Sababu 3 zilizonyuma ya vifo ktk mikutano ya Chadema,mtumishi wa Serikali anitonya

Kwanini unatumia nguvu kuisafisha policcm wakati Nape ni shahidi kuwa haya mambo yamepangwa ili kuhiujumu cdm!

Kwa kuzingatia comment ya ndukidi hapo juu ( Nape on Radio), na kwa kuangalia picha zilizoko hapa JF na gazeti la mwananchi, nahitaji kushawishiwa vinginevyo kuwa Kifo cha Daudi Mwangosi haikupangwa. Nakataa, kwa maoni yangu imepangwa. Swali ni je, Viongozi wa harakati hizi wako salama kiasi gani?
 
Aweda thanks,

Haya uliyoyasema kulingana na mlivyozungumza na huyo rafiki yako aliyeko kwenye mojawapo ya taasisi za serikali yana ukweli kwa 99.99%.
Kwa mtu yeyote aliye na akili timamu atagundua kuwa vurugu na mauaji yanayotokea kwenye mikutano ya CHADEMA mikakati ya CCM iliyoratibiwa kwa makusudi ili kutaka kuisambaratisha CHADEMA! Ni dhahiri kuwa baada ya CCM kuona nguvu ya CDM inaongezeka kila kukicha kwa kujizolea umaaarufu wameona waje na mpango wa KUUA KWA MAKUSUDI KWENYE KILA MKUTANO WA CHADEMA ILI IONEKANA KUWA CHADEMA NI CHAMA CHENYE VURUGU!

Tukichukulia haya mauaji ya Morogoro na Iringa ni wazi kabisa kuwa yalipangwa na CCM wakishirikiana na POLISI! Pale Morogoro tuliambiwa kuwa marehemu aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito siyo bomu la machozi wala risasi za moto. Maana ni kwamba CHADEMA ndiwo waliomwua marehemu kwa kumpiga na kitu kizito!!!!Ikumbukwe kuwa marehemu hakuwa akiandamana wala hakuwa mwana-CDM baali alikuwa amejikalia akiiuza magezeti!

Sasa jana kule Iringa aliyeuawa naye si mfuasi wala mwana-CDM baali MWADISHI WA HABARI WA CH 10! Kuna maswali ya kujiuliza hapa. Je,huyu Mwangosi pamoja na kuwa mwandishi wa CH 10 alikuwa pia mwanachama wa CDM?Je, kama hakuwa mwanachama alikuwa akitetea CDM wasizuiwe kuandamana? Nini uhusiano wa kifo cha MWANDISHI WA HABARI na maandamano ya CDM?

Kwa kweli hatuwezi kuwa na majibu ya maswali haya. Pengine IGP Mwema,RPC Iringa ndiwo wanaweza kutupa majibu yake.Hata hivyo kwa mtazamo wa harakaharaka naweza kusoma katikatikati ya mistari kuwa hizi ni mbinu za makusudi za kutaka KUWATISHA WATANZANIA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUDHURIA AU KUJIHUSISHA NA MAANDAMANO YA CHADEMA!

Hii message imelengwa kuwafikia Wananchi wa kawaida na Waandishi wa habari kwa kuua mtu kutoka kila kundi! Mesage ni kwamba kama wewe ni Mtanzania huruhusiwi kwenda kwenye maandamano ya Upinzani hasa CHADEMA. Vilevile kama wewe ni mwandishi wa habari wa chombo cha habari cha binafsi huruhusiwi kwenda kuandika taarifa za mkutano wa CDM kwa hali yoyote ile maana ukithubutu tu basi hakika UTAKUFA! Lakini kwa vyombo vya habari vya serikali kama TBC(radio&tv) na magazeti yake ya Uhuru,Mzalendo,The DailyNews,Habari Leo na mengineyo yenye uhusiano wa karibu na CCM kama Rai la Rostam Azizi hayawezi kuzuiliwa wala Waandishi wake kuuawa kinyama maana wao lazima wataandika kile walichoelekezwa na hao mabwana zao(CCM & Serikali yake).

Kuna kauli nyingi zimetolewa na vigogo wa CCM na zinaendelea kutolewa zenye mwelekeo wa kutaka aidha KUIFUTA CHADEMA kama chama cha siasa au KUZUIA MIKUTANO YAKE. Kauli ya Mwanasheria wa serikali bungeni ya kukusudia kutaka kuzuia mikutano ya vyama vya siasa tumeshaisikia na pia kauli ya kutaka KUIFUTA CHADEMA iliwahi kutolewa na Msajili wa Vyama vya siasa Bwana John Tendwa na Waziri wa Ofisi ya Rais-Mahusiano Bwana Steven Wassira! Kauli hizi si za kubeza hata kidogo. Bado kuna kauli za watu kama Januari Makamba kwamba Wapinzani hawawezi kushika Dola,wanachoweza kufanya ni kusajili Wanachama tu maana hawana uwezo! Kauli hii inaenda sambamba na ile ya Bwana S am Sitta kuwa CHADEMA hawana viongozi wa kuwawezesha kuongoza nchi. Kwamba CDM kiongozi waliyenaye ni Dr. Slaa tu maana Mwenyekiti wao wa Taifa ni DJ wa kumbi za starehe! Hizi ni propaganda tunaweza kuziita ni za kishenzi kama siyo za kihuni! Maana haiwezekani CDM chama chenye kuwakilisha Kambi ya Upinzani Bungeni-KUB useme hakina viongozi!

Hakuna Mtanzania atakayedanganyika na longolongo hizi za CCM. Ukweli unabakia kuwa CHADEMA ni tishio kwa CCM kwasababu kinaonekana kina Viongozi makini,weledi na wenye upeo mkubwa wa kuchanganua na kunyumbulisha mambo. Dr.Slaa- Katibu Mkuu wa chama mpaka sasa hayuko ndani ya Bunge lakini Watanzania wameshuhudia Bunge likiwashwa moto na Wabunge 45 akiwemo Mwenyekiti wa Taifa-CDM Mhe.Freeman Mbowe!CDM kimejijengea umaarufu mkubwa kwenye Bunge la Tanzania kwa kuibua na kuleta hoja motomoto na zenye changamoto kubwa Bungeni. CDM kina Wabunge ambao ni Mawaziri vivuli ambao wanaweza kuwa Mawaziri kamili kama CDM watashika Dola!

CCM wanajidanganya kuwa wao peke yao ndiyo wenye uwezo na akili ya kuongoza nchi hii kitu ambacho si kweli. Viongozi na Wabunge wa CHADEMA ni Watanzania na wana haki sawa ya kushika uongozi wowote wa nchi hii bila kijali itikadi za chama! Kila Mtanzania ana haki ya kushika uongozi wa nchi hii kwa mjibu wa Katiba na sheria za nchi hii. Hakuna mahali popote kwenye Katiba ya Tanzania panaposema kuwa Kiongozi yeyote wa nchi hii lazima awe mwanachama wa CCM!!!??CCM wanataka tuamini uongo wao huo. Tunasema hatudanganyiki.

CCM wanatakiwa siyo kuombwa waruhusu Demokrasia ichukue mkondo wake. Udikteta kamwe hautawasaidia CCM sana sana unazidi kukidhalilisha chama hiki ambacho kwa uhakika kabisa kiko ICU kikipumulia mashine. Very soon kitakufa na kuzikwa kama mbwa na maandishi kwenye Tombstone yatasomeka kama ifuatavyo:

CCM R.I.P.
BORN: 1977 DIED: 2015
 
Respect kamanda,uchambuzi ni mzuri unaeleweka....ALUTA CONTINUE!!!!
 
Nakubaliana na wewe ila hatutazikataa sheria hizo kwa kuandika tu JF kama tunavyofanya mimi na wewe basi. Lazima tuunge mkono juhudi za viongozi wetu baada ya kuandika humu. Nashawishika kuamini kwamba mpaka leo hapa JF kuna wafuasi wazuri sana wa Chadema ambao ninaamini hawajachangia M4C hata mara mmoja. Hii inarudisha nyuma juhudi za kujikomboa na tunaendelea kupewa huduma mbovu na kuuawa.

mkuu hapo umenena.
 
Yaani sababu zote zinaitoa CDM kwenye picha. Kwa nini unatumia nguvu kuisafisha kama tayari ni safi? Wananchi wana akili wanajua ukweli.
Haya ndo matatizo ya kuongea ukiwa na mavi mdomoni kama picha yako inavyojieleza....gamba mkubwa.
 
Wakuu,
Kuna sababu tatu za kutokea kwa vifo ktk mikutano ya Chadema . Sababu ya kubwa ya kwanza iliyonifanya hata leo nilete uzi huu hapa ni maelezo ya rafiki yangu anayefanya kazi ktk mmoja ya taasisi za serikal akinitonya kwamba, serikali inataka kutunga sheria ya kuzuia ama kuthibiti mikutano ya hadhara na maandamano kama ilivyokwisha dokezwa na mwanasheria mkuu wa serikali Bungeni. Tatizo kubwa ambalo linawakabili mpaka sasa serikalini, ni kukubalika kwa sheria hiyo mbele ya Umma. Hii inatokana na baadhi ya maofisa (yeye amewaita objective) wanadhani kwamba itapingwa sana na vyama vya siasa na hata wananchi hawataiunga mkono sheria husika. Mmoja ya mapendekezo ni kwamba ili kupunguza vurugu na usumbufu ktk mikutano na maandamano, viogozi wasiruhusiwe kwenda kwenye majimbo yasiyo yao kisheria (Hoja ya Anne Kilango Bungeni) bila kupata ruhusa na bila sababu inayoeleweka. Huyo bwana akasema, nina wasiwasi na vifo hivi na harakati zinaendelea huku serikalini za kuhalalisha sheria hiyo ambayo yeye pamoja na kufanya kazi kwa miaka mingi serikalini, ana ona kama ni mbovu kabla hata draft ya kwanza yenyewe haijaandaliwa.

Hoja ya pili kubwa sana ni hao Maofisa objective wanaopinga sheria hiyo, wanadhani kwamba sheria hiyo itagombanisha serikali na wafadhili kiasi cha kuzuia misaada na mikopo. Hoja hii ya pili ya wapinzani wa sheria hii ndio yenye nguvu kuliko kuliko ile ya kwanza. Sasa yeye ananiuliza, hebu fanyeni utafiti isijekuwa yanajengwa mazingira ya kuwalainisha wahisani na kuhalalisha sheria hiyo kabla sheria haijatungwa na hamjazuiwa kufanya shughuli zenu za kisiasa.
Kwa maoni yake japokuwa hana ushahidi, vifo hivi na utata unaozingira vifo vyenyewe kunaweza kuwa na uhusiano na taarifa zake. (Hayo ni ya rafiki yangu aliyoniambia)


Sababu ya 2; Vifo vya Singida na Morogoro, kwa nini vinaweza kuwa na mkono wa mtu.
Kifo cha Singida kwa kiwango kikubwa ina halalisha (justify) maelezo ya huyo rafiki yangu. Hii ni kwa sabau, Katika mikutano iliyofanyika Singida, viongozi wa Chadema walipata taarifa kuwa vurugu zitatokea ktk mkutano wao. Wakaomba ulinzi wa kutosha wa Jeshi la Polisi. Pamoja na kutoa taarifa polisi na polisi kuwepo, bado vurugu hizo zilitokea na mtu akafa katka mazingira ya kutatanisha viongozi hao wakiwa wameshaondoka. (Singida polisi hawakuhusishwa, lakini ndipo kulipo na ile kambi ya vijana wa ccm iliyofichuliwa na Dr Slaa). Baadaye polisi na ccm wakajenga mazingira ya kukihusisha Chadema. Chadema walipeleka hoja hiyo bungeni ili ijadiliwe kwa undani na ukweli ujulikane, wakakwama pamoja na kuiweka kwa urefu ktk maoni ya msemaji wa kambi hiyo – walizuiwa kusoma. Kitu gani kinafichwa?

Morogoro.
Morogoro polisi waliua. Mashuhuda wapo. Polisi ikajiundia kamati ya kujichunguza chap chap na kuleta matokeo feki kwa kiwango cha kutia aibu. Pili, kwa mujibu wa taarifa zilizotoka Jf na baadhi ya magazeti, kuna tetesi za wanandugu kushawishiwa ili kuichafuaChadema. Sakata hili lina maswali ya kujiuliza kama ifuatavyo. Kwa nini Chadema walikwekewa mizengwe kushiriki msiba huo. Kwanini wanandugu wa marehemu Ali ambao mwanzoni walikuwa wanaandaa mazishi vizuri na Chadema wakageuka ghafla na kutumia msiba huo dhidi ya Chadema kama hakuna mkono wa ccm na serikali? Tatu, ni lini ccm na serikali walikaa na kuwashawishi wanandugu wa Marehemu Ali dhidi ya Chadema ktk kipindi kifupi namna hii kama hamna maandalizi, kabla ya kifo? Ktk siku mbili waliwezaje kulifuatilia asili yake na wakawa tayari kwenda mkoa wa Tanga kutafuta ndugu zake kuwashawishi? Naomba kushawishiwa kuwa yote haya hayana maandalizi ya kabla.
Mmoja ya comment hapa chini [QUOTE=Ndukidi; Siku tatu kabla ya mkutano wa Morogoro Nape Nnauye akongea kwenye radio moja, alisikika akishauri wananchi wa Morogoro wasiende kwenye mkutano wa CDM kwani kutatokea vurugu na wanaweza kuumia.. alikuwa anaongea kama vile kuna mpango funali, nilikuwa namsikiliza na watu wengine , kuna mtu akasema mbona anaongea hivi , au wamepanga kufanya vurugu.. kilichotokea baada ya hapo wote tunajua...
Binafsi namini huu ni mkakati wa serikali kutaka ama kufuta CDM, au kupiga vita mikutano ya CDM kabisa.




Sababu # 3; inazohalalisha kuwa vifo hivi vina msukumo nyuma yake.
Chadema ilipoanza operesheni hii Morogoro baada ya ile ya kwanza kufanikiwa sana (tena huko mtwara na Lindi) ilikutana na mizengwe Mingi sana ya kukwamisha zoezi hili. Polisi walikuja na hoja nyingi sana dhaifu. Mara polisi wachache, mara kuna vyama vingine vimeomba kufanya mikutano nk. Chadema wakalazimika kwenda morogoro vijijini na kuahirisha morogoro mjini kwa muda. Maswali ya kujiuliza, Je, polisi walikuwa wanazuia mikutano kwa hoja dhaifu kwa msukumo wa nani? Je, tuamini kwamba baada ya kushindwa kuzuia mikutano ccm hawana plan B? Kama ipo ni ipi? Vifo hivi na utata wake vipi? Ni hoja yangu kuwa baada ya kukwama kuzuia mikutano husika wasingeweza kukaa kimya. Lazima wangekuja na mikakati mipya kama hii tunayoiona. Nashawishika kuamini kuwa wana mkono ktk vifo hivi.

Nikisema kwamba Serikali ikishindwa kutunga sheria ya kuzuia na kuthibiti mikutano hii, watatumia vifo hivi vyenye utata kuzuia mikutano husika, nitakosea? Je, wahisani na wananchi watawaelewa? Ni suala la Muda tu.
Je, kauli ya wasira kuwa tunaweza kuifuta Chadema inawaandaa wananchi kwa lipi? Je, mkakati wa kulifanikisha hilo ni upi? Nikidhania kwamba vifo hivi ni njia mmojawapo nitakosea? Je, baada ya CD ya ukabila, udini na ukanda kuchuja hii CD mpya ya vurugu itauza? Je, yote haya lengo lake ni nini? Kuifuta Chadema kama alivyosema wasira? Kuichafua ikataliwe na wananchi au kutisha wananchi wagomee mikutano yake na kuidhoofisha? Time will tell.

NB; Ikumbukwe, kiwango cha kukataliwa kwa ccm kabla na baada ya Uchaguzi wa Arumeru kinazidi kupanda. Hivyo ingekuwa ni jambo la kushangaza kwamba wakaamua kufa kibudu. Tafakari. [/QUOTE]
great thinker
 
Respect kamanda,uchambuzi ni mzuri unaeleweka....ALUTA CONTINUE!!!!

Umeeleweka siyo kwa wewe tu, hata RITZ & CO pia wameelewa. Maana walikuja kwenye uzi huu muda wa kutosha wakasepa kimya kimya. Maana yake ameelewa vizuri sana. Aluta continua

 
Umeeleweka siyo kwa wewe tu, hata RITZ & CO pia wameelewa. Maana walikuja kwenye uzi huu muda wa kutosha wakasepa kimya kimya. Maana yake ameelewa vizuri sana. Aluta continua

Nashukuru kamanda kama haya magamba umeyashika,nakuelewa sana ww ni mtu makini hata kwenye shughuli za kijamii tabata na hususani chama chetu....tupo pamoja kama askari wa miguu mpaka tuifikie nchi yetu ya ahadi iliyobakwa na haya manyang'au!!!!!
 
They will always fail in this mission, wapige mabomu na silaha zao zote lakini hatutatetereka, M4C daima.
 
Ukweli ni kuwa jamaa alikuwa na video inayoonyesha wananchi wakihama toka ktk mkutano wa c.c.m kwenda chadema baada ya kusikia slaa anafungua tawi ili kuondokana na hii aibu lengo lilikuwa ni kumnyang'anya vifaa vyake ila ndo hivo tena,na hii yote ni kutokana na chanel ten kuwa wawazi na baadhi ya mida kurusha live mikutano ya chadema.over
 
Sihitaji kukupa hints muuaji ni nani katika matukio yote haya, kauli ya Kamanda wa Police mkoa inajieleza " NAELEKEA KUSTAAFU HIVYO BADO NAKIPENDA KIBARUA CHANGU"
 
Back
Top Bottom