Sababu mbili kubwa za Mkutano mkuu kuwarejesha Mbowe na Dr Slaa uchaguzi wa ndani 2014

Wewe utakuwa mwanaCHADEMA lakini huifahamu CHADEMA katika mazingira ya jana na leo!.

Hao unaodai warudishwe lazima ufahamu kuwa hawahitaji kurudishwa kwa sasa kama fikra zako zinavyodhani kwa sababu wameishajirudisha wenyewe.

Mh. Mbowe na Dkt. Slaa kwa sasa wameishajenga mazingira ambayo hayahitaji hata kupigiwa kura ili kurudi katika nafasi zao za uongozi.

Mh. Mbowe na Dkt. Slaa wameishawafukuza na wanaendelea kuwafukuza wanachama wale ambao andiko lako ndiyo lilitakiwa liwaombe wawarudishe kina Mbowe na Dkt. Slaa katika nafasi zao.

Kwani hufahamu sababu iliyopelekea uchaguzi wa ndani wa CHADEMA Taifa kupigwa tarehe mara tatu ili waendelee kujenga mazingira ya kujirudisha wenyewe katika uongozi.

Kama unafahamu sababu zake, basi wewe utakuwa umetumwa pia kujenga mazingira ili ionekane kama kuna uwanja ulio sawa katika chaguzi za nafasi ya kitaifa ndani ya CHADEMA.

Kila siku ninasema, CHADEMA kimejengwa katika misingi ya kilaghai.
MwanaDiwani naona tumekutana hapa tena!!!
Vyama vya upinzani ni tofauti na chama kilichopo madarakani.
Gharama za kubadili viongozi kila baada ya miaka kumi zina faida na hasara yake na kuna wakati hasara inazidi faida.
Wakati wa Mtei,Bob Makani ungeweza kubadili uongozi bila athari kubwa kwa chama.Labda nikueleweshe kwa njia nyingine nayo ni kuwa mashambulizi yaliyokuwa yanavurumishiwa CDM wakati wa Mtei na Bob Makani ndiyo kama ya leo ya kufikia kuweka vinasa sauti chini ya kitanda?
Kwa nini CCM wanapenda uongozi wa CDM ubadilike,what is so special?
 
Hao waislamu wa kuwafukuza chadema watatoka wapi? ni sawa na CUF waseme kuwa chama chao si cha udini kwa vile waliowafukuza 100% ni waislamu hivi kweli CUF hao wakristo wanawatoa wapi?
Madiwani wa ARUSHA au MOSHI ulitarajia wawe wazaramo? Kile ni kifo cha wengi angalia wale mmoja mmoja walivyoshughulikiwa. je na hii hapa chini nayo ni vipi?
Mabadiliko ya katiba ya Chadema kuendana na uchagga

- Mtei M/kiti (mchagga)- hakuna ukomo wa muda
- Makani M/kiti (msukuma) muda ni vipindi viwili
- Mbowe M/kiti (mchagga) hakuna ukomo

Mkuu,
Kubali kushindwa naona umekwama hoja.
Kama hakuna waislamu wa kufukuzwa sasa kwa nini ulileta hoja hiyo?
Na kama hakuna makabila mengine nje ya wachaga wa kufukuzwa kwanini ulileta hoja hiyo? Unajua tatizo la propganda ukibanwa kwenye kona inakuwa ngumu kuchomoka.
Hivi wewe unataka kusema chadema haina wasilamu. Mkoa yote yenye wailamu wengi + Zbar mbona wana viongoziwa chadema na hawafukuzw? Au kuna waislamu wa wanapendwa na wanaofukuzwa? Je, Akina prof S. Abdallah na Hamad Yusuf, Mohamed Mzee nk ambao ni wajumbe wa kamati kuu ilikuwaje wakawafukuza wenzao kwa uonevu kama unachosema ni kweli? Je, unajua kuwa karibu nusu ya wajumbe 32 wa kamati kuu ni waislamu na ndo waliofanya uamuzi wa kuwafukuza hao waliotimuliwa? Je, unajua aliyesimamia kutimuliwa kwa zitto ndani ya kamati kuu? kwa taarifa yako siyo Mbowe wala Slaa. Mbowe aliongoza kikao na Slaa alikuwa anaandika minutes ya kikao. Fanya home yako.

Nije kwenye hoja yako mpya.
Katiba ya kwanza ya chadema ilikuwa na ukomo na ukomo huo ndo uliohitimisha uongozi wa Mzee Mtei muda wake ulipofika.
Bob Makani aliongoza kwa katiba hiyo hiyo,alikaa miaka 10 na baada ya muda wake kuisha aliondoka. Hakuondoka kwa kuwa ni msukuma au mwislamu.
Tatu, mwaka 2006 tuliandika katiba mpya na ndo katiba iliyoondoa ukomo wa uongozi kama ilivyo katiba ya vyama vingine kama CUF nk. kwa hiyo, sijajua hoja yako ni ipi?
 
Mkuu,
Kubali kushindwa naona umekwama hoja.
Kama hakuna waislamu wa kufukuzwa sasa kwa nini ulileta hoja hiyo?
Na kama hakuna makabila mengine nje ya wachaga wa kufukuzwa kwanini ulileta hoja hiyo? Unajua tatizo la propganda ukibanwa kwenye kona inakuwa ngumu kuchomoka.
Hivi wewe unataka kusema chadema haina wasilamu. Mkoa yote yenye wailamu wengi + Zbar mbona wana viongoziwa chadema na hawafukuzw? Au kuna waislamu wa wanapendwa na wanaofukuzwa? Je, Akina prof S. Abdallah na Hamad Yusuf, Mohamed Mzee nk ambao ni wajumbe wa kamati kuu ilikuwaje wakawafukuza wenzao kwa uonevu kama unachosema ni kweli? Je, unajua kuwa karibu nusu ya wajumbe 32 wa kamati kuu ni waislamu na ndo waliofanya uamuzi wa kuwafukuza hao waliotimuliwa? Je, unajua aliyesimamia kutimuliwa kwa zitto ndani ya kamati kuu? kwa taarifa yako siyo Mbowe wala Slaa. Mbowe aliongoza kikao na Slaa alikuwa anaandika minutes ya kikao. Fanya home yako.

Nije kwenye hoja yako mpya.
Katiba ya kwanza ya chadema ilikuwa na ukomo na ukomo huo ndo uliohitimisha uongozi wa Mzee Mtei muda wake ulipofika.
Bob Makani aliongoza kwa katibu hiyo hiyo,alikaa miaka 10 na baada ya muda wake kuisha aliondoka. Hakuondoka kwa kuwa ni msukuma au mwislamu.
Tatu, mwaka 2006 tuliandika katiba mpya na ndo katiba iliyoondoa ukomo wa uongozi kama ilivyo katiba ya vyama vingine kama CUF nk. kwa hiyo, sijajua hoja yako ni ipi?

Udini katika chadema haina maana kufukuzwa tu ila kutopewa nafasi na kubaguliwa waislamu lakini pia,
-Mzee Mtei hakuacha shauri ya ukomo ila alimuachia shemeji yake Bob Makani
-Bob Makani aliacha shauri ya ukomo kwa kuwa si mchagga
-Mbowe alipewa Uenyekiti shauri ni mkwe wa Mzee Mtei
 
Mikael P Aweda umeligoroga njoo ulinywe usiingie mitini:
-Mwenyekiti wa kwanza Mtei
-Mwenyekiti wa pili Bob Mkani shemeji wa Mtei
-Mwenyekiti wa tatu Mbowe mkwe wa Mtei
Je hii coincidence? hiki ni chama cha aina gani kama si cha ukoo?
 
Kaka kumrudisha Mbowe na Slaa madarakani kuingoza CDM kwenye dakika hizi za lalasalama ni PIGO kubwa sana kwa CCM. Ni kweli Mh. Mbowe amekuwa mbunifu mno kiasi inawachukua CCM miaka kuelewa mantinki nzima, hata mavazi tu ya CDM, Mh. Mbowe ameyabuni kuwa ya mfano wa Kombati, sasa juzi juzi CCM nao wamedesa kama ilivyo kawaida yao.

CCM kwa sasa wanahaha kuhakikisha hii combination hairudi tena kuiongoza CDM, kitu ambacho ni kichekesho kwani uamuzi wa kurudi ama kutorudi kwa makamanda hawa kuingoza CDM yapo mikononi kwa wajumbe wa mkutano mkuu pekee yake na si kiumbe mwingine yoyote.

Mbowe na Slaa ni viongozi ambao CDM bado inawahitaji mno kwa sasa ili kuimalizia kazi ndogo iyobaki ya kuunda Serikali 2015..

very true indeed....
 
Dr.Slaa na Mbowe wanaweza kuivusha Chedema salama 2015 kuliko waingie Viongozi wapya mwaka huu ambao watababaika mwakani kuelekea uchaguzi mkuu.Naunga mkono Mbowe na Dr. Washikilie usukani kipindi hiki kukabiliana na hujuma nyingi zilizoandaliwa na wapinzani wao kisiasa,pamoja na wasaliti.Wakiingia Viongozi wapya watayumbishwa kirahisi na ni mtaji kwa wanao watakia balaa

Hayo nayo ni mawazo mgado maana uchaguzi wa CDM Huwa unafanyika mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu ukiogopa viongongozi wapya kisa 2015 itafika tena 2019 useme tena wabakie walewale kwa sababu 2020 kuna uchaguzi mkuu
 
Wewe utakuwa mwanaCHADEMA lakini huifahamu CHADEMA katika mazingira ya jana na leo!.

Hao unaodai warudishwe lazima ufahamu kuwa hawahitaji kurudishwa kwa sasa kama fikra zako zinavyodhani kwa sababu wameishajirudisha wenyewe.

Mh. Mbowe na Dkt. Slaa kwa sasa wameishajenga mazingira ambayo hayahitaji hata kupigiwa kura ili kurudi katika nafasi zao za uongozi.

Mh. Mbowe na Dkt. Slaa wameishawafukuza na wanaendelea kuwafukuza wanachama wale ambao andiko lako ndiyo lilitakiwa liwaombe wawarudishe kina Mbowe na Dkt. Slaa katika nafasi zao.

Kwani hufahamu sababu iliyopelekea uchaguzi wa ndani wa CHADEMA Taifa kupigwa tarehe mara tatu ili waendelee kujenga mazingira ya kujirudisha wenyewe katika uongozi.

Kama unafahamu sababu zake, basi wewe utakuwa umetumwa pia kujenga mazingira ili ionekane kama kuna uwanja ulio sawa katika chaguzi za nafasi ya kitaifa ndani ya CHADEMA.

Kila siku ninasema, CHADEMA kimejengwa katika misingi ya kilaghai.

We kibaraka wa wasira unalo.
 
Udini katika chadema haina maana kufukuzwa tu ila kutopewa nafasi na kubaguliwa waislamu lakini pia,
-Mzee Mtei hakuacha shauri ya ukomo ila alimuachia shemeji yake Bob Makani
-Bob Makani aliacha shauri ya ukomo kwa kuwa si mchagga
-Mbowe alipewa Uenyekiti shauri ni mkwe wa Mzee Mtei
DINI uko wapi CDM?
Kwa nini mnapenda kujenga hoja dhaifu zisizo na ushahidi wa kutosha?
Hakuna sehemu ambayo Michael amegusia UDINI lakini kwa kuwa myopic mshakimbilia huko.
CCM isiyokuwa na UDNI mbona zaidi ya miaka kumi inahangaika na hoja ndogo ya KADHI?
Kikwete kila siku yuko America,ni kwa WAISLAMU huko?
Mimi ni MUISLAMU lakini nachukia mno mkigeuza UISLAMU kama mtoto yatima wa kuonewa huruma kila wakati.
Stop this please!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Udini katika chadema haina maana kufukuzwa tu ila kutopewa nafasi na kubaguliwa waislamu lakini pia,
-Mzee Mtei hakuacha shauri ya ukomo ila alimuachia shemeji yake Bob Makani
-Bob Makani aliacha shauri ya ukomo kwa kuwa si mchagga
-Mbowe alipewa Uenyekiti shauri ni mkwe wa Mzee Mtei

Kwa kweli mimi mtu anayejaribu kutetea hoja yake kwa kutumia hoja za udini huwa simwelewi hata chembe. Na kwa kweli nimekufuatilia hata sikuelewi unataka watu wenye akili timamu wakuelewe vipi, nimeshindwa,nimeshindwa kabisaaaa kukupata zaidi ya kukuona kuwa wewe labda na huko utokapo ndiyo wadini!!

Hebu jaribu kuangalia mambo kwa angle zote, acha tabia ya kuyatazama mapungufu ya mtu/watu kwa mtizamo wa kidini kwa sababu ni hatari sana. Acha kutumia silaha ya udini kama silaha ya kuwaangamiza adui zako wa kisiasa na hasa hasa pale unapokuwa huna uthibitisho wa ki-hoja, otherwise, we are detroying this beutiful nation unknowingly thinking that we are destroying our political opponents!!.

Baba wa Taifa hili Mwl J.K. Nyerere aliwahi kuonya juu athari za kupandikiza mbegu na ukabila na udini katika jamii huru kama hii ya kwetu, hebu tuendeleeni kuenzi haya na hakika tutaishi miaka mingi kwa amani.
 
Back
Top Bottom