Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,
Kuna hii kauli ya "asiyefanya kazi na asile". Jee siasa nayo ni kazi ya kustahili mshahara kwa jina la ruzuku kwa vyama vya siasa? . Ruzuku hii iendelee kuwepo watu waendelee kuitafuna au ifutwe? .

Japo sijafanya utafiti wa ni nchi ngapi zinagawa ruzuku kwa vyama vya siasa lakini kwa nchi masikini kama Tanzania , serikali inayowajibika kwa watu wake na kuheshimu rasilimali kiduchu za taifa, haiwezi fedha zinazokamuliwa kama kodi kwa wananchi masikini wa kutupwa wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu fedha hizo zinakuja kugawiwa bure kama ruzuku kwa watu wazima wenye nguvu zao! .

Je Huu sio ufisadi? .

Katika kuunga mkono juhudi za rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli za kubana matumizi ikiwemo kupunguza safari za nje, kuwaengua watumishi hewa, kufanya tumbua tumbua majipu ya ufisadi, namshauri rais wetu azifutilie mbali ruzuku za vyama vya siasa, huu ni ufisadi tuu kama ulivyo ufisadi mwingine wowote! .

Enzi za Nyerere kulitolewa ruzuku ya mbolea, mbegu bora na pembejeo za kilimo ili kuimarisha uzalishaji mali, sasa ruzuku hizo zimefutwa na badala yake mijitu mizima isiyo na matatizo yoyote, ndio inakaa bure kutafuna ruzuku ya bure bure huku masikini wakitaabika.

Asiyefanya kazi na asile! . Siasa sio kazi ya mshahara bali ni kazi ya kujitolea, ruzuku kwa vyama vya siasa ni ufisadi, jee is it just au ifutwe?.

Angalizo.
Japo ruzuku ni haki ya vyama vya siasa na inatolewa kwa mujibu wa katiba, lakini kiukweli ruzuku ni ufisadi tuu kama ulivyo ufisadi mwingine wowote na japo rais hana mamlaka ya kufuta jambo lolote lililoruhusiwa na katiba, lakini kwenye vita vya ufisadi akiamua anaweza.

Hata mikutano ya hadhara ya kisiasa popote uliruhusiwa na katiba lakini kufuatia ufisadi wa matumizi mabaya ya muda, badala ya vyama kuhamasisha watu wafanye kazi, vyama vinakalia kuhamasisha uzururaji kwa jina la maandamano na uvivu wa watu kukaa bure bila kufanya kazi kwa kisingizio cha kuhudhuria mikutano ya hadhara ya kisiasa nchi nzima. Rais Magufuli amepiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa popote na amefanikiwa.

Mishahara ni haki ya mwajiriwa, wakati wangine wakilipwa mishahara ya Shilingi 150,000 kwa mwezi, wengine wanalipwa shilingi milioni 40 kwa mwezi. Hiyo ni mishahara ya peponi. Rais Magufuli amebaini kuwa huo pia ni ufisadi hivyo ameamuru mishahara hiyo ikatwe na kima cha juu kubaki sii zaidi ya TZS 15.M.

Sasa kama haya yote rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli ameweza, anawezaje kuachia huu ufisadi mkubwa kabisa kwa jina la ruzuku uendelee kufanywa na serikali yake kwa kuwakamua kodi watu masikini wa nchi yake na kuwagawia bure bure watu matajiri kuitafuna? !.

Hakuna hata kuzisubiri Bunge kuifuta sheria ya ruzuku kwa vyama vya siasa, rais Magufulli kwavile ameamua kapambana na ufisadi na kubana matumizi, na ameweza, amefuta mikutano na maandanamano na ameweza, then apambane na ufisadi wote bila double standards na kubana matumizi yote yasiyo ya lazima zikiwemo kufuta ruzuku kwa vyama vya siasa, hata ikibidi kubakiwa na chama kimoja tuu CCM kitawale milele, sisi tuko tayari CCM itawale milele katika Tanzania isiyo na ufisadi.

Paskali

Rejea
Ruzuku kwa vyama vya siasa iondolewe Tanzania!

Ushauri : Ruzuku za vyama vya siasa kwa mwaka 1 zipelekwe kusaidia maafa Bukoba
Rais apitie upya ruzuku za vyama vya siasa, ni zaidi ya laana
Ruzuku kwa vyama vya siasa ifutwe
MAONI: Serikali isitishe ruzuku kwa vyama vya siasa hadi 2020
 
Waanze na CCM kwakuwa inachukua pesa nyingi sana pia imenyakua vitegauchumi vyote wakati wa chama kimoja hizi zilikuwa ni assets za serikali ccm wangeachiwa ofisi ya makao makuu tu,na vingine virudi serikali kuu. Wamekwapua na badonwanalipwa ruzuku wakati vyama vichanga havina pakushika vitanyanyukaje kama ruzuku inaishia ccm.
 
Wanabodi,
Kuna hii kauli ya "asiyefanya kazi na asile". Jee siasa nayo ni kazi ya kustahili mshahara kwa jina la ruzuku kwa vyama vya siasa? . Ruzuku hii iendelee kuwepo watu waendelee kuitafuna au ifutwe? .

Japo sijafanya utafiti wa ni nchi ngapi zinagawa ruzuku kwa vyama vya siasa lakini kwa nchi masikini kama Tanzania , serikali inayowajibika kwa watu wake na kuheshimu rasilimali kiduchu za taifa, haiwezi fedha zinazokamuliwa kama kodi kwa wananchi masikini wa kutupwa wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu fedha hizo zinakuja kugawiwa bure kama ruzuku kwa watu wazima wenye nguvu zao! .

Je Huu sio ufisadi? .

Katika kuunga mkono juhudi za rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli za kubana matumizi ikiwemo kupunguza safari za nje, kuwaengua watumishi hewa, kufanya tumbua tumbua majipu ya ufisadi, namshauri rais wetu azifutilie mbali ruzuku za vyama vya siasa, huu ni ufisadi tuu kama ulivyo ufisadi mwingine wowote! .

Enzi za Nyerere kulitolewa ruzuku ya mbolea, mbegu bora na pembejeo za kilimo ili kuimarisha uzalishaji mali, sasa ruzuku hizo zimefutwa na badala yake mijitu mizima isiyo na matatizo yoyote, ndio inakaa bure kutafuna ruzuku ya bure bure huku masikini wakitaabika.

Aliyefanya kazi na asile! . Siasa sio kazi ya mshahara bali ni kazi ya kujitolea, ruzuku kwa vyama vya siasa ni ufisadi, jee is it just au ifutwe? .

Pasco

Rejea
Ushauri : Ruzuku za vyama vya siasa kwa mwaka 1 zipelekwe kusaidia maafa Bukoba
Rais apitie upya ruzuku za vyama vya siasa, ni zaidi ya laana
Ruzuku kwa vyama vya siasa ifutwe
MAONI: Serikali isitishe ruzuku kwa vyama vya siasa hadi 2020
Sasa kama ni hivyo tuanze na kurudisha viwanja vya umma kutoka CCM pia majengo ya umma ambayo yalijengwa na umma yamekuwa mali ya CCM, afu tuje na mkaguzi akague mali za CCM ni kwenye ulipaji kodi likiwemo jengo la CCM hapo lumumba na mengine yote
 
Itakavyokuwa hivyo nadhani nafasi za uenyeviti wa vyama zitakuwa wazi kuanzia siku ya kwanza ya kufutwa kwa ruzuku hiyo.

Nafasi hiyo hairuhusiwi kugombewa na mtu mwingine kwenye baadhi ya vyama kwa sababu ya ruzuku tu.

Hawana uchungu na vyama vyao, wanachama ama wananchi.
Mkuu Hochimini, naunga mkono hoja, ila pia bado najiuliza kwenye needs na priorities, hiyo ruzuku kwa vyama vya siasa is it all that needs na ni muhimu kilivyo kuliko hata ruzuku ya mbolea na pembejeo za kilimo? .
Pasco
 
Kwanza ikifutwa itatupunguzia migogoro kwenye vyama watabaki wazalendo tu

HABARI SIJUI HUYU KAFUNGUA ACCOUNT MPYA wakati ya awali bado ipo MARA YULE KAOMBA KUONGEZEWA POSHO HADI M11 HAZITAKUWEPO
Mkuu Kwiu, siasa ni kazi ya kujitolea, haiwezekani watu wajitolee tuu halafu serikali yetu iwalipe pesa za umma wajitafunie. Huku ni kuigeuza siasa kuwa ni ajira.
Pasco
 
Hili ni suala la kisheria may be muanzie kulishauri bunge libadilishe sheria
Mkuu Mambaku, kweli hili ni suala la kisheria ila kwenye vita vya ufisadi, sheria weka pembeni!, hata mikutano ya hadhara ya kisiasa pia ni jambo la kisheria lakini imefutwa! . Magufuli akaamua, anaweza! , kwani sheria ndio nini na zimewekwa na nani? ,kama katiba tuu tunaibadilisha, itakuwa sheria? !.
Pasco
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom