Sababu 3 zilizonyuma ya vifo ktk mikutano ya Chadema,mtumishi wa Serikali anitonya

Wananchi wanauliwa ndugu zao kwa ukaidi wenu, watoto na wajane waliopoteza wapendwa wao.

Hapo kwenye blue, nimekusaidia ku-edit (reason for editing : typo) last edited by Mu-Israeli today at 13:45.

Wananchi wanauliwa ndugu zao kwa ukatili wenu ninyi polisi, watoto na wajane waliopoteza wapendwa wao
 
Yaani sababu zote zinaitoa CDM kwenye picha. Kwa nini unatumia nguvu kuisafisha kama tayari ni safi? Wananchi wana akili wanajua ukweli.
Wewe ni lazima polisi wa CC MABWEPANDE sura na tabia vinajionyesha!! uko kamati ya kuchunguzwa kupigwa kwa Ulimboka!!
 
Wewe ni lazima polisi wa CC MABWEPANDE sura na tabia vinajionyesha!! uko kamati ya kuchunguzwa kupigwa kwa Ulimboka!!

And that makes you what? Dr Slaa who persue poor youth to riot while he remained in his hotel room shaging waitres?
 
Naamini ya kuwa Chadema hawabebi silaha za moto au za jadi katika mikutano yao na hata maandamano yao,iweje mauaji yatokee kisha yahusishwe na CDM?jukumu la askari ni kulinda raia na mali zao,iweje washindwe kuwalinda wananchi wanaojitokeza katika mikutano na maandamano ya CDM?hawa ni wananchi wa tanzania na ulinzi ni haki yao,Jamani tunakoelekea siko,kuna siku wananchi watachoka kuuawa kama kuku na hapatatosha,kimsingi wananchi ni wengi kuliko polisi.
 
And that makes you what? Dr Slaa who persue poor youth to riot while he remained in his hotel room shaging waitres?
And you were under his bed!! So it is also you who installed the stupid recorders in DOM. Wewe ni gogo la msalani ndugu yangu!!
 
And you were under his bed!! So it is also you who installed the stupid recorders in DOM. Wewe ni gogo la msalani ndugu yangu!!

Kama nilivyowajibu TCU wenzako, kwenye uhai wa mtu sinaga masihara.
 
Naamini ya kuwa Chadema hawabebi silaha za moto au za jadi katika mikutano yao na hata maandamano yao,iweje mauaji yatokee kisha yahusishwe na CDM?jukumu la askari ni kulinda raia na mali zao,iweje washindwe kuwalinda wananchi wanaojitokeza katika mikutano na maandamano ya CDM?hawa ni wananchi wa tanzania na ulinzi ni haki yao,Jamani tunakoelekea siko,kuna siku wananchi watachoka kuuawa kama kuku na hapatatosha,kimsingi wananchi ni wengi kuliko polisi.
The same happened to King cobra (Rais wa Zambia) akigombea Urais. Walimzushia uwongo mwingi, uonevu mwingi sana, lakini mwisho wa siku waonaeaji wakawa wapinzani. No way out, bunduki haijawahi kusaidia kubakisha utawala dhalimu madarani. Historia inakataa.

 
Ulichosema ni sahihi, tunasubiri sasa tamko kali kutoka CDM, ikibidi watangazie umma kuwa kuanzia sasa hivi ni wajibu wa kila mwanchi kujilionda mwenyewe, wakienda kwenye mkutano kila mtu aanze kujihami

Ni kweli, hata hivyo tusiwaachie jukumu hili viongozi wa Chadema peke yao. Kila mmoja ana wajibika. Ukitoka kazini jioni pale jirani na home kila mtu aanzishe kijiwe Cha Chadema kiwe sauti ya dhidi ya ubadhirifu ktk serikali ya mtaani. Kwa pamoja tutuweza.
 
Wakuu,
Kuna sababu tatu za kutokea kwa vifo ktk mikutano ya Chadema . Sababu ya kubwa ya kwanza iliyonifanya hata leo nilete uzi huu hapa ni maelezo ya rafiki yangu anayefanya kazi ktk mmoja ya taasisi za serikal akinitonya kwamba, serikali inataka kutunga sheria ya kuzuia ama kuthibiti mikutano ya hadhara na maandamano kama ilivyokwisha dokezwa na mwanasheria mkuu wa serikali Bungeni. Tatizo kubwa ambalo linawakabili mpaka sasa serikalini, ni kukubalika kwa sheria hiyo mbele ya Umma. Hii inatokana na baadhi ya maofisa (yeye amewaita objective) wanadhani kwamba itapingwa sana na vyama vya siasa na hata wananchi hawataiunga mkono sheria husika. Mmoja ya mapendekezo ni kwamba ili kupunguza vurugu na usumbufu ktk mikutano na maandamano, viogozi wasiruhusiwe kwenda kwenye majimbo yasiyo yao kisheria (Hoja ya Anne Kilango Bungeni) bila kupata ruhusa na bila sababu inayoeleweka. Huyo bwana akasema, nina wasiwasi na vifo hivi na harakati zinaendelea huku serikalini za kuhalalisha sheria hiyo ambayo yeye pamoja na kufanya kazi kwa miaka mingi serikalini, ana ona kama ni mbovu kabla hata draft ya kwanza yenyewe haijaandaliwa.

Hoja ya pili kubwa sana ni hao Maofisa objective wanaopinga sheria hiyo, wanadhani kwamba sheria hiyo itagombanisha serikali na wafadhili kiasi cha kuzuia misaada na mikopo. Hoja hii ya pili ya wapinzani wa sheria hii ndio yenye nguvu kuliko kuliko ile ya kwanza. Sasa yeye ananiuliza, hebu fanyeni utafiti isijekuwa yanajengwa mazingira ya kuwalainisha wahisani na kuhalalisha sheria hiyo kabla sheria haijatungwa na hamjazuiwa kufanya shughuli zenu za kisiasa.
Kwa maoni yake japokuwa hana ushahidi, vifo hivi na utata unaozingira vifo vyenyewe kunaweza kuwa na uhusiano na taarifa zake. (Hayo ni ya rafiki yangu aliyoniambia)


Sababu ya 2 Vifo cha Singida na Morogoro kwa nini vinaweza kuwa na mkono wa mtu.
Kifo cha Singida kwa kiwango kikubwa inahalalisha (justify) maelezo ya huyo rafiki yangu. Hii ni kwa sabau, Katika mikutano iliyofanyika Singida viongozi wa Chadema walipata taarifa kuwa vurugu zitatokea ktk mkutano wao. Wakaomba ulinzi wa kutosha wa Jeshi la Polisi. Pamoja na kutoa taarifa polisi na polisi kuwepo, bado vurugu hizo zilitokea na mtu akafa katka mazingira ya kutatanisha viongozi hao wakiwa wameshaondoka. (Singida polisi hawakuhusishwa, lakini ndipo kulipo na ile kambi ya vijana wa ccm iliyofichuliwa na Dr Slaa). Baadaye polisi na ccm wakajenga mazingira ya kukihusisha Chadema. Chadema walipeleka hoja hiyo bungeni ili ijadiliwe kwa undani na ukweli ujulikane, wakakwama pamoja na kuiweka kwa urefu ktk maoni ya msemaji wa kambi hiyo – walizuiwa kusoma. Kitu gani kinafichwa?

Morogoro.
Morogoro polisi waliua. Mashuhuda wapo. Polisi ikajiundia kamati ya kujichunguza chap chap na kuleta matokeo feki kwa kiwango cha kutia aibu. Pili, kwa mujibu wa taarifa zilizotoka Jf na baadhi ya magazeti kuna tetesi za wanandugu kushawishiwa ili kuichafuaChadema. Sakata hili lina maswali ya kujiuliza kama ifuatavyo. Kwa nini Chadema walikwekewa mizengwe kushiriki msiba huo. Kwanini wanandugu marehemu Ali ambao mwanzoni walikuwa wanaandaa mazishi na Chadema wakageuka ghafla kukitumia msiba huo dhidi ya Chadema kama hakuna mkono wa ccm na serikali? Tatu, ni lini ccm na serikali walikaa na kuwashawishi wanandugu wa Marehemu Ali dhidi ya Chadema ktk kipindi kifupi namna hii kama hamna maandalizi kabla ya kifo? Ktk siku mbili waliwezaje kulifuatilia asili yake na wakawa tayari kwenda mkoa wa Tanga kutafuta ndugu zake kuwashawishi vinginevyo? Naomba kushawishiwa kuwa yote haya hayana maandalizi ya kabla.
Mmoja ya comment hapa chini [QUOTE=Ndukidi; Siku tatu kabla ya mkutano wa Morogoro Nape Nnauye akongea kwenye radio moja, alisikika akishauri wananchi wa Morogoro wasiende kwenye mkutano wa CDM kwani kutatokea vurugu na wanaweza kuumia.. alikuwa anaongea kama vile kuna mpango funali, nilikuwa namsikiliza na watu wengine , kuna mtu akasema mbona anaongea hivi , au wamepanga kufanya vurugu.. kilichotokea baada ya hapo wote tunajua...
Binafsi namini huu ni mkakati wa serikali kutaka ama kufuta CDM, au kupiga vita mikutano ya CDM kabisa.




Sababu 3 zinazohalalisha kuwa vifo hivi vina msukumo nyuma yake.
Chadema ilipoanza operesheni hii Morogoro baada ya ile ya kwanza kufanikiwa sana (tena huko mtwara na Lindi) ilikutana na mizengwe Mingi sana ya kukwamisha zoezi hili. Polisi walikuja na hoja nyingi sana dhaifu. Mara polisi wachache, mara kuna vyama vingine vimeomba kufanya mikutano nk. Chadema wakalazimika kwenda morogoro vijijini na kuahirisha morogoro mjini kwa muda. Maswali ya kujiuliza, Je, polisi walikuwa wanazuia mikutano kwa hoja dhaifu kwa msukumo wa nani? Je, tuamini kwamba baada ya kushindwa kuzuia mikutano ccm hawana plan B? Kama ipo ni ipi? Vifo hivi na utata wake vipi? Ni hoja yangu kuwa baada ya kukwama kuzuia mikutano husika wasingeweza kukaa kimya. Lazima wangekuja na mikakati mipya kama hii tunayoiona. Nashawishika kuamini kuwa wana mkono ktk vifo.

Nikisema kwamba Serikali ikishindwa kutunga sheria ya kuzuia na kuthibiti mikutano hii, watatumia vifo hivi vyenye utata kuzuia mikutano husika, nitakosea? Je, wahisani na wananchi watawaelewa? Ni suala la Muda tu.
Je, kauli ya wasira kuwa tunaweza kuifuta Chadema inawaandaa wananchi kwa lipi? Je, mkakati wa kulifanikisha hilo ni upi? Nikidhania kwamba vifo hivi ni njia mmojawapo nitakosea? Je, baada ya CD ya ukabila, udini na ukanda kuchuja hii CD mpya ya vurugu itauza? Je, yote haya lengo lake ni nini? Kuifuta Chadema kama alivyosema wasira? Kuichafua ikataliwe na wananchi au kutisha wananchi wagomee mikutano yake na kuidhoofisha? Time will tell.

NB; Ikumbukwe, kiwango cha kukataliwa kwa ccm kabla na baada ya Uchaguzi wa Arumeru kinazidi kupanda. Hivyo ingekuwa ni jambo la kushangaza kwamba wakaamua kufa kibudu. Tafakari. [/QUOTE]

Kila mwenye akili timamu anafahamu kuwa huo ndio ukweli wenyewe!!
 
Mwaka huu mbona magamba yataaibika na hizo sheria kandamizi hatutazikubali


Nakubaliana na wewe ila hatutazikataa sheria hizo kwa kuandika tu JF kama tunavyofanya mimi na wewe basi. Lazima tuunge mkono juhudi za viongozi wetu baada ya kuandika humu. Nashawishika kuamini kwamba mpaka leo hapa JF kuna wafuasi wazuri sana wa Chadema ambao ninaamini hawajachangia M4C hata mara mmoja. Hii inarudisha nyuma juhudi za kujikomboa na tunaendelea kupewa huduma mbovu na kuuawa.
 
And that makes you what? Dr Slaa who persue poor youth to riot while he remained in his hotel room shaging waitres?


Nawasihi wanajf kwa leo tusijadili hoja ya Ecoli maana anatutoa kwenye mjadala muhimu sana. Tunajadili hatma ya maisha yetu na watoto wetu na nchi yetu kwa ujumla. Mtu mwingine naomba asimjibu. Hii ndo mbinu ya kuharibu mjadala ya watu ambao wako kwenye pay roll ya Nape Nnauye.
 
Angalieni picha kwenye mwananchi, yule askali ndio kashutu mwanahabari live ananekana

Mkuu andrewk Kwa kweli kama tuna vyombo huru vya kufuatilia haki ile picha ni ushahidi tosha. Mtuhumiwa yupo mikononi mwa polisi lakini bado askari wanampiga sasa nini maana ya kuwa mikononi mwa polisi.Halafu yule askari aliemuelekeza mtutu hivi hajui bunduki inaweza kufyatuka katika purukushani kama ile!
 
Last edited by a moderator:
Kwanini unatumia nguvu kuisafisha policcm wakati Nape ni shahidi kuwa haya mambo yamepangwa ili kuhiujumu cdm!

Yaani sababu zote zinaitoa CDM kwenye picha. Kwa nini unatumia nguvu kuisafisha kama tayari ni safi? Wananchi wana akili wanajua ukweli.
 
Back
Top Bottom