Saa nyingine kujenga ni uwehu

Greg50

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
1,953
2,431
Umejenga mapinga ndanindani unafanya kazi makumbusho, kutoka kwako mpaka barabarani boda 1000, dala mpaka tegeta 1000, tegeta mpaka makumbusho 500, jumla kwenda 2500, jumla kwenda na kurudi 5000. Kwa siku 6 unazofanya kazi ni 6*5000=30,000 , kwa wiki 4 ni 30,000*4= 120,000/= kwa mwezi. Jumlisha kila siku kudamka sa kumi ili uwahi kazini, na kurudi saa nne usiku kisa foleni. Jumlisha makato ya mkopo wa ujenzi 300,000/= kila mwezi katika take home yako ya 800,000/= umebakiwa na 500,000/= kwa mwezi. Kuliko kupata shida zote hizi kisa tuu kuitwa baba mwenye nyumba, ni bora ukapanga zako nyumba hapohapo makumbusho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu huko kunaitwa kujenga liability home badala ya asset home, siyo lazima uanze kujenga nyumba ya kuishi wewe mwenyewe, unaweza anza na nyumba ya kupanga ili upige kwanza hela.
 
Back
Top Bottom