Sababu ya Miji yetu kuwa michafu nini?

mikimba

Member
Oct 20, 2010
6
0
Nimetembelea miji mingi ya tanzania lakini watu wake wana tabia ya Kuenzi uchafu.Dar-es-Salaam mtu mtanashati anaendesha gari anakunywa maji anatupa chupa barabarani.Mtu haoni aibu anatupa takatakata na watu wanamwangalia,Ukifika kigari kwa tabia ya watanzania mtafungwa kule kila jumanne barabara zote zinafagiliwa,Kanali Massawe amejifunza toka huko naamini Mji wa Bukoba ataurekebisha.Kutokana na tabia ya uchafu wa watanzania sioni faida ya kuadhimisha miaka 50 ya uchafu.Au wana JF mnasemaje? ,vipo visheria vingi mjini lakini havitumiki.Mara ukitupa uchafu faini shillingi 50,000/-lakini yote usanii.Miji yote inasheria lakini watekelezaji ni kama majua.
 

kibali

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
504
420
Kwa Tanzania mji wa Moshi wanajitahidi sana,ni msafi na hakuna anayetupa takataka ovyo maana fine ni nje nje,watchmen wako mpaka juu ya miti,moshi wanastahili pongezi
 

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,735
9,119
Watu hawana ustaarabu kabisa. Wengine wanaharibu hali ya hewa kwa kujamba.
 

kikahe

JF-Expert Member
May 23, 2009
1,350
280
Sababu ywa kwanza ni uchafu wa wakazi wenyewe na pili uzembe wa viongozi wa miji husika.
wapelekwe attachment MOSHI wakajifunze.
 

mteule

Senior Member
Aug 2, 2007
132
216
katika pita pita nilikutana na survey ya miji michafu duniani, nikakuta dar es salaam, jiji linalokaribisha kila mgeni ni jiji la nane (8) kwa uchafu.
 

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
3,964
1,876
Tangu biashara ya mifuko ya rambo na hizi chupa za maji zianze basi jiji likaaanza kuwa chafu hadi leo. nakumbuka miaka ya nyuma jiji lilikuwa safi kabisa!
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
74,134
75,090
Waislaam tunafundishwa kuwa unadhifu ni kutokana na iman "Annadhafa minnal Imaan"

Watu hawana iman ndio maana unaona uchafu unazidi.

Mpaka mtu unakirihika, nyumba zinajengwa bila mpango, mifereji imejaa taka na maji machafu, mijitu inakojowa hovyo barabarani.

Sababu moja kubwa ni mijitu mingi imehamia mijini kutoka maporini ambako hamna vyoo, hamna kanuni, hamna ustaarabu. Wengine viatu mpaka waje mjini ndio wanaanza kuvaa.

Shule hazifundishi?

Zamani Dar. Haikuwa hivi (kabla ya 80's). Palikuwa pasafi sana tu.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,908
287,685
Sababu Watanzania wengi wana tabia ya uchafu, vinginevyo wasingekubali hali ilivyo katika miji yetu mingi na hivyo kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha miji yetu inakuwa misafi kama miji ya wenzetu. Tumeridhika na mifereji iliyoziba na hadi kutoa harufu kali ya kutisha na kuwa maeneo ya mbu kuzaliana na pia kuwa chanzo kikuu cha kipindupindu na magonjwa mbali mbali ya tumbo yanayosababishwa na uchafu. Hatujali kutupa uchafu barabarani hovyohovyo kama tunakula ndizi, karanga, machungwa, machenza n.k. tunatupa hovyo tu na matokeo yake ndiyo hayo ya miji yetu kuwa katika uchafu uliokithiri.
 

SOBY

JF-Expert Member
Sep 19, 2011
1,268
456
Watanzania tuna tabia ya uchafu!!
Sio miji tu, vikwapa na nywele za kichwani huwa hatujali. Hasa madume, tunaona usela ndio dili.
We don't take care of ourselves, ukienda kupata manicure/pedicure saloon unaonekana shoga.
Hali ya hewa ya Dar inahitaji hygiene ya nguvu sana!!... let's change ndugu zangu.
 

Tidito L

Member
Jan 23, 2011
97
15
Kwa Tanzania mji wa Moshi wanajitahidi sana,ni msafi na hakuna anayetupa takataka ovyo maana fine ni nje nje,watchmen wako mpaka juu ya miti,moshi wanastahili pongezi
Acha sifa za uongo wewe mi niko uko pa safi ni ka parts kamoja toka stend njoo mawenzi road basi, njoo mbuyuni uone na kule dar street na kwingine kwingi.
Jingine population ya moshi ni ndogo mno.
Sema %kubwa ya wtz wanatembea wakia na stress kubwa k'babu ya serikari yao,hawatendei haki.
 

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,175
8,111
Nimetembelea miji mingi ya tanzania lakini watu wake wana tabia ya Kuenzi uchafu.Dar-es-Salaam mtu mtanashati anaendesha gari anakunywa maji anatupa chupa barabarani.Mtu haoni aibu anatupa takatakata na watu wanamwangalia,Ukifika kigari kwa tabia ya watanzania mtafungwa kule kila jumanne barabara zote zinafagiliwa,Kanali Massawe amejifunza toka huko naamini Mji wa Bukoba ataurekebisha.Kutokana na tabia ya uchafu wa watanzania sioni faida ya kuadhimisha miaka 50 ya uchafu.Au wana JF mnasemaje? ,vipo visheria vingi mjini lakini havitumiki.Mara ukitupa uchafu faini shillingi 50,000/-lakini yote usanii.Miji yote inasheria lakini watekelezaji ni kama majua.

WHAAAAT?! Barabarani? mbona umeenda mbali banaa!! Huko kwenye ma-gheto yetu kwenyewe ni shaghalabaghara; nini mitaani!!! gheto ni full mifuko ya plastic iliyokuwa imebebea chips mayai; vikasha vya take away, chupa tupu za uhai water, magazet na vigazet vya udaku, viatu vilivyotupwa huku na kule, soksi zilizogaa hovyo, mabeseni yaliyojaa maji machafu na vyombo vinavyonuka, na matakataka mengine kwa kwenda mbele! BISHENI?!
 

Songambele

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
4,613
2,419
watu wengi wanaosababisha uzalishaji mkubwa bila miundombinu ya kuhifadhi taka, kukosekana ustaarabu vichwani mwa watu.
Watu wanagombania kila kitu na kupenda kuongozwa.
Daladala wanagombea jitu limefika mwisho linataka liwe la kwanza kuhudumiwa. Ujenzi holela ndio chanzo kikubwa zamani masaki nyumba ndio zilizokuwa za kupigiwa mfano kila nyumba inakizimba cha taka uswahilini tulikuwa tunchimba mashimo sasa mtu kibao
 

TONGONI

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
1,041
373
Mkuu kweli umenena miji yetu michafu tena ni michafu balaa sababu,inasikitisha mpaka leo unakuta mijitu I'm sorry to say mijitu but to be honest ni mijitu,iko madaraka na wanajukumu la afya lakini mpaka leo bado tuna kaa na vinyesi majumbani,bado mpaka leo tuna vumbika vinyesi kwente nyumba zetu,pesa nyingi zinatumika kwenye miradi ya malaria lakini hakuna anayejali au kuona chanzo kikubwa ni mfomu wa vyoo tunavyo tumia,ukienda masoko ya nyama na samaki utadhani ndio kuna miradi ya kufuga nyuki kwa nzi,sikwambii siku kukiwa na mvua...Tazama barabara za mijini zilivyojaa mchanga,mifereji ya maji machafu tumegeuza ndio sehemu za kutupia taka,miji yetu usiku inatisha hata taa moja moja barabarani hakuna,yani hata sijui inakuwaje mambo haya!​
 

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,796
2,728
Kwa kifupi ni kwamba sisi Watanzania ni waigizaji wazuri sana wa mambo mabaya mathalani mambo yote ya nchi za wenezetu lkama vile kuvaa nguo fupi au niseme kutembea uchi, sasa hivi picha za mambo ya kutisha sisi sasa tunauana kama kuku, miziki yetu ya zamani imeuawa na western music, wajomba zetu wenyewe safari sana huko huko na mambo mengine. Tuliloshindwa kuiga ni ile tabia ya USAFI walionayo wazungu hilo sisi hatutaki kabisaaaaaa. Nadhani tunatakiwa kuwa na VIONGOZI wenye karama za uongozi kwani sasa hivi tuna viongozi UCHWARA hawajui wajibu wao kwa wananchi wanao waongoza. Utakuta kiongozi anaongozwa na watu wake hata katika vikao.
 

TOWNSEND

JF-Expert Member
May 8, 2011
2,598
460
miji pia inavyopangwa vibaya unachangia uchafu na hatuna wazimamizi yaani viongozi kama zama zile tizama miji ya zamani ilivyopangwa na wakoloni sio tabu kuchimba shimo la taka sehemu yako, lakini leo wanapima viwanja vidogo utafikiri tupo palestina au jerusalem
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom