Sababu 3 zilizonyuma ya vifo ktk mikutano ya Chadema,mtumishi wa Serikali anitonya

mara zote hapa jukwaani nimekuwa nikisema, serikali ya CCM kama zilivyo serikali nyingine ulimwenguni wanaanda matatizo ili kuja kuyatatua hayo matatizo dhumuni kubwa ni kuchanganya akili za wananchi wao ili kuwajengea hofu na uoga
 
Wakuu,
Kuna sababu tatu za kutokea kwa vifo ktk mikutano ya Chadema . Sababu ya kubwa ya kwanza iliyonifanya hata leo nilete uzi huu hapa ni maelezo ya rafiki yangu anayefanya kazi ktk mmoja ya taasisi za serikal akinitonya kwamba, serikali inataka kutunga sheria ya kuzuia ama kuthibiti mikutano ya hadhara na maandamano kama ilivyokwisha dokezwa na mwanasheria mkuu wa serikali Bungeni. Tatizo kubwa ambalo linawakabili mpaka sasa serikalini, ni kukubalika kwa sheria hiyo mbele ya Umma. Hii inatokana na baadhi ya maofisa (yeye amewaita objective) wanadhani kwamba itapingwa sana na vyama vya siasa na hata wananchi hawataiunga mkono sheria husika. Mmoja ya mapendekezo ni kwamba ili kupunguza vurugu na usumbufu ktk mikutano na maandamano, viogozi wasiruhusiwe kwenda kwenye majimbo yasiyo yao kisheria (Hoja ya Anne Kilango Bungeni) bila kupata ruhusa na bila sababu inayoeleweka. Huyo bwana akasema, nina wasiwasi na vifo hivi na harakati zinaendelea huku serikalini za kuhalalisha sheria hiyo ambayo yeye pamoja na kufanya kazi kwa miaka mingi serikalini, ana ona kama ni mbovu kabla hata draft ya kwanza yenyewe haijaandaliwa.

Hoja ya pili kubwa sana ni hao Maofisa objective wanaopinga sheria hiyo, wanadhani kwamba sheria hiyo itagombanisha serikali na wafadhili kiasi cha kuzuia misaada na mikopo. Hoja hii ya pili ya wapinzani wa sheria hii ndio yenye nguvu kuliko kuliko ile ya kwanza. Sasa yeye ananiuliza, hebu fanyeni utafiti isijekuwa yanajengwa mazingira ya kuwalainisha wahisani na kuhalalisha sheria hiyo kabla sheria haijatungwa na hamjazuiwa kufanya shughuli zenu za kisiasa.
Kwa maoni yake japokuwa hana ushahidi, vifo hivi na utata unaozingira vifo vyenyewe kunaweza kuwa na uhusiano na taarifa zake. (Hayo ni ya rafiki yangu aliyoniambia)


Sababu ya 2; Vifo vya Singida na Morogoro, kwa nini vinaweza kuwa na mkono wa mtu.
Kifo cha Singida kwa kiwango kikubwa ina halalisha (justify) maelezo ya huyo rafiki yangu. Hii ni kwa sabau, Katika mikutano iliyofanyika Singida, viongozi wa Chadema walipata taarifa kuwa vurugu zitatokea ktk mkutano wao. Wakaomba ulinzi wa kutosha wa Jeshi la Polisi. Pamoja na kutoa taarifa polisi na polisi kuwepo, bado vurugu hizo zilitokea na mtu akafa katka mazingira ya kutatanisha viongozi hao wakiwa wameshaondoka. (Singida polisi hawakuhusishwa, lakini ndipo kulipo na ile kambi ya vijana wa ccm iliyofichuliwa na Dr Slaa). Baadaye polisi na ccm wakajenga mazingira ya kukihusisha Chadema. Chadema walipeleka hoja hiyo bungeni ili ijadiliwe kwa undani na ukweli ujulikane, wakakwama pamoja na kuiweka kwa urefu ktk maoni ya msemaji wa kambi hiyo – walizuiwa kusoma. Kitu gani kinafichwa?

Morogoro.
Morogoro polisi waliua. Mashuhuda wapo. Polisi ikajiundia kamati ya kujichunguza chap chap na kuleta matokeo feki kwa kiwango cha kutia aibu. Pili, kwa mujibu wa taarifa zilizotoka Jf na baadhi ya magazeti, kuna tetesi za wanandugu kushawishiwa ili kuichafuaChadema. Sakata hili lina maswali ya kujiuliza kama ifuatavyo. Kwa nini Chadema walikwekewa mizengwe kushiriki msiba huo. Kwanini wanandugu wa marehemu Ali ambao mwanzoni walikuwa wanaandaa mazishi vizuri na Chadema wakageuka ghafla na kutumia msiba huo dhidi ya Chadema kama hakuna mkono wa ccm na serikali? Tatu, ni lini ccm na serikali walikaa na kuwashawishi wanandugu wa Marehemu Ali dhidi ya Chadema ktk kipindi kifupi namna hii kama hamna maandalizi, kabla ya kifo? Ktk siku mbili waliwezaje kulifuatilia asili yake na wakawa tayari kwenda mkoa wa Tanga kutafuta ndugu zake kuwashawishi? Naomba kushawishiwa kuwa yote haya hayana maandalizi ya kabla.
Mmoja ya comment hapa chini [QUOTE=Ndukidi; Siku tatu kabla ya mkutano wa Morogoro Nape Nnauye akongea kwenye radio moja, alisikika akishauri wananchi wa Morogoro wasiende kwenye mkutano wa CDM kwani kutatokea vurugu na wanaweza kuumia.. alikuwa anaongea kama vile kuna mpango funali, nilikuwa namsikiliza na watu wengine , kuna mtu akasema mbona anaongea hivi , au wamepanga kufanya vurugu.. kilichotokea baada ya hapo wote tunajua...
Binafsi namini huu ni mkakati wa serikali kutaka ama kufuta CDM, au kupiga vita mikutano ya CDM kabisa.




Sababu # 3; inazohalalisha kuwa vifo hivi vina msukumo nyuma yake.
Chadema ilipoanza operesheni hii Morogoro baada ya ile ya kwanza kufanikiwa sana (tena huko mtwara na Lindi) ilikutana na mizengwe Mingi sana ya kukwamisha zoezi hili. Polisi walikuja na hoja nyingi sana dhaifu. Mara polisi wachache, mara kuna vyama vingine vimeomba kufanya mikutano nk. Chadema wakalazimika kwenda morogoro vijijini na kuahirisha morogoro mjini kwa muda. Maswali ya kujiuliza, Je, polisi walikuwa wanazuia mikutano kwa hoja dhaifu kwa msukumo wa nani? Je, tuamini kwamba baada ya kushindwa kuzuia mikutano ccm hawana plan B? Kama ipo ni ipi? Vifo hivi na utata wake vipi? Ni hoja yangu kuwa baada ya kukwama kuzuia mikutano husika wasingeweza kukaa kimya. Lazima wangekuja na mikakati mipya kama hii tunayoiona. Nashawishika kuamini kuwa wana mkono ktk vifo hivi.

Nikisema kwamba Serikali ikishindwa kutunga sheria ya kuzuia na kuthibiti mikutano hii, watatumia vifo hivi vyenye utata kuzuia mikutano husika, nitakosea? Je, wahisani na wananchi watawaelewa? Ni suala la Muda tu.
Je, kauli ya wasira kuwa tunaweza kuifuta Chadema inawaandaa wananchi kwa lipi? Je, mkakati wa kulifanikisha hilo ni upi? Nikidhania kwamba vifo hivi ni njia mmojawapo nitakosea? Je, baada ya CD ya ukabila, udini na ukanda kuchuja hii CD mpya ya vurugu itauza? Je, yote haya lengo lake ni nini? Kuifuta Chadema kama alivyosema wasira? Kuichafua ikataliwe na wananchi au kutisha wananchi wagomee mikutano yake na kuidhoofisha? Time will tell.

NB; Ikumbukwe, kiwango cha kukataliwa kwa ccm kabla na baada ya Uchaguzi wa Arumeru kinazidi kupanda. Hivyo ingekuwa ni jambo la kushangaza kwamba wakaamua kufa kibudu. Tafakari. [/QUOTE]


Mkuu mbona hakuna kitu zaidi ya yale yale tuliyo yazoea kila siku? Hii habari yaonyesha ni yakutungwa na kama JF watakuwa wanaruhusu habari za kutungwa kwa maslahi ya kukibeba chama cha cdm ili hali aliyeitoa habari hii ni kiongozi wake basi tunapoteza mwelekeo na hadhi ya JF. Mie kesho nikitunga habari nyingine tunakwenda wapi ? Nilitegemea umtaje huyo mtu ili tukuamini na hoja yako iwe na mashiko, kwa hivi tu hakuna tu kajipange upya
 
Tusubiri tu wakati hawa wapangaji wa ikulu wamechoka kufikiri nasi tutawafundisha namna ya kufikiri sawasawa 2015 sio mbali wacha waendelee kutupa mzuka wa kuwachukia. Itafahamika tu
 
Everyone is crying out for peace yes
None is crying out for justice
(2x)

(CHORUS)
I don't want no peace
I need equal rights and justice (3x)
Got to get it
Equal rights and justice

Everybody want to go to heaven
But nobody want to die
Everybody want to go to up to heaven
But none o them (2x) want to die

CHORUS
(Just give me my share)

What is due to Caesar
You better give it on to Caesar
And what belong to I and I
You better (2x) give it up to I

CHORUS
(I'm fighting for it)

Everyone heading for the top
But tell me how far is it from the bottom
Nobody knows but
Everybody fighting to reach the top
How far is it from the bottom

CHORUS

Everyone is talking about crime
Tell me who are the criminals
I said everybody's talking about crime, crime
Tell me who, who are the criminals
I really don't see them

CHORUS

There be no crime
Equal rights and justice (Precedes each line below)
There be no criminals
Everyone is fighting for
Palestine is fighting for
Down in Angola
Down in Botswana
Down in Zimbabwe
Down in Rhodesia
Right here in Jamaica

by Peter Tosh.

I and I man,datz di trut man.Whatta gwon in dis world man,dem guys wanna get di bigger cake man and leave us wit noting man. Selassie Jah man.
 
Ipo siku Polisi nao watasema CCM siyo mama yangu wala Siyo baba yangu, litabakia Jeshi tu ambalo halina mkono mreefu kama wa Polisi kwenye kukandamiza upinzani, lakini sitashangaa siku hata jeshi likianza kuamuru watu wasikusanyike kwenye mikutano.
 
Hiv ndo kusema ni kweli ccm wana ndoto za kutawala milele? vipi watakapoondoka 2015 watabadili tena hiyo sharia yao ili iwe upande wao kama wapinzani?
 
Somo zuri sana.
Ukweli mtupu.

upuuzi mtupu. Wa- tz wanaendelea na sensa, wewe na ucharu wako unafanya mikutano ya hadhara. Ulikuwa wapi kufanya mikutano hiyo kuwaamasisha waislamu wasiigomee sensa. Kama kweli unaipenda nchi hii wakati huu si wakati wa mikutano ya hadhara hadi sensa ipite.

tena ndugu zangu nawapa taadhali sana, kuenda huko ni kwenda kujitafutia kuwa "sacrifice" za madaraka ya watu. Kwani walishajitangazia uwekundu ktk bendera yao. Kitu ambacho wahenga wetu walikubaliana kuwa kisiwepo ktk flag yetu. lakini kwa vichwa vyao vigumu wanasisitiza kuwepo kwa rangi hiyo.

Niaminivyo Slaa ni picha tu pale, wanywa damu na waroho kwa sasa wamejificha kabisa wakiwauwa mmoja mmoja kama kafara kwa kila mkoa hadi mikoa yote imalizike.

M4C hhhhoooyyyyeeeeeeee!!!!!
 
Kuna wahusika wanne, Serikali (CCM), Polisi, Chadema na sis wenye nchi, kama hoja hizo ni za kweli, nin Jukumu letu (Tufanyeje)??? Tumuamini nan kati ya hao?? Naona kichwa kinauma kwa kuitafakar hii miaka mitatu iliyobaki..!!
 
mkuu tumekupata lakini hata mbaraka alijigamba sana lakini muda ulipofika leo hii yuko wapi? ccm inge watawala wengi wa africa ambao leo hii ni marehemu au wanasota magerezani
 
Sababu ya 2; Vifo vya Singida na Morogoro, kwa nini vinaweza kuwa na mkono wa mtu.
Kifo cha Singida kwa kiwango kikubwa ina halalisha (justify) maelezo ya huyo rafiki yangu. Hii ni kwa sabau, Katika mikutano iliyofanyika Singida, viongozi wa Chadema walipata taarifa kuwa vurugu zitatokea ktk mkutano wao. Wakaomba ulinzi wa kutosha wa Jeshi la Polisi.


Morogoro.
Morogoro polisi waliua. Mashuhuda wapo. Polisi ikajiundia kamati ya kujichunguza chap chap na kuleta matokeo feki kwa kiwango cha kutia aibu. Pili, kwa mujibu wa taarifa zilizotoka Jf na baadhi ya magazeti, kuna tetesi za wanandugu kushawishiwa ili kuichafuaChadema. Sakata hili lina maswali ya kujiuliza kama ifuatavyo. Kwa nini Chadema walikwekewa mizengwe kushiriki msiba huo. Kwanini wanandugu wa marehemu Ali ambao mwanzoni walikuwa wanaandaa mazishi vizuri na Chadema wakageuka ghafla na kutumia msiba huo dhidi ya Chadema kama hakuna mkono wa ccm na serikali? Tatu, ni lini ccm na serikali walikaa na kuwashawishi wanandugu wa Marehemu Ali dhidi ya Chadema ktk kipindi kifupi namna hii kama hamna maandalizi, kabla ya kifo? Ktk siku mbili waliwezaje kulifuatilia asili yake na wakawa tayari kwenda mkoa wa Tanga kutafuta ndugu zake kuwashawishi? Naomba kushawishiwa kuwa yote haya hayana maandalizi ya kabla.

Mkuu kimantiki, hatuwezi kubishana na hoja yako kwamba vurugu na mauwaji haya ni mpango wa ccm na mashine zake. Ni vigumu kuamini eti CCM watakuwa tayari kuona wanateketea kama mshumaa bila kuchukua hatua yeyote. Niliwahi kujiuliza kuwa CCM watatumia uwanja gani kujibu mapigo ya CDM katika kasi hii, na watatumia hadhira ipi? Sikuwahi kupata jibu. Kwanye hili na sioni uwanja uliotambarare kwa CCM kuwa na ubavu wa kufanya hili.

Vifo hivi ni matokeo ya mipango isiyokuwa na mashiko ya ccm na mashine zake, ila kama ilivyo mipango ya wengi waliofilisika (tawala zinazofikia mwisho), huishia kuwa na madhara kwa wasiostahili na kuonekana ya kipuuzi na fedheha kubwa kwa taifa. Hivyo, mauwaji haya yamekuwa yakitokea kutokana na kutotumia busara pamoja na matumizi ya nguvu kubwa ambavyo hupelekea nafasi kubwa za kutokea madhara makubwa ikiwa ni pamoja na vifo. Ni vigumu kusema kuwa familia ya Ali pamoja na CCM walifahamu juu ya kifo cha Ali kabla hakijatokea, ila mipango ya kuikwamisha CDM kushiriki mazishi haya ni matokeo ya ubora wa mawasiliano na historia ambayo bado inaonyesha muamko wa eneo atokalo marehemu Ali (Muheza, Tanga) bado ni miongoni mwa maeneo yaliyotekwa nyara vya kutosha na CCM.

Kujairibu kuipaka matope mikutano ya CDM ili ionekana kuwa ni ya vurugu, na hivyo kutoa mwanya wa kupitisha sheria kandamizi, hilo sio ajabu. Kama wameweza kuhuriri ukabila, udini na mauwaji ya kimbari Rwanda kama njia za kuwatisha wananchi, Watashindwaje kuwatisha na hili la vurugu? Bahati mbaya waliyonayo ni kuwa sasa wananchi wanaona zaidi ya kusikia na wamepata uelewa ambao hawamtegemei JK atizame TV ikulu aje awahutubie kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi.

Ndugu yangu Aweda, hivi ni vita tena vikali. Hii nchi inamilikiwa na kundi la wanyanganyi wachache waliowaajiri maharamia wachache kuwalindia mali yao, hivyo basi sio rahisi wakubali kuona nchi waliojiridhisha inarejea mikononi mwa wananchi. Watapigana sana kwa kisingizio cha kulinda amani, ila ni kwa ajili ya kulinda maslahi yao na vizazi vyao.

Yatupasa tuchukue hatua, ikiwa ni kundeleza moto. Kama tulikuwa tunatumia mafuta ya taa sasa basi na tutumie petrol, kuhakikisha kasi ya M4C inakolea zaidi. Kama tujuavyo wao ccm wana majeshi, hadi mahakama ambavyo sasa wamekuwa sio walinzi wetu tena, ila wauwaji wetu. Je, sis tumebaki na nini?
 
Kama hana ushahidi basi hadithi yote hiyo ya nini? Hizi ni porojo zako na huyo karani wa serikalini.
 
Kwa hili sasa, hakuna mgogoro kati ya CDM na POLISI, ila kuna vurugu kati ya POLISI na RAIA wasio na hatia, tunaona kilicho tokea MOROGORO ni RAIA asie na hatia ndio wamemuua, Iringa pia wameludia usenge huo huo DHIKI KUU INAWANYEMELEA CCM pamoja POLISI.
 
kama sijakuelewa vile vurugu kati polisi na raia na sio chadema..!?? Kwa hiyo wanaohujumiwa ni raia na sio chadema.!
 
Nakubaliana nawe ! CDM si sehemu ya vurugu ila ni viongozi majuha wa jeshi hilo wanaotuma vijana kuua ! Inakera sana
 
Machozi yamenitoka kwa maauji ya IRINGA na MOROGORO

jikaze mkuu acha kulia lia beba silaha twende mbele kusaka uhuru kwani hata mkoloni mweupe aliua lakini hakumwaga utumbo kama vile huyu mkoloni mweusi(ccm) sijui kajifunza wapi......kamata silaha tukapambane ukifa au nikifa weka mzoga wangu pembeni songeni mbele na mapambano....mwangosi amepambana damu yake ni chachu kwetu...ole wake anaye cheka sasa maana kesho atasaga meno na kulia,mafisadi wacheke leo lakini 2016..............!God know
 
Bother hayavumiliki haya roho inauma
jikaze mkuu acha kulia lia beba silaha twende mbele kusaka uhuru kwani hata mkoloni mweupe aliua lakini hakumwaga utumbo kama vile huyu mkoloni mweusi(ccm) sijui kajifunza wapi......kamata silaha tukapambane ukifa au nikifa weka mzoga wangu pembeni songeni mbele na mapambano....mwangosi amepambana damu yake ni chachu kwetu...ole wake anaye cheka sasa maana kesho atasaga meno na kulia,mafisadi wacheke leo lakini 2016..............!God know
 
Kitu ambacho muda wote serikali wanacheza vibaya katika sakata la vifo kwenye matukio ya CDM ni kuwa upande wa wauaji moja kwa moja kiasi cha kushindwa hata ku-fake.Hakika hili ndilo linafanya waTZ wengi waamini wao ndio walioruhusu.
 
Back
Top Bottom