Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Sababu CHADEMA kukosa wabunge zaidi ya nusu mwaka 2020 zaanikwa.
Ndugu zangu,
kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2020 kumezuka taharuki baada ya matukio kadhaa ya baadhi ya wanasiasa wakiwemo wabunge, madiwani na hata wagombea urais kuhama vyama vyao hususani CHADEMA na kuhamia vyama vingine.
Kwa mwaka huu ,2019, waliokuwa wagombea Urais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania Ndg.Edward Lowassa (CHADEMA) na Maalim Seif Hamad mgombea urais Zanzibar (CUF) hawa wote waliwakilisha muungano usiokuwa rasmi ukiitwa UKAWA wamechana na vyama vyao na kwenda katika vyama vingine.Huku Lowassa akirejea CCM, na Seif akitimkia ACT-Wazalendo.
lazima tuseme ukweli, Muungano wa UKAWA uliibeba Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2015 huku ukikandamiza vyama vingine. Kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020 iwe kuna makubaliano baina ya vyama au yasiwepo CHADEMA itakuwa muathirika mkuu, kutokana na sababu/hoja zifuatazo;
Kwanza, ulaghai uliotumika na Mbowe kusimamisha wagombea CHADEMA katika majimbo ya vyama vingine hautakubalika tena. Ikimbukwe, wagimbea wa CHADEMA walimgomea Duni Haji kuwaachia majimbo wagombea wa CUF hususani katika maeneo ya mikoa ya kusini na Segerea huku Mbowe akitumia kigezo cha ''mahakama ya wananchi''. Waswahili wanasema ''uking'atwa na nyoka hata jani.......''
Pili, Nguvu ya Ndg.Edward Lowassa iliwabeba katika maeneo mengi hususani mijini kwani baadhi ya wafuasi wa Lowassa walioasi CCM walisaliti mbinu na kuwasaidia wapinzani kushinda. Mfano, Iringa, Dar, Mbeya, Arusha, na Kilimanjaro. Hata baada ya Uchaguzi madiwani wateule katika mkoa wa Dar walikusanyika katika ofisi ya Lowassa Mikocheni kumpa shukrani za dhati kwa kuwasaidia kushinda. Msaada huu wa Lowassa hautakuwepo mwaka 2020.
Tatu, hakuna ubishi mpasuko ndani ya Chadema baina ya viongozi, wanachama na wabunge ulisababishwa na hali ya kutoaminiana ni udhaifu mkubwa kuelekea mwaka 2020. Kitendo cha baadhi ya wabunge Chadema kung'atuka au kuvuliwa ubunge ''kiutatanishi'' kama Nassari ni dhahiri hali ni tete kuelekea uchaguzi mkuu 2020.
Nne, Mbowe,Lissu na wenzano hawatataka Zitto Kabwe awe ''bosi'' hasa ukizingatia mizengwe, vitimbi na kejeli na kumfukuza Chadema huku wakiapa kwa ''miungu yao'' Zitto ni ''msaliti'' na hatafanikiwa na hata kukibatiza chama chake cha ACT (''Allience for Cowards and Traitors'') na yeye kumpa jina la ''Ayatollah''. Ndio maana hata Tundu Lissu kapigwa na kigugumizi na uoga mwingi.
Tano, lazima tukubali huku bara na haswa mikoa ya kusini ambapo Cuf ina nguvu ni kutokana na jitihada za Lipumba ambaye alitumia hoja ya ''gesi asilia'' kwa kutumia kauli maarufu ya ''gesi haitoki''..tusibeze, yenye nguvu kusini ni Cuf na sio mtu na hata mwaka 2020 wataendelea kupata wabunge huko kusini kwani hata hao waliopo ni vijana aliowapika yeye.
Sita, ni dhahiri ACT Wazalendo sasa atazoa viti vya ubunge na wawakilishi nusu kutoka Zanzibar na pia ndio itakuwa pumulio la wanasiasa na wabunge wenye ugomvi na viongozi wao CCM,CUF na CHADEMA hivyo lazima itapata viti Tanganyika kukifanya kuwa Chama chenye ushawishi kwani pia kitakuwa na ushawishi Zanzibar.
Hoja hizi nilizoanishwa zikitumiwa vema katika mtazamo chanya na CHADEMA zitwasaidia kupunguza athari za maangamizo lakini wakiendelea kukaza shingo kwa kutoa kejeli muda utasema.
Nawasilisha.