Sababu ya Israel kutokushinda vita ni kujipiga yenyewe kwa asilimia 40 kutokana na woga

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,365
11,255
Huku vita kati ya Hamas na Israel vikikaribia kuvuka miezi 7 siri zaidi za udhaifu wa jeshi la Israel zinaendelea kufichuka.

Pamoja na kusifiwa kwa ubora wa vifaa na ukubwa wa jeshi la Israel imeelezwa kuwa jeshi hilo limekuwa likijitia hasara kubwa kwa kuua askari wake na kuangusha droni zake kwa asilimia 40.

Mara zote hizo jeshi hilo limekuwa likifanya hivyo bila kukusudia wakidhani ni droni za Hamas zikikaribia kuwafikia walipo.Jambo hilo limekuwa likiongeza hasara za kivita kwa kiwango kikubwa sana.

Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari vya Israel ulibaini makosa kama hayo yalifanyika siku ya mwanzo ya oktoba 7 pale Hamas walipofanya mashambulizi ya kushtukiza.

Baadhi ya matukio machache ya hasara kama hizo ambayo yaliwahi kufichuka ni pale jeshi la Israel lilipoua mateka 3 wa Israel waliokuwa wakijaribu kujiokoa huku jeshi hilo likiwahofia ni wapiganaji wa Hamas.

Ukweli wa Israel kujipiga yenyewe na kudondosha asilimia 40 ya droni zake umeelezwa na afisa mmoja wa jeshi la Marekani akitaja kuwa na takwimu za kutoka jeshi la Israel lenyewe.

US Marine officer claims 40% of drones the IDF has shot down were their own, report says

Friendly fire 🔥 is a normal occurrence in any combat engagement so such cases in the Israel/Hamas war are inevitable and the same doesn't exclude the Israeli rivals in the conflict.
 
Hata madonga atasema sababu kuu yake kushindwa hutokana na kujipiga mwenyewe masumbwi.
 
Friendly fire 🔥 is a normal occurrence in any combat engagement so such cases in the Israel/Hamas war are inevitable and the same doesn't exclude the Israeli rivals in the conflict.
40% sio friendly fire basi.Kuna kitu kinatokea ndani kwa ndani.
Hamas wakaze kamba tu.
 
Wamewaua wenzao juzi na kifaru
Vijana wadogo 5
Eti waliona mtutu wa bunduki ukichomoza kutoka kwenye jengo.Wakavurumisha mzinga wakawaua.
Huo ni woga na kuchanganyikiwa kwa jeshi la Israel.
Pia inaondosha dhana kuwa Israel wana teknolojia za ajabu ajabu kwenye vita.Kumbe hata wenyewe kwa wenyewe hawajuwani walipo.
Wacha waziri wa ulinzi wa Israel ampashe Netanyahu.
 
Huku vita kati ya Hamas na Israel vikikaribia kuvuka miezi 7 siri zaidi za udhaifu wa jeshi la Israel zinaendelea kufichuka.

Pamoja na kusifiwa kwa ubora wa vifaa na ukubwa wa jeshi la Israel imeelezwa kuwa jeshi hilo limekuwa likijitia hasara kubwa kwa kuua askari wake na kuangusha droni zake kwa asilimia 40.

Mara zote hizo jeshi hilo limekuwa likifanya hivyo bila kukusudia wakidhani ni droni za Hamas zikikaribia kuwafikia walipo.Jambo hilo limekuwa likiongeza hasara za kivita kwa kiwango kikubwa sana.

Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari vya Israel ulibaini makosa kama hayo yalifanyika siku ya mwanzo ya oktoba 7 pale Hamas walipofanya mashambulizi ya kushtukiza.

Baadhi ya matukio machache ya hasara kama hizo ambayo yaliwahi kufichuka ni pale jeshi la Israel lilipoua mateka 3 wa Israel waliokuwa wakijaribu kujiokoa huku jeshi hilo likiwahofia ni wapiganaji wa Hamas.

Ukweli wa Israel kujipiga yenyewe na kudondosha asilimia 40 ya droni zake umeelezwa na afisa mmoja wa jeshi la Marekanie akitaja kuwa na takwimu za kutoka jeshi la Israel lenyewe.

US Marine officer claims 40% of drones the IDF has shot down were their own, report says

mwisho wa hii vita kichwa cha habari kitakuwa Hamas waipiga Israel,USA,UK na German....ushindi mkubwa na wa maana sana huu kwa kikukndi cha mgambo kupiga mataifa hayo makubwa kwenye vita
 
Amin na kweli inawezekana.
Kwa sababu kila kitu Mungu anakiona na yeye ndiye mwenye nguvu kuliko wababe wote wa dunia.
Angalia viongozi wa juu wa Hamas inasadikiwa wapo Gaza na bado Israel kashindwa kuwakamata,Unadhani ni ujanja wa Hamas peke yao.
 
Back
Top Bottom