Sababu Kuu tatu zinazopelekea ndoa Kuvunjika!

Sababu Kuu tatu zinazopelekea ndoa Kuvunjika!

Wateule

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2010
Posts
390
Reaction score
368
Mtaalam wa masuala ya mapenzi na ndoa, Timothy Scheiman,anasema Talaka [divorce] huwa zinatokea na tofauti huwa ni nyingi zisizo namuafaka [irreconcilable differences], lakini talaka nyingi hutokea chini yasababu kuu tatu, ambazo zinatokana na; kujamiiana; fedha; ndugu, jamaa, namarafiki. Scheiman anaendelea kuzichambua sababu hizo kuu tatu kama ifuatavyo:
Kujaamiiana (Sex)
Mtaalam anasema, kujaamiiana kumekuwa ni chanzo kikuu chakwanza kwa ndoa nyingi kuvunjika. Iwe ukosefu wa kujamiiana, kujamiiana kidogo,ukosefu wa elimu kuhusu tendo zima la kujaamiiana, au kujaamiiana na mtu ambayehakukusudiwa (wrong person). Scheiman anaendelea kusema kwamba inamshangazasana kuona watu wanaingia kwenye ndoa wakati ufahamu wao wa tendo la ndoa ukochini sana. Pamoja na hilo, anaonya kwamba hii sio sababu ya watu kufanyamajaribio kwanza kabla ya kuoana (experiment before marriage), bali ni kwa wanandoa kusoma vitabu, kuulizana na kuzungumza kuhusu vile vinavyowapendeza na kuwavutiakatika tendo hilo muhimu, ili kuridhishana. Kwa maneno mengine, mke atafutekipi kinachomridhisha (please) mume, na alkadhalika mume atafute kipi kinachomridhishamke.
Zaidi anasema, hofu na kutokujua huweza kusababisha matatizomakubwa katika ndoa. Pia, kulazimisha mshirika mmoja (partner) kushiriki kwenyemitindo na matendo (positions and acts), ambayo haipendi au kukubaliana nayo,pia inasababisha matatizo makubwa. Anashauri wana ndoa wawe makini na wawazizaidi katika mawasiliano yao, ili kuepuka hii sintofahamu. Kwa msaada zaidi,anapendekeza wanandoa wasome kitabu kiitwacho "The Act of Marriage"kilichoandikwa na Tim Lahaye. Anasema kitabu hiki kina mandhali ya kikristo,lakini hakifichi kitu inapokuja suala la kujaamiiana. Ana amini kwamba kamawanandoa watajieleimisha, basi matatizo yatapungua katika nyanja hii.
Fedha (Finance)
Hapa mtaalam ana anza na ovyo kali kwamba moja kati ya vituambavyo vinaweza vikateketeza ndoa ni malumbano kuhusu fedha. Wakati wanandoawana madeni au wanalumbana fedha kiasi gani imetumika au kuhifadhiwa, kunawezakukatokea matatizo makubwa. Katika suala hili, mtaalam anashauri wanandoawafanye yafuatayo:
1. Wasijiingize kwenye madeni makubwa , na kama mpokwenye madeni sasahivi, basi huu ni wakati muafaka wa kujipanga na kujinasuakwenye madeni hayo.
2. Ana amini Bajeti mara nyingi hazitekelezekikwenye ndoa, lakini anashauri angalau kuwepo makubaliano baina ya wanandoakwamba matumizi yeyote yanayozidi $100 (ni kama 160,000 za Kitanzania) yapate barakaza wanandoa kabla ya kuhidhinishwa.
3. Kila mshirika katika ndoa awe na fedha " kichaa"kidogo (mad money) za kutumbua kutoka katika kila malipo ya wiki (kwa wale waBongo malipo ya kila mwezi) angalau hata shilling chache au tudola kadhaa.Lengo hapa ni kuwa na uhuru wa kuzitumia pesa hizo utakavyo, nje ya makubalianoyaliyotajwa hapo juu.
4. Mwisho, wanandoa lazima wahakikishe kwambawanahifadhi pesa zao (saving) hata kama kiasi kidogo kwa week, kwanikikidundulizwa kiasi hicho kinakuwa kikubwa mbele ya safari.

Ndugu, jamaa, na marafiki
Mtaalam anatahadharisha kwamba hao watu waliotajwa hapo juuwanaweza wakawa sumu katika ndoa kama mwanandoa hayupo makini. Watu waowaliotajwa wanahusisha pia mama, baba, madada, makaka, na kadhalika. Hawa siwashirika katika ndoa, ndoa ni ya watu wawili tu,yaani mke na mume. kwahiyo haowatu lazima wawe na mipaka katika ndoa yako. Kama utawaruhusu watu waowazungumze wanachotaka kuhusu mwenza wako au ndoa yako, basi ujue unaelekeakuizika ndoa yako, ana malizia kusema mtaalam.

Wewe una maoni gani kuhusu hizi sababu za uvunjifu wa ndoa?Je unafikiri hizi sababu zina mashiko yeyote katika jamii yetu ya Kitanzania?


Imeandaliwa na: www.thehabari.com


Chanzo: Yahoo Voices
 
Lakini wakati mwingine mtu unafikia mahala unamchoka/ unamkinai tu mwenza wako.

Kibinadamu ni vigumu sana kuwa na kitu kilekile miaka nenda rudi bila kutaka kingine.

Haiingii akilini kabisa eti kwa vitu vingine ni sawa kubadilisha ladha au mandhari lakini ikija kwenye mambo ya ndoa basi inakuwa si sawa kufanya hivyo.

Ni binadamu gani aliyehuru awezaye kula chakula hicho hicho kila siku kwa miaka mingi bila kutaka kubadili? Mambo ya uaminifu kwenye ndoa ni njozi tu.
 
Hizo ni baadhi ya sababu

lakini tukizama kwa undani haziwezi hesabika kama tutaamua kuziorodhesha, naweza sema kila binaadamu anakua na visingizio vyake pale atakapomchoka mwenza
 
Lakini wakati mwingine mtu unafikia mahala unamchoka/ unamkinai tu mwenza wako.

Kibinadamu ni vigumu sana kuwa na kitu kilekile miaka nenda rudi bila kutaka kingine.

Haiingii akilini kabisa eti kwa vitu vingine ni sawa kubadilisha ladha au mandhari lakini ikija kwenye mambo ya ndoa basi inakuwa si sawa kufanya hivyo.

Ni binadamu gani aliyehuru awezaye kula chakula hicho hicho kila siku kwa miaka mingi bila kutaka kubadili? Mambo ya uaminifu kwenye ndoa ni njozi tu.

Mbona hilo linawezekana tu tena sanaa! mbona kila mtu ana baba yake mzazi mmoja/ mama mbona hakuna aliyekinaiwa kuwa na baba/mama yuleyule....ni swala la mtazamo tu.
 
Mbona hilo linawezekana tu tena sanaa! mbona kila mtu ana baba yake mzazi mmoja/ mama mbona hakuna aliyekinaiwa kuwa na baba/mama yuleyule....ni swala la mtazamo tu.

Kama baba na mama wameishi pamoja kwa miaka mingi haina maana hakuna aliyechepuka. Wote mnaweza kuchepuka na bado mkaendelea na ndoa (ndoa jina tu, of course).
 
Kama mimi ndio ningekua Timony Scheiman hiyo namba tatu ndio ingekua ya kwanza, na nyengine ingekua ni KUCHAGUA MTU ASIYE SAHIHI KWAKO, hapo utakuta imejumuisha mambo mengi sana ambayo hiyo ya kwanza na yapili utaikuta hapo
 
Ukiona uko kwenye ndoa then unamkinai mwenzako ujue huyo uliye nae sio sahihi kwako. umelazimsha ndoa ,Mliangalia utashi wenu binafsi. Me naamini ukimkabidhi Mungu atakupa mtu sahihi utaona kuchanua na kufanikiwa katika ndoa yenu . Hya mambo ya mtaalam me wala sion kama yanaapply Mana ni jambo gani gumu la Kumshind Bwana? Ushauri kwa vijana ambao hatujaoa kama mimi tukitaka kuoa tummulize Mungu ni yupi mke mwema ?co habari unaenda kumuomba Mungu nipe mke mwema halafu una picha ya msichana fulani ambye uko nae ktk mahusiono unasema nipe huyu . Unafikir Mungu Mungu atafanyje atakupa huyohuyo hata kama sio wako then tunaimba anameremeta anameremeta baada ya miaka mitatu tutaimba amechakaa amechakaa why? Haukuwa mpango wa Mungu kuoa au kuolewa na huyo Yeremia29:11-14 ni wazi kuwa mpango wa Mungu ni kutusaidia na kutusaidia hadi tunafikia mwisho mwema hapa duniani sio kutuangusha kufiki
 
Back
Top Bottom