SABABU ZA KUHIFADHI ENEO LA KILOMITA 1500

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Eneo la kilomita 1500 ni muhimu sana kwa ikolojia ya Hifadhi ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Eneo hilo ni mazalia ya wanyamapori, vyanzo vya maji kwa ajili ya ikolojia ya Serengeti, Mapitio ya wanyamapori wahamao kutoka Serengeti na Ngorongoro kwenda na kutoka Masai Mara- Kenya. Eneo hilo ni shoroba muhimu iliyobaki katika ikolojia ya Serengeti – Ngorongoro – Masai Mara. Eneo hili linawekewe vigingi na kuhifadhi kwa sababu zifuatazo:-

a. Kuhifadhi mfumo ikolojia wa Serengeti kwa kuwa eneo hili ni mazalia na mapito ya nyumbu wahamao ambao ni kivutio kikuu cha utalii kwa dunia na chanzo kikubwa cha mapato ya Serikali kupitia utalii.

b. Kuhifadhi eneo la mtawanyiko wa wanyamapori hususan nyumbu, pundamilia, swalatomi na pofu.

c. Eneo hilo lina vyanzo vya maji vya mito Grumeti na Pololeti ambayo inachangia zaidi ya nusu ya ustawi wa Hifadhi ya Taifa Serengeti.

d. Tishio kubwa kwa uhifadhi wa wanyamapori katika Loliondo na Hifadhi ya Taifa Serengeti ni ongezeko kubwa la mifugo. Koo zote za Wamaasai katika Loliondo ziko pia upande wa Kenya na wana mahusiano ya karibu sana. Katika mazingira hayo, hakuna Purko, Loita au Latayok wa Loliondo atamzuia Purko, Loita na Latayok wa Kenya sawiya kuingiza mifugo ndani ya WMA na Hifadhi ya Taifa Serengeti. Kwa sababu hiyo WMA haitaweza kudumu kama si kuanza.

e. Katika eneo linalobaki baada ya kubakiza Pori Tengefu Loliondo sheria ya ardhi ya vijiji namba 5 ya mwaka 1999 itumike kutenga na kuweka mipaka ya vijiji. Serikali ikishirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi wenyewe ichukue hatua ya kupanga shughuli za kilimo, ufugaji na makazi kwa mujibu wa Sheria ya Mipango ya Matumizi bora ya ardhi namba 6 ya mwaka 2007.
 
Back
Top Bottom