mcshonde
Member
- Jul 15, 2022
- 66
- 152
Septemba 2022 shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines Group) lilisaini mkataba wa kumiliki 49% ya shirika la ndege la Nigeria.
Hatua hiyo ikalifanya Shirika hili linalomilikiwa na serikali ya Ethiopia kwa 100% kuendelea kutawala anga la Afrika, kwani linamiliki mashirika mengine kama:-
24% ya hisa African Airline (ASKY) la Lomé Togo.
49% ya hisa katika Shirika la Ndege la Malawi.
45% ya shirika la ndege la Zambia
49% ya mashirika ya ndege ya Tchadia kutoka Chad.
99% ya umiliki wa hisa Ethiopian-Mozambique Airlines LTD
51% ya Umiliki wa Hisa wa DHL-ET Huduma za Usafirishaji mizigo.
Upo mpango wa kuingia mkataba na Air Djibouti pamoja na Guinea Ecuatorial Airlines.
Kwanini shirika hili lenye wafanyakazi 17000 linazidi kukua zaidi!?
Licha ya kumilikiwa na serikali kwa asilimia 100, Ethiopian Airlines yenye ndege 178 inazidi kukua kwa sababu:-
a) Serikali imeliruhusu kufanya biashara na kutoingilia utendaji wa bodi hasa inapomchagua mkurugenzi mtendaji/CEO (sio kawaida sana barani Afrika)
b) Ufanisi wa usimamizi wake (hakuna ujanja ujanja na upigaji, viongozi wake ni wataalamu wanaoijua biashara)
c) Nafasi yake ya kijiografia
d) Ukosefu wa washindani wanaofaa ndani ya Afrika
e) Kwa ujumla ni “mbinu kali” za kuwaweka washindani nje ya mstari.
Kipindi cha janga la Uviko-19 mashirika mengi yalitangaza kupata hasara mwisho wa mwaka 2020, lakini Ethiopian Airline lilikuwa kati ya mashirika machache duniani yaliyopata faida.