Sababu ya mishahara serikalini kuchelewa hii hapa

Sababu ya mishahara serikalini kuchelewa hii hapa

bomouwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,149
Reaction score
800
Kwa wafanyakazi wa serikali mpaka leo hii tar2 bado hawajapata mishahara yao.. lakini katika kufanya uchunguzi usio rasminimegundua ya kua WENYE AKAUNTI ZA CRDB wao walishapata tangu ijumaa ya tar29 na wengi wanaolalamika kutopata mishahara hawa ni wale wa benki ya NMB ingawa sijajua kama NBC wamepewa..
ushauri ni kwamba, kwakua crdb imeshachukua tenda ya kugawa mishahara ya serikali kwa hiyo ni muhimu kwa mliopeleka akaunti zenu za mabenki mengine kwa ofisi ya mishahara sasa mkabadili na mfungue akaunti mpya CRDB ili mishahara ipatikane kwa uhakika.
 
Mjumbe hauwawi.. salama wote? wale wahanga wakukosa mshahara wa mwezi wa nane hii sasa ni mpya walahiii.... nlikua mahali fulani kufanya mambo yangu bahati mbaya nkasikia watu wawili wanaongea kua hazina imelazimika kutoa fungu kulipeleka mjengoni kulipa waheshimiwa wanaolala wakati huohuo wakiwaacha walalahoi walale hoi kwelikweli... nyie mliosehemu nyeti (sio za mwili) namaanisha ndani ya system, hii habari ipo kweli?
 
Mara wengine wanadai CRDB ndo wamesababisha, wengine wanadai ni mminyo wa mishahara hewa, hili la dodoma nalo ni lingine
 
tatizo je, watumishi wametaarifiwa sababu?
 
kwa wafanyakazi wa serikali mpaka leo hii tar2 bado hawajapata mishahara yao.. Lakini katika kufanya uchunguzi usio rasminimegundua ya kua wenye akaunti za crdb wao walishapata tangu ijumaa ya tar29 na wengi wanaolalamika kutopata mishahara hawa ni wale wa benki ya nmb ingawa sijajua kama nbc wamepewa..
Ushauri ni kwamba, kwakua crdb imeshachukua tenda ya kugawa mishahara ya serikali kwa hiyo ni muhimu kwa mliopeleka akaunti zenu za mabenki mengine kwa ofisi ya mishahara sasa mkabadili na mfungue akaunti mpya crdb ili mishahara ipatikane kwa uhakika.

acha uongo wewe
mimi napokelea mshahara nmb na tar 28 jioni saa 12:30 pesa imeingia
 
acha uongo wewe
mimi napokelea mshahara nmb na tar 28 jioni saa 12:30 pesa imeingia

Rafiki wewe ndiye muongo. Mimi nina account crdb mpaka sasa sijapata
 
acha uongo wewe
mimi napokelea mshahara nmb na tar 28 jioni saa 12:30 pesa imeingia

wewe unamatatizo ya akili na hauko sawa bila shaka.watu wanapozungumza mambo ya ukweli kwa mustakabali wa familia zao na maisha yao usilete utani kabisa... usiseme watu waongo wakati watumishi wengi wa serikali hawajapata mishahara na humu tunaongea haya ili tujuzane.sasa uwe na busara ya maneno yako.
 
Wewe ndo unamatatizo,,jamaa kasema mshahara uliingia tarehe 28 wewe unambishia. Asa tumuamini nani, wewe au yeye ambaye hela iliingia.?
 
Sisi wa sekta binafsi tunashangaa tu...mweh! Poleni wakuu
 
Wewe ndo unamatatizo,,jamaa kasema mshahara uliingia tarehe 28 wewe unambishia. Asa tumuamini nani, wewe au yeye ambaye hela iliingia.?

nyehunge... swala la msingi hapa ni jamaa kusema hii mambo ni "uongo" wakati watu kibao kwenye mawizara mengi bado mpaka leo, sasa kama amepata ni sawa sijakataa ila nimemkatalia kusema uongo kwamba kwakua yeye kapata basi na wengine wamepata. nawasilisha
 
acha uongo wewe
mimi napokelea mshahara nmb na tar 28 jioni saa 12:30 pesa imeingia

We c mwanajeshi ndo maana.. Sisi sio wanajeshi

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom