Dr. Zaganza
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 1,801
- 2,715
Watu wengi ni masikini kwa sababu kuu tatu
1. Ujinga
Kutokujua jinsi gani ulimwengu wa pesa unavyofanya kazi. Wengi tumekuzwa katika mfumo wa "shule"...soma nursery, mpaka A-level then omba mkopo go to UNIVERSITY ...ukimaliza tembeza bahasha kuomba ajira serikalini, ukishapata unaanza kulipa mkopo kwa miaka zaidi ya 15 huku ukiishi maisha ya mshahara mwezi mpaka mwezi. Ukija kustuka umri wa kustaafu ushafika huna cha maana ulichokifanya. Leo hii tajiri akipaki ndinga lake hutasikia masikini wakisema kuwa jamaa kasoma sana yule ndio maana kafika pale alipo,maneno utakayoyasikia ni jamaa ni drug dealer, fisadi,jambazi, amewatoa kafara wazee wake, freemasoj n.k
2. Uvivu
Hapa unatakiwa uelewe kuwa ili ufike kwenye utajiri basi jua kuwa unashindana na kundi kubwa la watu katika kuisaka pesa, matajiri huwa hawalali, muda wote wanaisaka pesa ilipo tofauti na wafanyakazi wa serikalini unaingia kazini saa 2 na nusu unatoka saa 9 ukitoka unakwenda kulala nyumbani, ukisubiri kesho ifike.Matajiri muda wote wapo macho tembea barabarani usiku uone malori yao yanavyoingiza pesa, miradi yao inaingiza pesa masaa 24 bila kupumzika ila masikini hufanya kazi kwa muda mchache tu .Na muda ulobaki ni kujali mpira au muziki na siasa.
3. Kiburi
Ujuaji unafanya watu wengi kubaki katika umasikini. Ili uwe dereva mzuri ni lazima ufundishwe na mkufunzi mzuri...mfano mtu utakwenda VETA au NIT ili uive katika fani ya udereva, vivyo hivyo huwezi kuwa tajiri kama upo mbali na matajiri, huwezi kuwa tajiri kama hujakaa chini na waliokutangulia katika utajiri ukapata misingi ya nini ufanye kuelekea katika njia ya utajiri. Masikini wengi ni wajuaji, wanaridhika kuwa wao wanajua nini wafanye matokeo yake wanaendelea kubaki katika umasikini. Kaa karibu na uwaridi ili upate kunukia au fuata nyuki upate asali. Tusiwe viburi kujifunza kwa matajiri.