Sasa kama baadhi ya mifumo ime paralyze unataka rais akae kimya?.Hayo matatizo yote unafikiri muarobaini wa kuyaondoa ni Rais Magufuli tu???
Ni kwa misingi hiyo ya kumuamini fulani, kero za watu wengi wanazielekeza kwake kama vile hakuna viongozi wengine na hii si afya ktk utalawa sababu tutatengeneza 'one man show system' hatufanyi kazi kimfumo bali tunafanya kazi kimaagizo toka juu.
Yoyote utakaye teuliwa hatoonekana anafaaa km vile Rais, watu wanataka kusikia kauli ya Rais tu sio ya waziri ama mtu mwingine ambaye hata Rais amempa dhamana, maana kutokana na uteuzi na utenguzi usio na kikomo yawezekana imejengeka dhana miongoni mwa wananchi kwamba wateuliwa wanamuangusha Rais, sasa wananchi wanaona twende kwa Rais tu.
Anayeteua anaonekana siku zote yupo sahihi na wanaotenguliwa ambao kimsingi wamepewa brand name 'majipu' ndo tatizo, kwa akili ya kawaida ukisikia daktari anatumbua jipu ni lazma uone anafanya la maana sana hata kama wakati mwingine hatuelezwi sababu ya uteuzi na utenguzi ama huu utumbuaji kama unavyoitwa ila tunashangilia tu.
Tusitarajie ubunifu sababu kila anayeteuliwa anataka 'ku maintain status quo'.
Rais akifanya ziara ya kushtukiza utasikia na viongozi wa mikoa nao wanafanya ziara hizo.
Rais akitumbua na viongozi wa mikoa huku wanatambua.
Rais akikaa na makundi ya watu kama wafanyabiashara, viongizi wa dini nk utasikia mkuu was mkoa amewaita wasanii wote kwenye mkoa.
Kuna mtu aliwahi sema tuna viongozi wengi mabeki kuliko washambuliaji, akimaanisha wengi wanaowaza kulinda nafasi zao kuliko kuleta tija ya mafanikio.
Lengo la haya yote ni kuendena na kasi, kipimo cha utendaji mzuri wa kiongozi ni kuendana na kasi ya Rais na kufanya anayofanya, ubunifu ni ndoto ktk style hii.
Yote haya yanatokea ktk serikali inayohubiri uzalendo lakini utasikia sana ktk muktadha ama hadhara ya uma usio wa kiitikadi, vingozi wakisema, "serikali ya Magufuli", "serikali ya chama cha Mapinduzi" badala ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Mara ngapi umemsikia rais akilalamika kuhusu viongozi anaowateua kutokuchukua actions kwa issues ndogo ndogo tu. Kwa kifupi serikalini kuna uzembe mkubwa sana wa utendaji kazi kuanzia ngazi za juu hadi chini. Nazungumza from the experience kwani nimefanya kazi private sector na Government pia. Serikalini hamna kuwajibishana mtu aki underperform. Tofauti na private ambapo uki underperfom unawekwa pembeni.