.
 
Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
12,077
17,693
Kupiga sio kitu nzuri vyema ni table talk.WANAOPIGA WAKE ZAO BADO HAWAJAZINDUKA KIAKILI na wengi wanaopigwa ni wale magori kipa au hawana kimbilio lingne zaidi ya kumtegemea mume wake ndo maana huwa wanashindwa hata kwenda kuwashitaki wanaume zao. WANAWAKE WENGI WAO WANAOPIGWA NAO HAWAJAZINDUKA KIAKILI
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,474
6,534
unajua tatzo la kumpiga mwandan wako au mkeo hutokana na tabia ila siku zote anaesababsha yote haya ni mwanamke mwenyewe. Kwann anasababsha huwa wanapenda kufanya vitu ambavyo umemkanya au mliongea ili mrad aone utachukuwa hatua gan na hapo ndipo unapokuta mwny kukosa uvumilivu anamshushia kipigo.

Ninaamini kabisa hapo ulikusudia kuandika ILA WAKATI MWINGINE au KUNA WANAWAKE WENGINE.
Maana kwa kuandika hivyo ulivyoandika ni kama unasema siku zote ni wanawake tu wanaokosea na kuwafanya waume zao wawapige.
 
Hivi unajua kuwa mwanamke ni mtu mzima? Anakanywa mtoto mdogo, mtu mzima mnajadiliana! Je ofisini secretary wako akikosea pamoja na kwamba 'umemkanya' unampiga?

Na wewe mf; mkeo akikukanya kunywa pombe na kuchelewa kurudi nyumbani usiposikia akupige?

Maana yangu kila mtu anakwazwa once in a while; je njia rahisi ya kumdispline mtu ni kipigo?

Labda swali la msingi ni kuwa; lengo hasa la kumpiga mwenzio ni nini? Kumrudi, kumkomoa, kumuumiza, kumfundisha au kumaliza Hasira zako?
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,540
13,438
Kupiga sio kitu nzuri vyema ni table talk.WANAOPIGA WAKE ZAO BADO HAWAJAZINDUKA KIAKILI na wengi wanaopigwa ni wale magori kipa au hawana kimbilio lingne zaidi ya kumtegemea mume wake ndo maana huwa wanashindwa hata kwenda kuwashitaki wanaume zao. WANAWAKE WENGI WAO WANAOPIGWA NAO HAWAJAZINDUKA KIAKILI

Lakini wengine ni wafanyakazi, mwanajamii alitupa historia yake kule kwa The Finest; mimi pia nilipigwa sana na kudhalilishwa, nilikuwa na kipato changu kizuri tu. Ila kuna ukweli kuwa wenye uwezo tunaweza kutoka kwenye relation hizo zaidi ya wale wasio na uwezo wa kipato!
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,540
13,438
Ninaamini kabisa hapo ulikusudia kuandika ILA WAKATI MWINGINE au KUNA WANAWAKE WENGINE.
Maana kwa kuandika hivyo ulivyoandika ni kama unasema siku zote ni wanawake tu wanaokosea na kuwafanya waume zao wawapige.

Mj1; hata kama mwanamke kakosea na hakanyiki, ukimpiga ndio atabadilika? Jua mwanamke aliyeolewa ni mtu mzima tayari. Mimi siamini kuwa kipigo ndio fundisho, nashindwa hata kuelezea; lkn kwa mwanaume aliyeniabuse mimi it was insecurity na kujaribu kuprove uanaume wake!
 
MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,474
6,534
Lakini wengine ni wafanyakazi, mwanajamii alitupa historia yake kule kwa The Finest; mimi pia nilipigwa sana na kudhalilishwa, nilikuwa na kipato changu kizuri tu. Ila kuna ukweli kuwa wenye uwezo tunaweza kutoka kwenye relation hizo zaidi ya wale wasio na uwezo wa kipato!

Kaunga, uko sawa kabisa. Kwa hii post yako ninaomba nisiongeze kitu kwani imekamilika. Abuse cuts across haijalishi msomi, tajiri au masikini ikipata nafasi ya kuwa exercised inakuwa. Katika maisha yangu sikuwahikumwona baba yangu akinyanyua mkono kumpiga mama yangu (sijui huko chumbani kwao) na wala sikuwahikufikiria kuwaza kuwa pamoja na 'uelewa wangu kielimu,' iko siku ningekuwa abused na kuvumilia kila kilipokuwa kinatokea hadi kufikia siku ya kusema basi.
Mj1; hata kama mwanamke kakosea na hakanyiki, ukimpiga ndio atabadilika? Jua mwanamke aliyeolewa ni mtu mzima tayari. Mimi siamini kuwa kipigo ndio fundisho, nashindwa hata kuelezea; lkn kwa mwanaume aliyeniabuse mimi it was insecurity na kujaribu kuprove uanaume wake!

Hapo kwenye red hapo kaunga nadhani wapigaji wengi wanaangukia hapo. Kweli kabisa.
 
Rogie

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
7,567
6,610
unazungumzia kumpiga mke kwa vp,say amekosa/amefanya maudhi au basi tu wajisikia kumpiga. wangu alishawahi kuniudhi nilimnasa vibao viwili na later aligundua kuwa ni kweli alikosa. hii nayo utasema ni nn?
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,735
22,971
unajua tatzo la kumpiga mwandan wako au mkeo hutokana na tabia ila siku zote anaesababsha yote haya ni mwanamke mwenyewe. Kwann anasababsha huwa wanapenda kufanya vitu ambavyo umemkanya au mliongea ili mrad aone utachukuwa hatua gan na hapo ndipo unapokuta mwny kukosa uvumilivu anamshushia kipigo.

inawezekana unaamini mwanamke akipigwa ndo anajua kapendwa? Hv unampiga huyo ni mtoto? Na pale mwanaume anapokosea,mwanamke ashushe kipigo au kwa kuwa wao hawana nguvu? Mie nadhani ukimpenda mke/mume na kumthamini huwezi kunyosha mkono wako juu yake, mtazungumza kama watu wazima na kumaliza tofauti. Kumpiga mwenza wako ni dharau ya hali ya juu.

Mwanamke hapigwi ngumi, anapigwa na kitenge tena wax original
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
32,735
22,971
unazungumzia kumpiga mke kwa vp,say amekosa/amefanya maudhi au basi tu wajisikia kumpiga. wangu alishawahi kuniudhi nilimnasa vibao viwili na later aligundua kuwa ni kweli alikosa. hii nayo utasema ni nn?

na mtoto akikosea unamfanya nini? Wewe ukikosea anakulamba makofi?
Wanawake mnaanza kupigwa kdg kdg leo kofi moja kesho mawili mtondogoo ngumi, mwishowe atakucharanga na visu
 
Rogie

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
7,567
6,610
inawezekana unaamini mwanamke akipigwa ndo anajua kapendwa? Hv unampiga huyo ni mtoto? Na pale mwanaume anapokosea,mwanamke ashushe kipigo au kwa kuwa wao hawana nguvu? Mie nadhani ukimpenda mke/mume na kumthamini huwezi kunyosha mkono wako juu yake, mtazungumza kama watu wazima na kumaliza tofauti. Kumpiga mwenza wako ni dharau ya hali ya juu.

Mwanamke hapigwi ngumi, anapigwa na kitenge tena wax original

hapo kwenye red mkuu naona bado unaongelea wanawake wa kipindi cha mama zetu co hawa wa dot.com
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,540
13,438
unazungumzia kumpiga mke kwa vp,say amekosa/amefanya maudhi au basi tu wajisikia kumpiga. wangu alishawahi kuniudhi nilimnasa vibao viwili na later aligundua kuwa ni kweli alikosa. hii nayo utasema ni nn?

Anayekuudhi/aliyekuudhi duniani ni mkeo tu? Mwalimu wako hajawahi kukuonea, utawala wa sasa hujawahi kuudhi? Hujawahi kunyimwa haki zako? Je kwanini huwanasi vibao hao wengine?

Unamnasa kibao mkeo kwakuwa wamliki, au kwakuwa hawezi jidefend? Mimi nakuona weak; n u take all ur trouble to the vulnerable and defendless being like mkeo!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom