Sababu ya wanaume kutoka nje ya ndoa

Sababu ya wanaume kutoka nje ya ndoa

mtzmweusi

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
8,700
Reaction score
9,070
Wana mmu habari zenu,mie nimefanya karesearch na nimegundua kuwa moja ya sababu tena kubwa inayowafanya wanaume kutoka nje ya ndoa zao ni hii,wanawake wengi huwa wanaonyesha mapenzi sana kwa waume zao ila wakishazaa mtoto mapenzi huamishia kwa mtoto yani anakuwa hana time nawewe kbsaa hivyo hupelekea wanaume wakatafute huko hicho wanachokikosa
 
Mimi nadhani ni shatani tu huwa anawapitia wanaume lakini kiukweli wanaume ni watu waaminifu sana kwenye ndoa zao

(hapo vipi!!)
 
Unataka justification ya kutoka nje ya ndoa nini mkuu, wewe toka tu usitafute sababu, eti mwanamke akishazaa mapenzi anahamishia kwa mtoto, inamaana ukimuomba hakupi, hafui nguo, jaribu na wewe siku moya kukaa na mtoto.
 
hii tabia ya kutoka nje ya ndoa jamani nionavyo mimi ni TABIA NA HULKA BINAFSI ZA MHUSIKA....waweza kumpenda sana hata km una watoto lakini akiamua tu na kiranga chake basi huyoooooooo humuoniiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!ni kuombeana tu kwa kweli.
 
Sikubaliani na mtoa hoja. Akili ya mwanadamu hufanya kile anachofikiri ndiyo maana ukiamini kwamba mapenzi yatahamia kwa mtoto basi utatoka tu nje ya ndoa. Pole kama umetoka.
 
ni kautamaduni u wanaume wamajiwekea wala si hiyo kitu kingine::: kuna wanawake wanaonyesha mapenzi kwa mumewe, na ukiambiwa mumewe anaweza toka nje na watoto wasiojua kuoga vizuri bado. uwezi amini.....ni tabia ya mtu na kautamaduni tu...
 
Na hili la kutoka nje mke anapokuwa mjamzito sababu ni nini?

Sent from my iPad using JamiiForums mobile app
 
mi nadhani ni tabia tu ya mume mwenyewe maana kuwa na mtoto haiingiliani na mapenzi yao
 
Sababu ni ukosefu wa adabu tu hakuna lingine, mwanaume mwenye adabu zake haweza kufanya hayo, lazima atamfanyia heshima mke wake na watoto zake.
 
Huwa wanasahau kama na sisi ni watoto pia tunataka kuveshwa nepi
 
hii tabia ya kutoka nje ya ndoa jamani nionavyo mimi ni TABIA NA HULKA BINAFSI ZA MHUSIKA....waweza kumpenda sana hata km una watoto lakini akiamua tu na kiranga chake basi huyoooooooo humuoniiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!ni kuombeana tu kwa kweli.
user-online.png
mtzmweusi

Nakubaliana nawe... ni tabia na hulka za wanaume wengi kama siyo wachache... Onaaaa!!
man.jpg

Bwana anakila kitu mezani lakini Mmmmh hatulii!
user-online.png
mtzmweusi
 
Mimi nadhani ni shatani tu huwa anawapitia wanaume lakini kiukweli wanaume ni watu waaminifu sana kwenye ndoa zao

(hapo vipi!!)

Msimsingizie shetani.........mbona huyo Shetani hakutumi ukaibe Benki

anakutuma kuparamia papuchi tu
 
..halafu tabia ya kudai mke anakuwa busy na watoto ndio ikupe uhalali wakufanya madudu mbaya sana, kwani wakati yeye yupo busy na malezi wewe unashindwa hata kuonesha support yako kwake kwa kitu hicho ambacho pia ni kigeni kwake??! mambo gani haya?!
 
Si wakati wote. hii yaweza tu kuchochoe tabia ya uzinzi wa mtu.chamsingi ni akina dada na mam zetu kujitahidi kuonesha kamakwelu bado unampenda mumeo hata baada ya kuzaa,na hapa zaidi ni usafi mana wakati wa kunyonyesha kama mwanamke hayuko makini kwa usafi anaweza kupunguza mvuto kwa mumewe ,ni hayo tu kwa sasa.
 
Unataka justification ya kutoka nje ya ndoa nini mkuu, wewe toka tu usitafute sababu, eti mwanamke akishazaa mapenzi anahamishia kwa mtoto, inamaana ukimuomba hakupi, hafui nguo, jaribu na wewe siku moya kukaa na mtoto.

Mke wako unamuomba! Kivipi? Haya makubwa!!!!!
 
Hii mimi naipinga. Mtoto akizaliwa kiukweli mama ana kazi kubwa sio tu kiulezi ila baiolojia ya kuwa karibu na kumlisha mtoto.

Amini nakwambia kama mama asipokuwepo mtoto anapata tabu sana kwenye makuzi yake.

Mimi na mke wangu tuna katoto kadogo tu na kusema ukweli kanachukua airtime ya kutosha. Tunafanyaje??

Mimi nimejiweka kwenye mazingira ya kiutoto. So mke wangu ana watoto wawili! Mimi mkubwa, na mtoto wetu mdogo. So kama mtoto akinyonyeshwa, mimi natania(utani very constructive) kuwa na mimi nataka ninyonyeshwe, pia sisi watoto kila mmoja ana nyonyo yake, so nikikuta dogo ananyonyeshwa ziwa langu kimbembe(kiutani).

Kufanya hivi kunaleta mshikamano na umoja. Issue ya kutoka nje ya ndoa ni HULKA na TAMAA za mtu. Embu jaribu kufikiria wakati unafanya huo uasherati mtoto wako anakuangaliaje? Unataka awe na maisha mazuri au awe muasherati pia?

Fikiria kama mama akiamua pia kumuacha mtoto na kufanya uasherati?

Shiriki na mama katika malezi na makuzi ya mtoto. Tendo la ndoa lipo na muda upo kabisa, fanya kadiri inavyowezekana ila kama hali ya kiafya na kisaikolojia ya mama hairuhusu kuwa mpole. Afterall HAUTAKUFA!
 
..halafu tabia ya kudai mke anakuwa busy na watoto ndio ikupe uhalali wakufanya madudu mbaya sana, kwani wakati yeye yupo busy na malezi wewe unashindwa hata kuonesha support yako kwake kwa kitu hicho ambacho pia ni kigeni kwake??! mambo gani haya?!
Exactly na mtoto ni wa wote...badi na ubini ni wa baba (Man) ...hii hulka!
 
Back
Top Bottom