Sababu za JK kumnyima Samuel Sitta na kumpa Anne Makinda nishani hizi hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu za JK kumnyima Samuel Sitta na kumpa Anne Makinda nishani hizi hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Dec 12, 2011.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Nimeshangazwa na kusikitishwa na Kitendo cha Rais JK kumnyima Nishani aliyekuwa Spika wa Bunge tisa Mhe. Samuel Sitta na Kumpa nishani hiyo Spika wa Sasa Anne Makinda ambaye hana vigezo alivyovitaja Rais.

  Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kuwa hadi sasa, Anne Makinda hamkaribii na wala haoneshi dalili ya kufikia robo ya utendaji wa Samuel Sitta, mbaya zaidi hata mwaka mmoja bado hajamaliza kwenye hicho kiti, huo utendaji uliotukuka kauonyesha lini ilihali hadi sasa ni mauzauza tu?

  Kama kwa viwango vya Rais, Anne Makinda ni mtendaji bora zaidi ya Sitta, basi ndugu zangu tujue kuwa nchi hii tunajiongoza wenyewe.

  Mhe. Samuel Sitta alipoulizwa sababu za kutopata nishani hiyo, alisema kwa sasa asingependa kulizungumzia suala hilo na kusisitiza, "hilo liache kwanza, sitaki kulizungumzia" Aidha, Rais Kikwete aliweka wazi kwamba, nishani hizo zimetolewa kwa Makamu Rais na mawaziri wakuu wastaafu walio hai ama waliokufa, walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madarakani, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao.

  Maoni yangu

  Kama Fedha za kuwezesha uwepo wa nishani hizi unatokana kodi zetu, nadiriki kusema fedha zetu zimechezewa kwani baadhi ya waliopewa hawana sifa mbele ya Umma ya kupewa nishani hizo zilizotokana na Kodi zetu kwa mfano, Mkapa. Mzee huyu pamoja na kuliongoza Taifa alijimilikisha kifisadi mgodi wa kiwira kupitia kampuni yake na mkewe tena akiwa bado madarakani. Hiyo heshima anayoisema JK huyu mzee anayo anatoka nayo wapi????Nani atamuheshimu kwa wizi alioufanya??

  Mzee huyu na mtuhumiwa wa ufisadi - Mramba walituingiza mkenge ktk manunuzi ya Rada na mambo mengine mengi ya hovyo hovyo kwa mtu wa hadhi yake kuyafanya. Spika Anne Makinda mara kadhaa amenukuliwa akitaka Posho za wabunge ziongezwe tena kwa hoja za kitoto kabisa za kupanda kwa gharama za maisha huku akijua kuwa Serikali kiuchumi ipo dhohoflihali.

  Kimsingi huyu mama hana utu na ni mbinafsi, anajijali yeye na tumbo lake. Anapendelea wazi wazi wabunge wa chama chake. Itoshe tu kusema kuwa huyu mama hana sifa za kuwa Spika ila Jinsia yake ndo ilimbeba kama tulivyoambiwa na waliompitisha kugombea nafasi ya uspika.

  Kitendo cha Rais kutompa Nishani Mhe. Samuel Sitta, Spika ambaye kwa asilimia kubwa alionyesha uzalendo wa hali ya juu kwa kuruhusu mijadala ya ufisadi kujadiliwa kwa marefu na mapana yake Bungeni, ni dhahiri kuwa Rais wetu yupo kwa ajili ya mafisadi/wezi wa Rasilimali zetu na sio kwa ajili ya Wananchi.

  Nlitegemea Rais ampe Sitta nishani kwa moyo wa Uzalendo aliouonyesha akiwa Madarakani. Wataalam wa mambo ya kijamii wanaweza wakahusisha kitendo cha Sitta kunyimwa Nishani, pamoja na kutoteuliwa kugombea Uspika kuwa kinatokana na chuki aliyonayo Rais kwa yale aliyoyafanya Sitta akiwa Spika wa Bunge la Tisa. Kimsingi inaonekana Rais hakupenda yale aliyoyafanya Sitta akiwa Spika.

  Kwa kuwaacha watumishi wanaostahili kupata Nishani hizo na kuwapa watu wasio na sifa za kupata nishani hizo. Ni dhahiri kuwa Nishani hizo zimepoteza sifa na kamwe haziwezi kuheshimiwa machoni mwa Watanzania.

  Source: Mwananchi 12/12/2011
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mama Makinda ni mwanafunzi wa Uspika kwa Mhe Samuel Sitta, STANDARDS AND SPEED, aliyegawiwa nishani ya taifa kumpongeza kufeli kwake kuhifadhi mafunzo aliyoyapata juu ya jinsi ya kuendesha bunge la vyama vingi bila itikadi za kisiasa.

  Hivyo, mwanafunzi yeyote wa uspika atakayetokana na huyu mama hivi sasa huenda naye asitufae huko tuendako.
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Je ni kwa nini wanapewa wanasiasa tu! Je watanzania wengine wanaochangia kwa pesa yao au wanaojitolea kwenye mambo mengine ni vipi?
   
 4. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mama Makinda na Nishani wapi na wapi? Wampatie Mheshimiwa Tundu Lissu hiyo Nishani!
   
 5. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtoa tuzo uwezo wake wa kufikiria tuuchunguze, unatia mashaka!
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hizi nishani zitaendelea kukigawa chama zaidi
   
 7. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Yaani huyu baba au ni kilaza wa hali ya juu, au ni jeuri wa kupindukia na hajali kuhusu reputition yake. Kwa mtu yeyote mwenye busara kuliko kuchagua watata ni bora angeacha the whole thing.

  Sidhani kama kutoa Tuzo ilikuwa ni Jambo la maana sana; vitu vya msingi, kama kutoa dira/vision ya miaka mingine 50, wala haikumungia akilini!
  Pffuuueeewwww
   
 8. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ilikuwa zamu ya spika wa kike kupata nishani hamuelewi nini?
   
 9. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  anajitahidi kuwawezesha wanawake, ila ningefurahi kama wanawake nao wangechangia hii mada kuona wanazungumzaje juu ya hili, kiufupi wale wote waliostahili kupewa nishani hii wamekuwa wakiilalamikia serikali ya awamu ya nne kwa utendaji mbovu labda ndio imepelekea wao kutotunukiwa
   
 10. k

  kayumba JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Umenena, mkuu!
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hakuna nishani ya MTEI wa chadema walioachwa na kikwete wanaweza kutunukiwa hii
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  misukosuko ya Siita na Lowassa ndani ya taifa hili inatosha kuwanyima nishani kama kipimo kitaanzia kwenye vyama vyao vya siasa
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  chama ndicho kinakupa nafasi ya uongozi kama kinaona hujakiwakilisha vema hakina sababu ya kukupa nishani. suala la msingi viongozi hao wanaweza kupewa nishani hata na vyama vya upinzani kama vinaona Siita au Lowassa wanastahili.
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Nishani zimekaa kiushikaji zaidi halafu hizo nishani wanataka kutuaminisha kuwa hakuna watu waliofanya mambo makubwa nje ya CCM au hakuna watu ambao hawako CCM na wanastahili kupata hizo nishani?
   
 15. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #15
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo ndio ninapopataka mimi haswaaaa.
   
 16. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #16
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Lowassa kafukuzwa uwaziri Mkuu na sitta kafukuzwa uspika leo mnajiuliza kwa nini wamekosa nishani ni fikra mgando hizo wakati suala liko wazi
   
 17. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #17
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Misukosuko ipi kaipata Sitta?...labda kama unataka kusema kuonesha nia yake ya kuutaka Urais ndio inamfanya asipate hiyo nishani hapo kidogo nitaelewa
   
 18. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #18
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mbowe na Dr salaa inakuaje wamekosa nishani
   
 19. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #19
  Dec 12, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  natafuta joke mtu aliyenayo anipostie... Ni ile ya mashindano ya wanasayansi ambayo Tz ilishiriki. Nasi tukatia fora. Baada ya mtoto aliyezaliwa bila kichwa, na wanasayansi wa kibongo wakamwekea nazi badala yake na leo ni kiongozi mkubwa wa Taifa letu!
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  You must be out of your freakin mind...ni lini Sitta alifukuzwa uspika ukiwa hauna uhakika na unachoongea ni bora kukaa kimya kuliko kuonekana katuni mbele ya watu
   
Loading...