Danny Jully
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 4,416
- 3,860
Mkuu Pasco hizo shughuli za maana ambazo ili zifanyike ni lazima ruzuku ifutwe ni zipi? Na kama ni za maana kweli kuliko hiyo ruzuku ya vyama kwa nini zisipangiwe bajeti yake? Tumekuwa na huu mtazamo sana kwamba kwa nini pesa fulani isiende kufanya mambo ya maana. Hata ndege zilizonunuliwa tulidai pesa zake zingeenda kufanya hayo maana kwani ni watz wangapi wana uwezo wa kutumia huo usafiri? Kupanga ni kuchagua mkuu, tumekubali ruzuku iwepo tena kisheria. Nani kakuambia hii nchi ni maskini? Hivyo vijisenti tu vya ruzuku ndio vinakusumbua?Mkuu Kilimba, ni kweli ruzuku ni haki ya vyama vya siasa, lakini hata mikutano pia ni haki ya vyama vya siasa, baada ya kuonekana mikutano haina maslahi kwa taifa, imefutwa, why not ruzuku? .
Jee kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa ni jambo jema kuliko hizo fedha zingetumika kwenye shughuli nyingine za maana zaidi.
Pasco