Sababu ya mambo kubaki 'Kama kawaida' pamoja na teua/tengua, maelekezo, maelezo na 'mikwara' ya Rais Magufuli

..Raisi alisema kuna watu anataka waishi kama MASHETANI.

..Sasa kuna namna nzuri ya kufanya wafanyabiashara waishi kama mashetani zaidi ya kuwatoza kodi kubwa na kuwapiga faini kikatili?

..Kwa maoni yangu Tra walikuwa wanatekeleza kauli ya Raisi. Ni bahati mbaya kwamba amekuja kuwageuka lakini for the last three years alikuwa akiwasifia.
sikumbuki mara ya mwisho walitangaza lini makusanyo ya kujisifia
 
Mzee yuko hoi
tapatalk_1559999290797.jpeg
 
Mnamlaumu Magufuli bure tu. Tanzania hii hata atawale malaika bado watu watalalamika tu.
Sisi Watanzania/waafrika wengi wao ni wabinafsi na wazembe sana. Hatujali kazi, Hatufanyi kazi kwa weledi. Mtu akipata nafasi flani anaitumia kuiba ama kunyanyasa wengine. Tunapenda sana kulalamika sometimes with no reasons. Pia ni wanafiki sana. Mtu anaweza kufanya kosa ila akiazibiwa kelele zinapigwa kila kona. Tuna wivu Uliopitiliza. Viongozi wakipewa nafasi hawawi wabunifu katika kuboresha kazi zaidi ya kusubiri mshahara mwisho wa mwezi na Kuplani jinsi ya kupiga allowance.
Kwa kifupi hii nchi hata apewe Mbowe, Zito, Maalimu ama Lipumba bado watu watalalamika tu.
Japo Magu ana mapungufu kidogo ila kwa upande wangu namkubali sana. Maana nlishabahatika kuwa kiongozi kwenye taasisi ya Serikali so Watanzania nawajua. Magu anajitahidi kuwapatia. Maana nlishangaa hata PM alivyowaacha wale jamaa wa TRA waliozuia mzigo wa mfanyabiashara wa Kariakoo unreasonably.
“In Magufuli I Trust”.
“Magufuli again 2020”.

Suluhisho la watu kulalamika ni katiba mpya ya rasimu ya Warioba. Lakini inaonekana ww una mawazo ya katiba inayomfanya mtu kuwa Mungu mtu. Tukiwa na taasisi imara zitapunguza malalamiko kwani watu watakaa kwenye nafasi kwa uwezo na sio upendeleo. Cha ajabu rais mwenye nia njema hataki utawala wa taasisi zenye nguvu kwani atakosa kusifiwa yeye binafsi. Sasa kama rais anachagua viongozi karibu wote nchini, tena kwa utashi wake, hapo unategemea kupata viongozi bora au viongozi wanaomsujudu rais ili wapate mlo?
 
Rasimu ya Warioba ikitumiwa na watu wakawa seriously kuitekeleza nadhani robo tatu ya Watanzania wataishia jela.
WaTZ tuna udhaifu mkubwa wa kufuata taratibu na sheria.
Pia sijajua Rasimu ya warioba imeeleza nini kuhusu rushwa, ubinafsi na kutokuwajibika kwa waTZ.
 
Yale yalikuwa maoni halisi ya wananchi, kama wananchi waliweka sheria za kuishia jela, ikitokea hivyo hawana wa kumlaumu. Hiyo rasimu kuna uzi wake humu. Pitia ujionee mwenyewe.
 
Mnamlaumu Magufuli bure tu. Tanzania hii hata atawale malaika bado watu watalalamika tu.
Sisi Watanzania/waafrika wengi wao ni wabinafsi na wazembe sana. Hatujali kazi, Hatufanyi kazi kwa weledi. Mtu akipata nafasi flani anaitumia kuiba ama kunyanyasa wengine. Tunapenda sana kulalamika sometimes with no reasons. Pia ni wanafiki sana. Mtu anaweza kufanya kosa ila akiazibiwa kelele zinapigwa kila kona. Tuna wivu Uliopitiliza. Viongozi wakipewa nafasi hawawi wabunifu katika kuboresha kazi zaidi ya kusubiri mshahara mwisho wa mwezi na Kuplani jinsi ya kupiga allowance.
Kwa kifupi hii nchi hata apewe Mbowe, Zito, Maalimu ama Lipumba bado watu watalalamika tu.
Japo Magu ana mapungufu kidogo ila kwa upande wangu namkubali sana. Maana nlishabahatika kuwa kiongozi kwenye taasisi ya Serikali so Watanzania nawajua. Magu anajitahidi kuwapatia. Maana nlishangaa hata PM alivyowaacha wale jamaa wa TRA waliozuia mzigo wa mfanyabiashara wa Kariakoo unreasonably.
“In Magufuli I Trust”.
“Magufuli again 2020”.
Umeanza vizuri ila hapo chini umeharibu... unanikumbusha kwenye uandishi wa insha umaliziaji ulikuwa ni kitu cha msingi sana...
 
Okay Mkuu. Maadamu katiba ya zamani inaruhusu uhuru wa kutoa maoni basi siwezi bishana na wewe.
But kwangu mimi naona Magu ndio Raisi anayetufaa kwa wakati huu japo ana mapungufu machache ya kiubinadamu
 
Mkuu kumbuka katiba ya zamani inanirihusu kutoa maoni. Ushaanza kuninyima uhuru wa kutoa maoni Mkuu ilihali mnalilia katiba ya Warioba😀!!.
 
Okay Mkuu. Maadamu katiba ya zamani inaruhusu uhuru wa kutoa maoni basi siwezi bishana na wewe.
But kwangu mimi naona Magu ndio Raisi anayetufaa kwa wakati huu japo ana mapungufu machache ya kiubinadamu

Kwa taarifa yako mkuu, marais wote waliopita walikuwa na wafuasi wao waliokuwa wakitumia maneno haya haya yakwako kwamba rais wa wakati huo ndio aliyekuwa anafaa. So hujaongea neno au utetezi wowote mpya kulinganisha na nyakati za huko nyuma.
 
Juz badala Ampongeze Msaidiz wake kwa kufanikisha Marufuku ya mifuko ya plastiki kwa ustadi mkubwa.....
Akaanza kujisifia kua alitoa maelekezo tangu mwaka jana tena akalaumu na kukosoa kua wizara wamechelewa sana....!
Eeeh bhwana! hii nilikuwa sijaipata. Basi Mzee TUPA TUPA mada yake ni 100%.

Kilichonishangaza zaidi hadi sasa ni TRA. Baada ya kelele nyingi sana za wakati ule nikadhani walijirekebisha!

Tabia ya kutaka kufanya kila kitu wewe, matokeo yake ndio haya. Na bado kabisa! Atapata 'frustration' asipoangalia 'stress' itamwelemea. Matokeo yake huwa ni hatari!
 
Tatizo ni yeye kujigeuza kuwa ndiyo katiba nchi. Na laana ya kuvuruga katiba ni kuwa kila kitu huwa hakiendi badala yake anasingizia kukosa uzalendo na mabeberu wakati huo huo akijifanya mtakatifu kwa kudai kumtanguliza Mungu mbele wakati alishamdhihaki kwa kuvuruga katiba ambayo aliapa kuwa atailinda na kumaliza na kibwagizo cha MUNGU NISAIDIE.
 
Jengo ni la umma na lipo kwa maslahi ya umma na taifa kwa ujumla.

Uwanja ni wa umma na upo kwa maslahi ya umma na taifa kwa ujumla

Kutua ndege za maana siyo hoja ya msingi, hata Musoma uwanja upo lakin hakuna ndege za maana zinazotua pale.

Vivyo hivyo taa si za mtu binafsi.
Wakati mwingine muwe mnapata aibu ya kutetea yasiyostahili kutetewa.
 
..Raisi alisema kuna watu anataka waishi kama MASHETANI.

..Sasa kuna namna nzuri ya kufanya wafanyabiashara waishi kama mashetani zaidi ya kuwatoza kodi kubwa na kuwapiga faini kikatili?

..Kwa maoni yangu Tra walikuwa wanatekeleza kauli ya Raisi. Ni bahati mbaya kwamba amekuja kuwageuka lakini for the last three years alikuwa akiwasifia.
Hebu fikiria, siyo hawa TRA waliokuwa wanasifika kwa kuvuka malengo, kuweka rekodi ya ukusanyaji wa kodi?
Hizo kodi zingetoka wapi kama sio kunyang'anya wafanya biashara!
 
Ukiona bulb zaidi ya moja kila unapoiweka kwenye holder inaungua, basi tatizo sio bulb ila ni holder, holder ndio inatakiwa kutolewa.
 
Mnamlaumu Magufuli bure tu. Tanzania hii hata atawale malaika bado watu watalalamika tu.
Sisi Watanzania/waafrika wengi wao ni wabinafsi na wazembe sana. Hatujali kazi, Hatufanyi kazi kwa weledi. Mtu akipata nafasi flani anaitumia kuiba ama kunyanyasa wengine. Tunapenda sana kulalamika sometimes with no reasons. Pia ni wanafiki sana. Mtu anaweza kufanya kosa ila akiazibiwa kelele zinapigwa kila kona. Tuna wivu Uliopitiliza. Viongozi wakipewa nafasi hawawi wabunifu katika kuboresha kazi zaidi ya kusubiri mshahara mwisho wa mwezi na Kuplani jinsi ya kupiga allowance.
Kwa kifupi hii nchi hata apewe Mbowe, Zito, Maalimu ama Lipumba bado watu watalalamika tu.
Japo Magu ana mapungufu kidogo ila kwa upande wangu namkubali sana. Maana nlishabahatika kuwa kiongozi kwenye taasisi ya Serikali so Watanzania nawajua. Magu anajitahidi kuwapatia. Maana nlishangaa hata PM alivyowaacha wale jamaa wa TRA waliozuia mzigo wa mfanyabiashara wa Kariakoo unreasonably.
“In Magufuli I Trust”.
“Magufuli again 2020”.
Hayo matatizo yote unafikiri muarobaini wa kuyaondoa ni Rais Magufuli tu???

Ni kwa misingi hiyo ya kumuamini fulani, kero za watu wengi wanazielekeza kwake kama vile hakuna viongozi wengine na hii si afya ktk utalawa sababu tutatengeneza 'one man show system' hatufanyi kazi kimfumo bali tunafanya kazi kimaagizo toka juu.

Yoyote utakaye teuliwa hatoonekana anafaaa km vile Rais, watu wanataka kusikia kauli ya Rais tu sio ya waziri ama mtu mwingine ambaye hata Rais amempa dhamana, maana kutokana na uteuzi na utenguzi usio na kikomo yawezekana imejengeka dhana miongoni mwa wananchi kwamba wateuliwa wanamuangusha Rais, sasa wananchi wanaona twende kwa Rais tu.

Anayeteua anaonekana siku zote yupo sahihi na wanaotenguliwa ambao kimsingi wamepewa brand name 'majipu' ndo tatizo, kwa akili ya kawaida ukisikia daktari anatumbua jipu ni lazma uone anafanya la maana sana hata kama wakati mwingine hatuelezwi sababu ya uteuzi na utenguzi ama huu utumbuaji kama unavyoitwa ila tunashangilia tu.

Tusitarajie ubunifu sababu kila anayeteuliwa anataka 'ku maintain status quo'.

Rais akifanya ziara ya kushtukiza utasikia na viongozi wa mikoa nao wanafanya ziara hizo.

Rais akitumbua na viongozi wa mikoa huku wanatambua.

Rais akikaa na makundi ya watu kama wafanyabiashara, viongizi wa dini nk utasikia mkuu was mkoa amewaita wasanii wote kwenye mkoa.

Kuna mtu aliwahi sema tuna viongozi wengi mabeki kuliko washambuliaji, akimaanisha wengi wanaowaza kulinda nafasi zao kuliko kuleta tija ya mafanikio.

Lengo la haya yote ni kuendena na kasi, kipimo cha utendaji mzuri wa kiongozi ni kuendana na kasi ya Rais na kufanya anayofanya, ubunifu ni ndoto ktk style hii.

Yote haya yanatokea ktk serikali inayohubiri uzalendo lakini utasikia sana ktk muktadha ama hadhara ya uma usio wa kiitikadi, vingozi wakisema, "serikali ya Magufuli", "serikali ya chama cha Mapinduzi" badala ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom