S 400 ya urusi na IRONE DOME ya Israel

pia kumbuka bomu la kwanza la Nuclear Duniani ni lileee lilipiga Sodoma na Gomora Mungu alilitumia hili ....la sasa ni photo copy.

Mungu ni mzee wa vita pia....mpaka sasa.
Ulizipata biblia ipi hizi habari??
 
Dogo kumbuka Mungu alisema hivi kwa wayahudi weusi namnukuu...
Mkinikataa Mimi Mungu wenu nitanyanyua hata mawe yanitumikie! Mwisho wa nukuu..
Ndo hayo mawe sasa ya leo.
.
Sasa ndo hivi sehemu zooote za kumbukumbu ya kale kuhusu kazi ya Mungu zimefufuliwa vizuri sana na hao hao ma-zion wa leo na wanapiga hela vibaya kwa kazi ya utalii.

Kila kitu kilicho kwa Biblia pale uyahudi ya leo utakuta kumbukumbu yake.

Unauwezo nenda huna tulia tukupe fact tuliofika. Gethsimane. Maji aliyo kanyaga Yesu akatembea juu yapo unaruhusiwa kuchota kidogo...ukaone maajabu yake.

Infact km Weye ni msomaji wa Biblia mzuri utaona mengi ya kweli.
King Solomon temple ruins ipo mpaka kesho....


Ndo hayo. Km hujui Biblia na hujawahi kuisoma utaona kizungu zungu tu kula vihepe ulale...umepitwa.
Na kamwe hawataguswa na paka yeyote!!
Uleee ufunuo wa Yohana utatimia baadaye sana.siyo kwa wkt huu!! Hao ndo yaleee mawe aliyo sema Mungu tena kwa kauli yake mwenyewe....sasa pinga Mungu uone moto!Babuu...
King Solomon tample ipo? Inamaana madini yote yale bado yapo!. Wejamaa, pamebaki ramani foundation pekee na sivi ginevyo. Leta picha tuone kwa ushahidi.
 
Kuna watu humu wanakera sana kupenda kutoa mijadala ya uzi kwa kulita hoja tofauti.hapa tunazungumzia mfumo wa ulinzi wa kijeshi jitu linaleta mambo ya kiimani
Ukisha itaja Israel tambua imani ni lazima itahusika.
 
S 400
S ni herufi ya 23 katika muundo wa alfabeti,Hii inamaana ya kuwa S 400,inaweza kufanya kazi tofauti 23 kwa wakati mmoja.
400 ni umbali ambao makombora yote yenye ukubwa kuanzia mpira wa gofu yanaweza kutunguliwa.Zaidi ya hilo,kuna umbali wa ziada wa km 250,katika umbali huu makombola ya adui hufanyiwa jamming,kuhakiwa au kuvurugwa mifimo yake bila kufunguliwa,sasa kombola likikoswa ndani ya kilomita hizo 250 za kwanza,ndo huja kutunguliwa ndani ya km 400 hizo nyingine.Kwa maana hii S 400 hufanya kazi ndani ya KM 650.Ndio maana S 400 ilipofungwa Siria kipindi flani,ilitengeneza "NO FLY ZONE" katika nchi tano zilizipo karibu na Siria ukijumlisha na Israel ( Hakuna kitu chochote ambacho kiliweza kuruka katika nchi hizo tano bila ya kufumuliwa)
Hii Iron Dome,inaonekana ni bora kwa sababu Israel inapigana na HAMAS( Kikundi kidogo tu) lakini kwenye vita kamili au vita na mataifa ya kibabe, Iron Dome haiwezi kuwa na ufanisi wa kutisha.
Nani kakudanganya
 
Iron dome ufanisi wake ni kwa roketi za masafa mafupi.

Mwaka 2006 vita baina ya Hizbullah na Israel takribani roketi 4000 za masafa mafupi yalirushwa na Hizbullah na kuleta madhara makubwa Israel.

Mwaka 2000 na 2008 zaidi ya 4000 mortars na roketi 4000 zilirushwa kutokea Gaza kuelekea Israel ndiyo ikapelekea kuundwa Iron Dome ambayo range yake ni 70km.

Huwezi ukapima ufanisi wake kwa vikombora dhaifu vinavyorushwa na HAMAS. Ufanisi wake utapimwa kwenye vita kamili.

Kwa ufupi Iron Dome ni kwa ajili ya wanamgambo wa HAMAS na Hizbullah.

S-400 ni ya masafa marefu. Ina locate tageti kwa umbali wa km 600 na ikaiharibu kwa umbali wa km 400.

S-400 inapambana na tageti 72 kwa wakati mmoja na kutrack tageti 160 kwa wakati huo huo.

Inashambulia aina zote za aerial target ikijumuisha aircraft, ballistic na cruise missile kwa range ya km 400...... Nitaishia hapa!

Kwa ufupi S-400 ni kwa ajili ya silaha za kisasa tishio.

Ijapokuwa kazi zake ni tofauti ila S-400 ni bora zaidi ya Iron Dome.
Hiyo S 400 iliwahi kushambulia wapi na tukaona huo ufanisi wake.

Iron Dome inafanya kazi kila siku na tunaona.
 
we dada unaongea uongo mwingi mpk unaboa.
hiz stori za kimbea kakumezesha nani?
hukusoma???. Siku ukijua utakuwa umechelewa sana dogo.
Huu ni ufunguo wa taarifa..nishukuru nimekupa hii akili bure....
Ndo mlivo division zero!!
 
Kwa sasa hivi duniani hakuna Defensive system hatari kama hii S 400 ukiacha S- 500 ambayo haijawa released bado ...
 
Iron Dome ni bora sana mkuu, yaani HAMAS wamerusha zaidi ya kombora 1,500 lakini zote zimekuwa intercepted na Iron Dome,kilichoangukia Israel ni mabaki ya Rockets za HAMAS lakini si makombora yao
Iron dome ni outdated in-terms of range na efficient ni kama S-300 hiyo S-400 ni habari nyingine chief
 
Hiyo S 400 iliwahi kushambulia wapi na tukaona huo ufanisi wake.

Iron Dome inafanya kazi kila siku na tunaona.
Iron Dome imefanya kazi kwny vita ipi? Kudungua vikombora vya Hamas vilivyoundwa kienyeji nacho ni kipimo cha kulinganisha na S400?
 
Iron Dome imefanya kazi kwny vita ipi? Kudungua vikombora vya Hamas vilivyoundwa kienyeji nacho ni kipimo cha kulinganisha na S400?
Hamas wana makombora yao yale ukiyafyatua unaweza kuya-trace hewani kama zile fataki za sherehe. Mengi ya makombora yao yanatengenezwa gereji hayana hata guidance
 
Kwa sasa hivi duniani hakuna Defensive system hatari kama hii S 400 ukiacha S- 500 ambayo haijawa released bado ...
nakubaliana na wewe mkuu

S-400 hi nikiboko sio mchezo ukiona zinavyotema zil kombola,,Na ndio mfumo bola nazani na very expensive
 
Iron Dome na S-400 zote ni Air Defence Systems lakini zina malengo tofauti kabisa.


Iron Dome inazuia makombora madogo madogo, na imekuwa designed specifically kwa ajili ya kuwadhibiti Hamas na Hezbollah.

S-400 ni Air Defence System kazi kubwa ni kuzuia ndege za adui.

Iron Dome imeshajaribiwa mara nyingi, na ime-prove kupiga kazi kweli kweli. S-400 inaogopwa kwa sababu ya ufundi walionao Warusi kwenye hizi systems, fight jet yoyote ya 4th Generation kurudi nyuma kinadharia haiwezi kupenya. S-75 iliwatesa USA wakati wa Vietnam war; zimepita version kama 2 mpaka kufika kwenye S-400. Unaweza pata picha S-400 itakuwa advanced kiasi gani.
 
Mimi nadhani swala la ulinzi na usalama wa nchi ni swala siri ya vyombo husika kwa nchi husika.
Sio rahisi kwa nchi kuweka wazi kila kitu kuhusu security details zake. Hivyo naamini tunachoelezwa kuhusu ufanisi wa hizi teknolojia za kiusalama za nchi fulani ni sehem ndogo sana ya uhalisia wa teknolojia yenyewe, na pia inakua disclosed kwa kiwango ambacho hakitaathiri usalama wa nchi.
Hivyo kwa mtazamo wangu ni vigumu sana kuweza kuwa na mizania sahihi ya kupima ni security system ipi ni bora zaid ya nyingine katika mazingira kama haya.
Sasa mkidiscuss hiv vitu, tanzania tunaiweka wap?

Au tunaiweka kwa kufanya recruitment ya failure!

Tanzania yangu sijui naiona wap baada ya miaka hamsin
 
Back
Top Bottom