Sababu ya mambo kubaki 'Kama kawaida' pamoja na teua/tengua, maelekezo, maelezo na 'mikwara' ya Rais Magufuli

Hayo matatizo yote unafikiri muarobaini wa kuyaondoa ni Rais Magufuli tu???

Ni kwa misingi hiyo ya kumuamini fulani, kero za watu wengi wanazielekeza kwake kama vile hakuna viongozi wengine na hii si afya ktk utalawa sababu tutatengeneza 'one man show system' hatufanyi kazi kimfumo bali tunafanya kazi kimaagizo toka juu.

Yoyote utakaye teuliwa hatoonekana anafaaa km vile Rais, watu wanataka kusikia kauli ya Rais tu sio ya waziri ama mtu mwingine ambaye hata Rais amempa dhamana, maana kutokana na uteuzi na utenguzi usio na kikomo yawezekana imejengeka dhana miongoni mwa wananchi kwamba wateuliwa wanamuangusha Rais, sasa wananchi wanaona twende kwa Rais tu.

Anayeteua anaonekana siku zote yupo sahihi na wanaotenguliwa ambao kimsingi wamepewa brand name 'majipu' ndo tatizo, kwa akili ya kawaida ukisikia daktari anatumbua jipu ni lazma uone anafanya la maana sana hata kama wakati mwingine hatuelezwi sababu ya uteuzi na utenguzi ama huu utumbuaji kama unavyoitwa ila tunashangilia tu.

Tusitarajie ubunifu sababu kila anayeteuliwa anataka 'ku maintain status quo'.

Rais akifanya ziara ya kushtukiza utasikia na viongozi wa mikoa nao wanafanya ziara hizo.

Rais akitumbua na viongozi wa mikoa huku wanatambua.

Rais akikaa na makundi ya watu kama wafanyabiashara, viongizi wa dini nk utasikia mkuu was mkoa amewaita wasanii wote kwenye mkoa.

Kuna mtu aliwahi sema tuna viongozi wengi mabeki kuliko washambuliaji, akimaanisha wengi wanaowaza kulinda nafasi zao kuliko kuleta tija ya mafanikio.

Lengo la haya yote ni kuendena na kasi, kipimo cha utendaji mzuri wa kiongozi ni kuendana na kasi ya Rais na kufanya anayofanya, ubunifu ni ndoto ktk style hii.

Yote haya yanatokea ktk serikali inayohubiri uzalendo lakini utasikia sana ktk muktadha ama hadhara ya uma usio wa kiitikadi, vingozi wakisema, "serikali ya Magufuli", "serikali ya chama cha Mapinduzi" badala ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Sasa kama baadhi ya mifumo ime paralyze unataka rais akae kimya?.
Mara ngapi umemsikia rais akilalamika kuhusu viongozi anaowateua kutokuchukua actions kwa issues ndogo ndogo tu. Kwa kifupi serikalini kuna uzembe mkubwa sana wa utendaji kazi kuanzia ngazi za juu hadi chini. Nazungumza from the experience kwani nimefanya kazi private sector na Government pia. Serikalini hamna kuwajibishana mtu aki underperform. Tofauti na private ambapo uki underperfom unawekwa pembeni.
 
Kila kiumbe hujitofautisha kwa sifa zake. Vipo vunavyofahamika na kujitanabaisha kwa kutaga mayai, kuzaa, kuruka, kutambaa, kutembea na kadhalika. Sifa hutofautisha.

Alipoingia madarakani Rais Magufuli, wananchi na wasaidizi/wateule wake walikuwa wakisubiri Rais ajitanabaishe. Sasa wameshamjua. Wanafuata kadiri atakavyo.

Wanamjua kuwa anapenda YEYE NA NI YEYE TU ABUNI JAMBO. Wao wanasubiri ubunifu wake. Wanamjua kuwa HACHELEWI KUKUGEUKA UKITHUBUTU KUBUNI AU KUAMUA. wasaidizi wanamngoja aseme wafanye nini.

Wasaidizi HAWAJUI KINACHOMFURAHISHA WALA KINACHOMKWAZA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO. Wanamsubiri atoe maelekezo. Wanamsubiri kila wakati aseme. Ndiyo maana makongamano hayaishi.

Wasaidizi wanamjua KUWA HASHINDWI GHAFLA NA TENA HADHARANI KUKUPANDISHA CHEO, KUKUTUMBUA/KUKUTEUA,KUKUSHUSHA AU HATA KUSEMA KWANINI AMEFANYA HIVYO. Daima wanasubiri muongozo.

Kutokana na hayo, wakubadilisha Ni YEYE. Aruhusu wasaidizi wake wabuni, waamue, waseme na watende bila kusubiri maelekezo. Wasaidizi wataenendelea kumsikiliza, kuandika maagizo na kuendelea na 'kawaida' iliyopo.

Dawa Ni kutoka kwa muundaji mwenyewe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Kilosa, Morogoro)

Mi nimechoka kabisaaaaaa, hili linchi nimelichoka kabisaaa,
Mtu huachi watu wafanye kazi.Sasa hao anawateua na baada ya miezi mitatu anatumbua atakuwa amerekebisha kweli??? Ni akili ipi mtu anatumia kufikiri?unadhani wewe ni mungu na unajua kila kitu?Nanyi wateule kataeni kuteuliwa maana mnadhalilika na kudhalilishwa na mtukufu mtume wenu.Ukikataa kuteuliwa heshima kwa mke na watoto wako itabaki wewe ni baba bali ukiteuliwa na kutumbuliwa hata ukifanya jambo dogo tu tofauti na matarajio basi mama na watoto watakunyoshea kidole kwa kuwa walishajua wewe huwezi ndo maana hata mteule mtume mtukufu alikutengua.
 
Sasa kama baadhi ya mifumo ime paralyze unataka rais akae kimya?.
Mara ngapi umemsikia rais akilalamika kuhusu viongozi anaowateua kutokuchukua actions kwa issues ndogo ndogo tu. Kwa kifupi serikalini kuna uzembe mkubwa sana wa utendaji kazi kuanzia ngazi za juu hadi chini. Nazungumza from the experience kwani nimefanya kazi private sector na Government pia. Serikalini hamna kuwajibishana mtu aki underperform. Tofauti na private ambapo uki underperfom unawekwa pembeni.
Ndo tunajiuliza kutumbua tumbua ndo solution??? kama ni hivyo mbona bado hali ni ile ile...

Yeye ndo anawaweka, yeye huyo huyo anawatumbua, je sio kwamba yawezekana Rais hachagui watu sahihi na baadae analazimika kutumbua tumbua???

Tupe uzoefu wako.
 
Hadi leo hawajamuelewa ama ni wapigaji? Wizi na uvivu ndo kinachowasumbua watz na si rais wetu
 
Sasa kama baadhi ya mifumo ime paralyze unataka rais akae kimya?.
Mara ngapi umemsikia rais akilalamika kuhusu viongozi anaowateua kutokuchukua actions kwa issues ndogo ndogo tu. Kwa kifupi serikalini kuna uzembe mkubwa sana wa utendaji kazi kuanzia ngazi za juu hadi chini. Nazungumza from the experience kwani nimefanya kazi private sector na Government pia. Serikalini hamna kuwajibishana mtu aki underperform. Tofauti na private ambapo uki underperfom unawekwa pembeni.
Unajipa promo za kipumbavu kabisa! Kama ulifanya kazi serikalini basi ulikuwa muhudumu wa chai!
 
Wewe ndiyo umetaja muarobaini wa matatizo mengi yanaikabili nchi yetu katika awamu hii. Rasimu ya Jaji Warioba irejelewe tu!
Akitaka afanikiwe akubali tu kujenga mfumo imara kupitia katiba mpya ya Jaji Warioba. Na kama kweli ana nia njema na nchi hii, basi hana budi kutanguliza maslahi ya nchi kwanza badala ya chama chake cha mapinduzi.
 
Uongozi unahitaji akili ,busara na hekima kitu ambacho jiwe hana ,sasa mabadiliko yatatoka wapi ?
 
Mzee wetu alipotea sana. Tulimmiss sawa BA Nyani Ngabu, sijui ukimya wake una nini. Rejea Taf tunamiss comment zako na kiingereza chako cha ukweli sana
ahaa mkuu 😂 Bombabomba!! MWINGINE naye kapotea UNAMKUMBUKA???

anaitwa HUTAKI UNAACHA alikuwa akipost ! jamii forum inanyamaza kwa muda ! HUTAKI UNAACHA YUKO WAPI??
 
Naweza kusema kuwa bado tu hawajamjua anataka nini, Rais anataka kiongozi mzarendo na aliyejikana kwa masrahi mapana ya taifa na si mtu anayewaza masrahi yake huku akijua yeye ni kiongozi wa umma

Kuwa kiongozi wa umma ni kujitoa kwa ajili ya wananchi na si kuwaza utakuwa umemiliki nini baada ya kustaafu au kumaliza muda wako wa uongozi.

Kuwa kiongozi si kupata fursa ya kukufanya uwe tajili baali uwe daraja la kuwavusha wananchi na taifa kwa ujumla kufikia malengo.
Wanaomshabikia ni hawa ambao unaweza kupima hata kwa kuangalia uwezo wao wa kuandika.

Mtu anashindwa kuandika hata aya angalao moja iliyonyooka kwa Kiswahili kizuri, halafu kweli ataweza kuelewa hata hoja inayojariliwa?
 
Jengo ni la umma na lipo kwa maslahi ya umma na taifa kwa ujumla.

Uwanja ni wa umma na upo kwa maslahi ya umma na taifa kwa ujumla

Kutua ndege za maana siyo hoja ya msingi, hata Musoma uwanja upo lakin hakuna ndege za maana zinazotua pale.

Vivyo hivyo taa si za mtu binafsi.
Unakielewa ulichoandika? Kwa maelezo haya unaweza Jenga jengo KUBWA LA aviation LIULI HUKO NYASA.... Maana hata likijengwa huko bado litakuwa la UMA ingawa huko ndege hamna
 
Kila kiumbe hujitofautisha kwa sifa zake. Vipo vunavyofahamika na kujitanabaisha kwa kutaga mayai, kuzaa, kuruka, kutambaa, kutembea na kadhalika. Sifa hutofautisha.

Alipoingia madarakani Rais Magufuli, wananchi na wasaidizi/wateule wake walikuwa wakisubiri Rais ajitanabaishe. Sasa wameshamjua. Wanafuata kadiri atakavyo.

Wanamjua kuwa anapenda YEYE NA NI YEYE TU ABUNI JAMBO. Wao wanasubiri ubunifu wake. Wanamjua kuwa HACHELEWI KUKUGEUKA UKITHUBUTU KUBUNI AU KUAMUA. wasaidizi wanamngoja aseme wafanye nini.

Wasaidizi HAWAJUI KINACHOMFURAHISHA WALA KINACHOMKWAZA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO. Wanamsubiri atoe maelekezo. Wanamsubiri kila wakati aseme. Ndiyo maana makongamano hayaishi.

Wasaidizi wanamjua KUWA HASHINDWI GHAFLA NA TENA HADHARANI KUKUPANDISHA CHEO, KUKUTUMBUA/KUKUTEUA,KUKUSHUSHA AU HATA KUSEMA KWANINI AMEFANYA HIVYO. Daima wanasubiri muongozo.

Kutokana na hayo, wakubadilisha Ni YEYE. Aruhusu wasaidizi wake wabuni, waamue, waseme na watende bila kusubiri maelekezo. Wasaidizi wataenendelea kumsikiliza, kuandika maagizo na kuendelea na 'kawaida' iliyopo.

Dawa Ni kutoka kwa muundaji mwenyewe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Kilosa, Morogoro)

Jukumu LA loudspeaker ni kunena atakayo MC.
 
Mzee Tupatupa ulipotea kidogo, tafadhali toa tamko kuhusu hali ya uchumi inchini

Vinginevyo wasalimie Kilosa, usisahau kutuletea samaki
 
Nape alijiongeza kikamkuta,Mwigulu alijiongeza kumtumbua msajili mambo ya ndani kwa kuwaandikia KKKT barua isiyo na baraka zake,naye kikamkuta kilichomkuta!!!
Yaani kukuru kakara!
Watendaji na viongozi mbalimbali serikalini na majeshini Waliotumbuliwa hadi sasa wamekua wengi ndani ya miaka minne hii duh hatari... Ngoma ikifika 2025 cjui itakuaje
 
Naweza kusema kuwa bado tu hawajamjua anataka nini, Rais anataka kiongozi mzarendo na aliyejikana kwa masrahi mapana ya taifa na si mtu anayewaza masrahi yake huku akijua yeye ni kiongozi wa umma

Kuwa kiongozi wa umma ni kujitoa kwa ajili ya wananchi na si kuwaza utakuwa umemiliki nini baada ya kustaafu au kumaliza muda wako wa uongozi.

Kuwa kiongozi si kupata fursa ya kukufanya uwe tajili baali uwe daraja la kuwavusha wananchi na taifa kwa ujumla kufikia malengo.
Hivi unawezaje kua na account jamii forums wakati hata matumizi ya "R" na "L" huyajui??? (Mzarendo, masrai, tajili)
 
Kila kiumbe hujitofautisha kwa sifa zake. Vipo vunavyofahamika na kujitanabaisha kwa kutaga mayai, kuzaa, kuruka, kutambaa, kutembea na kadhalika. Sifa hutofautisha.

Alipoingia madarakani Rais Magufuli, wananchi na wasaidizi/wateule wake walikuwa wakisubiri Rais ajitanabaishe. Sasa wameshamjua. Wanafuata kadiri atakavyo.

Wanamjua kuwa anapenda YEYE NA NI YEYE TU ABUNI JAMBO. Wao wanasubiri ubunifu wake. Wanamjua kuwa HACHELEWI KUKUGEUKA UKITHUBUTU KUBUNI AU KUAMUA. wasaidizi wanamngoja aseme wafanye nini.

Wasaidizi HAWAJUI KINACHOMFURAHISHA WALA KINACHOMKWAZA KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO. Wanamsubiri atoe maelekezo. Wanamsubiri kila wakati aseme. Ndiyo maana makongamano hayaishi.

Wasaidizi wanamjua KUWA HASHINDWI GHAFLA NA TENA HADHARANI KUKUPANDISHA CHEO, KUKUTUMBUA/KUKUTEUA,KUKUSHUSHA AU HATA KUSEMA KWANINI AMEFANYA HIVYO. Daima wanasubiri muongozo.

Kutokana na hayo, wakubadilisha Ni YEYE. Aruhusu wasaidizi wake wabuni, waamue, waseme na watende bila kusubiri maelekezo. Wasaidizi wataenendelea kumsikiliza, kuandika maagizo na kuendelea na 'kawaida' iliyopo.

Dawa Ni kutoka kwa muundaji mwenyewe!

Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwasasa Kilosa, Morogoro)
Mzee unazunguka wewe,kila siku location mpya.
 
Back
Top Bottom