Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

Rwanda, Uganda zajitoa Bandari ya Dar

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
chenge.jpg

Na Raymond Kaminyoge,

Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.

Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.

"Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam," alisema Hanspope.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... "Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo."

Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.

Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.

Kamati ya Bajeti

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alisema katika kikao kijacho cha Bunge, kamati hiyo itaibana Serikali kuhusu mikakati inayofanywa kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.

"Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi," alisema.

Alisema vitendo vya askari wa usalama barabarani kudai rushwa pia ni miongoni mwa vikwazo pamoja na urasimu mkubwa katika utoaji wa mizigo bandarini ikilinganishwa na bandari nyingine.

"Ni lazima tujifunze kwa majirani zetu Msumbiji, upanuzi wa haraka wa Bandari ya Beira umekuwa kikwazo kwetu, kampuni nyingi zimeanza kuitumia bandari hiyo," alisema.

Chenge alikitaka chama hicho kuiandikia kamati hiyo mapendekezo yake ikiwa ni hatua ya kunusuru uchumi wa nchi ili waweze kuijadili bungeni.

Umoja wa nchi tatu

Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na mwenyeji wao Yoweri Museveni walikutana mjini Kampala, Uganda na kuamua kuitumia Bandari ya Mombasa kwa shughuli zao.

Waliahidi kuimarisha ufanisi katika huduma za Bandari ya Mombasa ili kuhakikisha bidhaa zinafika mapema Uganda na Rwanda.

Pia walikubaliana kujenga reli mpya ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Mombasa kwenda Kenya na Uganda.

Viongozi hao walikubaliana pia kushirikiana katika sekta ya nishati hasa ikizingatiwa kuwa Uganda imegundua mafuta.

Nchi hizo tatu ambazo zimeruhusu kwa raia wao kusafiri kwa vitambulisho pale wanapotembelea nchi tatu miongoni mwao, zitakutana tena Kenya mwezi huu.
 
Sasa kama mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ni Andrew Chenge unategemea watu wako serious kweli na serikali hii?
Yaani ktk watu wote mzee wa vijisent ndio amepewa uenyekiti?
Kazi tunayo
 
Yaani sasa tutaitegemea zaidi Zambia labda na Burundi tu katika kuitumia bandari ya Dar es Salaam.
Malawi nao huitumia bandari hiyo lakini nadhani itafifia sana.
 
serikali dhaifu itatusaidia vipi katika hili labda mh Mwakyembe na sitta kigeugeu tusaidie jaman uchumi wetu itadidimia.
 
Kwani bandari ya tz inawafaidisha watanzania wangapi? Pia mizigo ya rwanda inayopitia tz ni ya bilioni ngapi? Bandari ya tz kitambo inaliwa na mafisadi. Kwa hyo kama walishndwa kuisimamia mpaka watu wakachoka watulie waangalie sekta zingine. Serikali itapata fundisho na itakua serious kusimamia masuala ya mapato. Watajiju mafisadi wanaofaidi bandarini.
 
Hao wasafirishaji kwa nini hawaleti mchanganuo wa kitakwimu....

1. Inachukua siku ngapi kuondosha kontena bandarini (Dsm/Mombasa)
2. Gharama za uondoshaji huo zikoje?
3. Unatumia siku ngapi kusafirisha kontena kwenda Uganda ama Rwanda?
4. Kero za traffic police kwa Tanzania na Kenya zikoje?

Kubwa zaidi hao kina Hanspope watwambie tukiondoa mizani wanatuhakikishiaje kuwa hawatabeba mizigo zaidi ya uzito unaoruhusiwa???

Bila kufanya haya tutakuwa tunapiga siasa tu!!

Kikubwa serikali yetu iongeze ufanisi tu bandarini, barabara ziimarishwe, tufufue reli ya kati jambo ambalo kina Hanspope hawato-support....mwisho wa siku wafanya biashara wa Rwanda na Uganda wataangalia njia ipi inawapa faida!!!!
 
I said it somewhere else,
Before you embark on a journey of revenge, dig two graves.

Mara zote kwenye ugomvi huwa hakuna mshindi kamili..huu mkorogano unaoendelea ni lazima utugharimu na sisi.

Everything has a price. Rwanda and Tanzania are losers! Kenya is the most winner. Uganda - neutral!
 
Hao wasafirishaji kwa nini hawaleti mchanganuo wa kitakwimu....

1. Inachukua siku ngapi kuondosha kontena bandarini (Dsm/Mombasa)
2. Gharama za uondoshaji huo zikoje?
3. Unatumia siku ngapi kusafirisha kontena kwenda Uganda ama Rwanda?
4. Kero za traffic police kwa Tanzania na Kenya zikoje?

Kubwa zaidi hao kina Hanspope watwambie tukiondoa mizani wanatuhakikishiaje kuwa hawatabeba mizigo zaidi ya uzito unaoruhusiwa???

Bila kufanya haya tutakuwa tunapiga siasa tu!!

Kikubwa serikali yetu iongeze ufanisi tu bandarini, barabara ziimarishwe, tufufue reli ya kati jambo ambalo kina Hanspope hawato-support....mwisho wa siku wafanya biashara wa Rwanda na Uganda wataangalia njia ipi inawapa faida!!!!

Naunga mkono hoja
 
Yaani sasa tutaitegemea zaidi Zambia labda na Burundi tu katika kuitumia bandari ya Dar es Salaam.
Malawi nao kuitumia bandari hiyo lakini nadhani itafifia sana.
Kwa hakika miaka ya Malawi kuitumia bandari ya Dar es Salaam inahesabika. Wana mipango ya kupitisha bidhaa zao Msumbiji zaidi na zaidi. Kuna mradi aliuanzisha Rais wao Marehemu Bingu Mutharika wa kujiunganisha na bahari ya Hindi (Pwani ya Msumbiji) kwa kutaumia mto Shire. Bandari ya Nsanje kwenye mto huo (ndani ya Malawi ) ilianza kujengwa - japo ujenzi umesimama baada ya Bingu kufariki. Kuna msukumo mkubwa wa kuurudia na kuukamilisha mradi huu, hasa sasa baada ya uhusiano unaosuasua na Tanzania.
 
Wewe si ndio ulikuwa ukishabikia conflict ya rwanda na Tz,haukuangalia kitakachofuata mbele ilhali uganda na rwanda ni kitu kimoja.
Also tuitangaze bandari yetu kwa kupunguza gharama kama fast jet uone competition.

Yaani sasa tutaitegemea zaidi Zambia labda na Burundi tu katika kuitumia bandari ya Dar es Salaam.
Malawi nao huitumia bandari hiyo lakini nadhani itafifia sana.
 
let them Go nothing to worry! kuendelea kulialia na RWANDA&UGANDA kutumia bandari yetu au lah kwetu ni changamoto lakini pia tujue kua ni muda mrefu hawakupenda kufanya hivyo ila kwa sasa ndo wamejidhiirisha roho zao zikoje! Tumshukuru Mungu kwakua na bahari cha msingi apa ndo iwe chachu ya kusimamia na kuanzisha vyanzo vya mapato vingine..leo tunalaumiana lakini tujiulize je nchi ambazo hazina BAHARI chumi zao zinaendeshwaje? Tuwekeje kwenye GAS na italipa tu acha watuondolee Jams na usumbufu
 
Back
Top Bottom