Sababu za JK kumnyima Samuel Sitta na kumpa Anne Makinda nishani hizi hapa!

Hizi hapa chini ni kashfa za Mkapa. Je, alistahili kupata Nishani ya Msanii!? Sidhani kama hao walionyimwa nishani hizo za kisanii wana kashfa nzito zaidi ya Mkapa.

Kashfa ya kufanya biashara akiwa Ikulu, kashfa ya ununuzi wa ndege ya Rais, helicopters za jeshi na magari ya jeshi, mkataba wa kuingiza Makaburu kutoka RSA na kuwapa management positions pale TANESCO, kashfa ya mkataba wa madini ambapo tunaambulia 3% tu, kashfa ya uuzwaji wa nyumba za Serikali, kashfa ya wizi uliofanywa na Mkapa wa Kiwira Coal Mining, kashfa ya wizi wa EPA, Meremeta na Kagoda ambao hizo zpte zilitokea wakati wa Mkapa na kashfa ya ununuzi wa rada.
 
Sitta kwa maneno yake mwenyewe alisema ni mbinu za mafsad zilizomzuia kuukwaa uspika kwa mara y 2.we unabisha nn?we jamaa kichwa kibovu.so n kama kufukuzwa japo n kwa vtendo tu
 
Nimeshangazwa na kusikitishwa na Kitendo cha Rais JK kumnyima Nishani aliyekuwa Spika wa Bunge tisa Mhe. Samuel Sitta na Kumpa nishani hiyo Spika wa Sasa Anne Makinda ambaye hana vigezo alivyovitaja Rais. Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kuwa hadi sasa, Anne Makinda hamkaribii na wala haoneshi dalili ya kufikia robo ya utendaji wa Samuel Sitta, mbaya zaidi hata mwaka mmoja bado hajamaliza kwenye hicho kiti, huo utendaji uliotukuka kauonyesha lini ilihali hadi sasa ni mauzauza tu???Kama kwa viwango vya Rais, Anne Makinda ni mtendaji bora zaidi ya Sitta, basi ndugu zangu tujue kuwa nchi hii tunajiongoza wenyewe.

Mhe. Samuel Sitta alipoulizwa sababu za kutopata nishani hiyo, alisema kwa sasa asingependa kulizungumzia suala hilo na kusisitiza, "hilo liache kwanza, sitaki kulizungumzia" Aidha, Rais Kikwete aliweka wazi kwamba, nishani hizo zimetolewa kwa Makamu Rais na mawaziri wakuu wastaafu walio hai ama waliokufa, walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madarakani, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao.

Maoni yangu

Kama Fedha za kuwezesha uwepo wa nishani hizi unatokana kodi zetu, nadiriki kusema fedha zetu zimechezewa kwani baadhi ya waliopewa hawana sifa mbele ya Umma ya kupewa nishani hizo zilizotokana na Kodi zetu kwa mfano, Mkapa. Mzee huyu pamoja na kuliongoza Taifa alijimilikisha kifisadi mgodi wa kiwira kupitia kampuni yake na mkewe tena akiwa bado madarakani. Hiyo heshima anayoisema JK huyu mzee anayo anatoka nayo wapi????Nani atamuheshimu kwa wizi alioufanya???Mzee huyu na mtuhumiwa wa ufisadi - Mramba walituingiza mkenge ktk manunuzi ya Rada na mambo mengine mengi ya hovyo hovyo kwa mtu wa hadhi yake kuyafanya. Spika Anne Makinda mara kadhaa amenukuliwa akitaka Posho za wabunge ziongezwe tena kwa hoja za kitoto kabisa za kupanda kwa gharama za maisha huku akijua kuwa Serikali kiuchumi ipo dhohoflihali. Kimsingi huyu mama hana utu na ni mbinafsi, anajijali yeye na tumbo lake. Anapendelea wazi wazi wabunge wa chama chake. Itoshe tu kusema kuwa huyu mama hana sifa za kuwa Spika ila Jinsia yake ndo ilimbeba kama tulivyoambiwa na waliompitisha kugombea nafasi ya uspika.

Kitendo cha Rais kutompa Nishani Mhe. Samuel Sitta, Spika ambaye kwa asilimia kubwa alionyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kuruhusu mijadala ya ufisadi kujadiliwa kwa marefu na mapana yake Bungeni, ni dhahiri kuwa Rais wetu yupo kwa ajili ya mafisadi/wezi wa Rasilimali zetu na sio kwa ajili ya Wananchi. Nlitegemea Rais ampe Sitta nishani kwa moyo wa Uzalendo aliouonyesha akiwa Madarakani. Wataalam wa mambo ya kijamii wanaweza wakahusisha kitendo cha Sitta kunyimwa Nishani, pamoja na kutoteuliwa kugombea Uspika kuwa kinatokana na chuki aliyonayo Rais kwa yale aliyoyafanya Sitta akiwa Spika wa Bunge la Tisa. Kimsingi inaonekana Rais hakupenda yale aliyoyafanya Sitta akiwa Spika.

Kwa kuwaacha watumishi wanaostahili kupata Nishani hizo na kuwapa watu wasio na sifa za kupata nishani hizo. Ni dhahiri kuwa Nishani hizo zimepoteza sifa na kamwe haziwezi kuheshimiwa machoni mwa Watanzania.

Source: Mwananchi 12/12/2011

Ni visasi na kumchanganya Sitta...nadhani labda angetuambia kuwa anampa huyu mama nishani kwasababu ya kujitahidi kulinda maslahi ya chama,na wakati mwingine wasaidizi wa ikulu wawe makini,kuna mambo yanayoonekana ni ya kawaida lakini yanamadhara makubwa sana kwa image ya ikulu..naamini kuna watu walimshauri kuhusu hili...baya zaidi huyu mama katoka kujichanganya kuhusu posho za wabunge,halafu unatuambia kuwa ni mtendaji makini...Nadhani kuna mengi nyuma ya pazia yanayohusu nishani ya huyu mama..na inawezekana kubwa lililomuwezesha ni kufanikisha kuupitisha mswada wa mabadiliko ya katiba kirahisi sana....
 
Sita hakupewa kwa sababu ndiye aliyefanya na kusaidia upinzani kuwa na nguvu sa hivi!bi kiroboto kwa mtazamo wa kikwete ndiye anayestahili kwa sababu ya uamuzi wake wa kukandamiza upinzani!sita ndiye aliyeruhusu mafisadi akiwemo kikwete kujadiliwa kwa kina na kutajwa hadharani katika bungw la tsa na kufanya wapinzani kupata umaarufu,thus hakustahili tuzo.
 
Nimeshangazwa na kusikitishwa na Kitendo cha Rais JK kumnyima Nishani aliyekuwa Spika wa Bunge tisa Mhe. Samuel Sitta na Kumpa nishani hiyo Spika wa Sasa Anne Makinda ambaye hana vigezo alivyovitaja Rais. Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kuwa hadi sasa, Anne Makinda hamkaribii na wala haoneshi dalili ya kufikia robo ya utendaji wa Samuel Sitta, mbaya zaidi hata mwaka mmoja bado hajamaliza kwenye hicho kiti, huo utendaji uliotukuka kauonyesha lini ilihali hadi sasa ni mauzauza tu???Kama kwa viwango vya Rais, Anne Makinda ni mtendaji bora zaidi ya Sitta, basi ndugu zangu tujue kuwa nchi hii tunajiongoza wenyewe.

Mhe. Samuel Sitta alipoulizwa sababu za kutopata nishani hiyo, alisema kwa sasa asingependa kulizungumzia suala hilo na kusisitiza, "hilo liache kwanza, sitaki kulizungumzia" Aidha, Rais Kikwete aliweka wazi kwamba, nishani hizo zimetolewa kwa Makamu Rais na mawaziri wakuu wastaafu walio hai ama waliokufa, walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madarakani, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao.

Maoni yangu

Kama Fedha za kuwezesha uwepo wa nishani hizi unatokana kodi zetu, nadiriki kusema fedha zetu zimechezewa kwani baadhi ya waliopewa hawana sifa mbele ya Umma ya kupewa nishani hizo zilizotokana na Kodi zetu kwa mfano, Mkapa. Mzee huyu pamoja na kuliongoza Taifa alijimilikisha kifisadi mgodi wa kiwira kupitia kampuni yake na mkewe tena akiwa bado madarakani. Hiyo heshima anayoisema JK huyu mzee anayo anatoka nayo wapi????Nani atamuheshimu kwa wizi alioufanya???Mzee huyu na mtuhumiwa wa ufisadi - Mramba walituingiza mkenge ktk manunuzi ya Rada na mambo mengine mengi ya hovyo hovyo kwa mtu wa hadhi yake kuyafanya. Spika Anne Makinda mara kadhaa amenukuliwa akitaka Posho za wabunge ziongezwe tena kwa hoja za kitoto kabisa za kupanda kwa gharama za maisha huku akijua kuwa Serikali kiuchumi ipo dhohoflihali. Kimsingi huyu mama hana utu na ni mbinafsi, anajijali yeye na tumbo lake. Anapendelea wazi wazi wabunge wa chama chake. Itoshe tu kusema kuwa huyu mama hana sifa za kuwa Spika ila Jinsia yake ndo ilimbeba kama tulivyoambiwa na waliompitisha kugombea nafasi ya uspika.

Kitendo cha Rais kutompa Nishani Mhe. Samuel Sitta, Spika ambaye kwa asilimia kubwa alionyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kuruhusu mijadala ya ufisadi kujadiliwa kwa marefu na mapana yake Bungeni, ni dhahiri kuwa Rais wetu yupo kwa ajili ya mafisadi/wezi wa Rasilimali zetu na sio kwa ajili ya Wananchi. Nlitegemea Rais ampe Sitta nishani kwa moyo wa Uzalendo aliouonyesha akiwa Madarakani. Wataalam wa mambo ya kijamii wanaweza wakahusisha kitendo cha Sitta kunyimwa Nishani, pamoja na kutoteuliwa kugombea Uspika kuwa kinatokana na chuki aliyonayo Rais kwa yale aliyoyafanya Sitta akiwa Spika wa Bunge la Tisa. Kimsingi inaonekana Rais hakupenda yale aliyoyafanya Sitta akiwa Spika.

Kwa kuwaacha watumishi wanaostahili kupata Nishani hizo na kuwapa watu wasio na sifa za kupata nishani hizo. Ni dhahiri kuwa Nishani hizo zimepoteza sifa na kamwe haziwezi kuheshimiwa machoni mwa Watanzania.

Source: Mwananchi 12/12/2011
Rais fake, nishani zake fake, mawazo yake fake, uwezo wake fake! Makinda kapewa nishani kwa sababu amepitisha mchakato wa katiba kama alivyoagizwa. Na bado mtasikia mengi kwa bibi huyu kufanyiwa kwani aliyemweka anataka awaambie watz kuwa mama huyu ni chaguo sahihi hata kama wanaona tofauti. Hongera JK kuendelea kuibomoa ccm, na bado subirini JK atasaini posho hiviya wabunge hivi karibuni kuidhinisha yale aliyofanya Makinda. Pole watz
 
sita ni mkristo tena mlutheri,
Tuzo yake atapewa na Mungu siku ya mwisho mwacheni mzee wa watu apumzike.
 
Huyo jamaa yetu nina wasiwasi na shule yake kwa alipitapita je,make kila anachokifanya kina kuwa tofauti kabisa na kiwango cha elimu yake. Ila jibu ni kwamba huyu binadamu ana chuki binafsi au amesoma lkn kuelimika ndo imekuwa ngumu kweli.Jamani anaboa huyu mtemi wetu JK.
 
natafuta joke mtu aliyenayo anipostie... Ni ile ya mashindano ya wanasayansi ambayo Tz ilishiriki. Nasi tukatia fora. Baada ya mtoto aliyezaliwa bila kichwa, na wanasayansi wa kibongo wakamwekea nazi badala yake na leo ni kiongozi mkubwa wa Taifa letu!

nimekukubali mkuu!
 
Je, katika utumishi uliotukuka ni wanasiasa tu ndio wanastahili kweli? Mbona kuna wanajeshi wana mchango mkubwa katika historia ya nchi yetu? Je wao waendelee kumeza mate bila nishani kwa mchango wao wa kujitoa mhanga na kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya nchi hii kweli? Nadhani hawajafurahi... Hivi Msuguri bado yupo hai? Kiaro? ...!!!!! Ama kweli mishangao haitakoma ktk Tanzania ya miaka 50 na siku 3
 
:hatari:mpaka leo bado haujajua hatuna KIONGOZ??TULIE NAYE NAMFANANISHA NA BI KIREMBWE...HAYA NI MADUDU YAKE YA MWISHO MWISHO..Lakini nahis wanajuana
 
kwa lugha nyepesi na isiyo na mkwaruzo NISHANI ZIMETOLEWA KIUPENDELEO NA KUANGALIANA SURA
 
unapopima akili ya mtoa nishani na kutoa majibu kuwa haina akili vipi akili ya aliyemzuia asiye na akili kuaibika bungeni..je naye hana akili?mi nadhani hapa wote hawana akili..yaani wanafikiri kwa tumbo...MTOA NISHANI NA ALIYENYIMWA{MR. SIX}WOTE MATATIZO KATIKA NCHI
 
Back
Top Bottom