Sababu ya furaha iko ndani yako.

Sababu ya furaha iko ndani yako.

badshah

Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
51
Reaction score
33
[h=1]Sababu ya furaha iko ndani yako.[/h] Sote tuna roho na miili. Sehemu ya roho siku zote huwa na furaha. Ni sababu ya furaha. Akili na fikra zako ndizo zinazuia virutubisho hivi vya furaha. Kama vile mawingu yanapoficha mwanga wa jua. Lakini jua siku zote huwaka na halijawahi kuzimika. Tunatafuta furaha nje, kwasababu tunaamini kuwa furaha ipo huko nje, lakini kwa uhakika furaha imo ndani yetu wenyewe. Huanzia ndani, lakini tunaidhihirisha furaha hii kwa matendo na matukio ya nje, kwa tunavyovimiliki na kwa watu.


Haijalishi ni shughuli gani hutafutwa, katika muda ambao furaha hutarajiwa jambo fulani hutokea. Iwe ni uoga wa kufika katika kilele cha mlima mrefu, kula keki tamu au kushinda bahati nasibu.


Katika kilele cha furaha, mchakato wa fikra husimama. Kunakuwa na ukimya wa ndani kwa ndani, na hofu zinaanguka. Kunakuwa na amani. Mashindano na hatari vyote huondoka. Hii huweza kudumu kwa muda mfupi hivi au hata mrefu kidogo. Katika amani hii kubwa tunajisikia furaha. Sio kwamba kuna kitu tumepata au kuna mafanikio fulani katika jambo ndiyo limeleta furaha hii, Hapana! Ni kitu fulani cha ndani kwa ndani na hakihusiani kabisa na jambo lolote la nje.

Staryte - Education, Entertainment & Development - Elimu, Burudani na Maendeleo
 
Kweli kabisa. To be happy is a choice. Na ukiwaachia wengine kazi ya kukufurahisha utaumia sana.
 
Na sababu za stress zipo ndani pia.
 
Waambiwa raha jipe mwenyewe. ..ukingoja kupewa. ..utasubiri sana
 
Yegoooo!!! hahahahah lol! Najua hiki kitu kinakuzingua sana. Sasa kwa kuwa umeshakisikiliza kwa leo unaweza kupanda kitandani lol! Ahsante sana Mkuu Yegomasika.
 
Last edited by a moderator:
Yegoooo!!! hahahahah lol! Najua hiki kitu kinakuzingua sana. Sasa kwa kuwa umeshakisikiliza kwa leo unaweza kupanda kitandani lol! Ahsante sana Mkuu Yegomasika.
Hii nyimbo kila nikiisikiliza asubuhi, basi siku hiyo huwa napiga/nabeba box kama sina akili nzuri vile!.
 
raha jipe mwenyewe kucheka kunaongeza afya na siku za kuishi.....make your self hapy do not expect to get it from others
 
Sawa Mkuu ukitaka kubeba box nyingi basi unajua ni wapi pa kutafutia motivation.

Usiku mwema

Hii nyimbo kila nikiisikiliza asubuhi, basi siku hiyo huwa napiga/nabeba box kama sina akili nzuri vile!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom