Ruzuku kwa vyama vya Siasa: Mnaonaje tumshauri Rais Magufuli aifutilie mbali ruzuku hii? Ni ufisadi

Wanabodi,
Kuna hii kauli ya "asiyefanya kazi na asile". Jee siasa nayo ni kazi ya kustahili mshahara kwa jina la ruzuku kwa vyama vya siasa? . Ruzuku hii iendelee kuwepo watu waendelee kuitafuna au ifutwe? .

Japo sijafanya utafiti wa ni nchi ngapi zinagawa ruzuku kwa vyama vya siasa lakini kwa nchi masikini kama Tanzania , serikali inayowajibika kwa watu wake na kuheshimu rasilimali kiduchu za taifa, haiwezi fedha zinazokamuliwa kama kodi kwa wananchi masikini wa kutupwa wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu fedha hizo zinakuja kugawiwa bure kama ruzuku kwa watu wazima wenye nguvu zao! .

Je Huu sio ufisadi? .

Katika kuunga mkono juhudi za rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli za kubana matumizi ikiwemo kupunguza safari za nje, kuwaengua watumishi hewa, kufanya tumbua tumbua majipu ya ufisadi, namshauri rais wetu azifutilie mbali ruzuku za vyama vya siasa, huu ni ufisadi tuu kama ulivyo ufisadi mwingine wowote! .

Enzi za Nyerere kulitolewa ruzuku ya mbolea, mbegu bora na pembejeo za kilimo ili kuimarisha uzalishaji mali, sasa ruzuku hizo zimefutwa na badala yake mijitu mizima isiyo na matatizo yoyote, ndio inakaa bure kutafuna ruzuku ya bure bure huku masikini wakitaabika.

Aliyefanya kazi na asile! . Siasa sio kazi ya mshahara bali ni kazi ya kujitolea, ruzuku kwa vyama vya siasa ni ufisadi, jee is it just au ifutwe?.

Angalizo.
Japo ruzuku ni haki ya vyama vya siasa na inatolewa kwa mujibu wa katiba, lakini kiukweli ruzuku ni ufisadi tuu kama ulivyo ufisadi mwingine wowote na japo rais hana mamlaka ya kufuta jambo lolote lililoruhusiwa na katiba, lakini kwenye vita vya ufisadi akiamua anaweza.

Hata mikutano ya hadhara ya kisiasa popote uliruhusiwa na katiba lakini kufuatia ufisadi wa matumizi mabaya ya muda, badala ya vyama kuhamasisha watu wafanye kazi, vyama vinakalia kuhamasisha uzururaji kwa jina la maandamano na uvivu wa watu kukaa bure bila kufanya kazi kwa kisingizio cha kuhudhuria mikutano ya hadhara ya kisiasa nchi nzima. Rais Magufuli amepiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa popote na amefanikiwa.

Mishahara ni haki ya mwajiriwa, wakati wangine wakilipwa mishahara ya Shilingi 150,000 kwa mwezi, wengine wanalipwa shilingi milioni 40 kwa mwezi. Hiyo ni mishahara ya peponi. Rais Magufuli amebaini kuwa huo pia ni ufisadi hivyo ameamuru mishahara hiyo ikatwe na kima cha juu kubaki sii zaidi ya TZS 15.M.

Sasa kama haya yote rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli ameweza, anawezaje kuachia huu ufisadi mkubwa kabisa kwa jina la ruzuku uendelee kufanywa na serikali yake kwa kuwakamua kodi watu masikini wa nchi yake na kuwagawia bure bure watu matajiri kuitafuna? !.

Hakuna hata kuzisubiri Bunge kuifuta sheria ya ruzuku kwa vyama vya siasa, rais Magufulli kwavile ameamua kapambana na ufisadi na kubana matumizi, then apambane na ufisadi wote bila double standards na kubana matumizi yote yasiyo ya lazima zikiwemo ruzuku kwa vyama vya siasa.

Pasco

Rejea
Ushauri : Ruzuku za vyama vya siasa kwa mwaka 1 zipelekwe kusaidia maafa Bukoba
Rais apitie upya ruzuku za vyama vya siasa, ni zaidi ya laana
Ruzuku kwa vyama vya siasa ifutwe
MAONI: Serikali isitishe ruzuku kwa vyama vya siasa hadi 2020
Ni mawazo mazuri sana Pasco. Ni busara Vyama vya Upinzani vifutiwe Ruzuku na ibaki kwa Chama Tawala tu ili haki itendeke maana hivyo Vyama havina la maana zaidi ya maandamano tu!!
 
Naunga mkono kabisa, hata hizo mali za umma zinazosadikika ziko ccm zirudishwe serikalini kisha anayetaka uongozi wa kisiasa ajitolee tu.maana yaweza kuwa kazi ya wito pia.
 
Baada ya kufutwa hutasikia tena vyama vingi Tanzania.
Mkuu Shemtibu, tulivyo anzisha vyama vingi lengo lilikuwa ni kupata vyama viwili au vitatu strong kuleta strong opposition na sio huu utitiri wa vyama! .
Ruzuku ikifutwa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nayo ifungwe tuu, namuona kama Jaji Mutungi hana lolote la maana la kufanya, apangiwe kazi nyingine.
Pasco
 
Wazo zuri naunga mkono hoja.
Ruzuku ipelekwe kununua pembejeo ili iwasaidie wakulima.
Mkuu Kitulo, naunga mkono hoja.
Fedha za ruzuku zikafanyiwe shughuli nyingine yoyote ya maana zaidi kuliko kuwapa watu wazima na nguvu zao na viungo vyao kamili, bora hata wazigawe kuwatunza wazee, wenye ulemavu, wasiojiweza na watoto yatima.
Pasco
 
Vipi magari ya vx na v8 unaonaje vyenyewe havina shida kwenye kubana matumizi alafu ujue ccm mgawo wao utakupo palepale
Mkuu Ongata, VX na V8 pia ni tatizo ila kwa barabara zetu magari hayo yanahitajika tena tulihitaji Landrover 110 ila amini usiamini bei ya Landrover 110 ni juu kuliko VX! .

Ruzuku ikifutwa CCM bado utabaki imara kutokana kumiliki vitega uchumi vya kutosha ilivyo loot kutoka kwa Watanzania.
Pasco
 
Anzisha mchakato wa kisheria,kama kwenda mahakamani kuiomba mahakama ifute sheria ya ruzuku,vyama vya siasa vijitegemee mbona vyama vya michezo,vyama vya ushirika havipati ruzuku kutoka serikalini na vimeweza kuendesha shughuli zao.
Hayo mamilioni ya ruzuku wanaopewa vyama vya siasa zipelekwe kuwasaidia wakulima,wafugaji,wavuvi,wafanyabiashara wadogo wadogo nk.
 
Waanze na CCM kwakuwa inachukua pesa nyingi sana pia imenyakua vitegauchumi vyote wakati wa chama kimoja hizi zilikuwa ni assets za serikali ccm wangeachiwa ofisi ya makao makuu tu,na vingine virudi serikali kuu. Wamekwapua na badonwanalipwa ruzuku wakati vyama vichanga havina pakushika vitanyanyukaje kama ruzuku inaishia ccm.
Mkuu Kaka Kiiza, kwa hili la CCM ku loot mali za Watanzania, tusimlaumu CCM kwa sababu hata Mungu alisema "Mwenye nacho, ataongezewa, na asiye nacho atanyanganywa hata kidogo alichonacho "

Ruzuku ikifutwa vyama vidogo vitakufa na kubaki vyama vikubwa tuu hivyo kuondoa utitiri wa vyama na kupata strong opposition.
Pasco
 
Mara zote nimekuwa nikivutiwa sana na hoja zako mkuu Pasco hasa kutoka na na kiwango kikubwa cha uchambuzi makini na neutrality of arguments. Lakini katika mada yako ya leo nadhani "umeteleza" mkuu. Ni kama naona kivuli tu cha Pasco lakini si Pasco mwenyewe halisi.

Kama unakubali kuwa ruzuku ipo kikatiba inakuwaje unataka tumshauri rais avunje sheria na katiba ya nchi? Rais akiwa mvunja sheria na katiba nini yatakuwa madhara yake katika nchi hii? Umesema vema kwamba kuna mambo mengine ambayo yapo kisheria (na kikatiba pia) ambayo rais "ameyapiga chini". Sawa, lakini nadhani anspofanya hayo tumwache afanye yeye kwa matakwa yake mwenyewe lakini si kwa sisi kumshauri vibaya ili kama sifa au lawama zimfikie mwenyewe. Nadhani hata yeye hatahitaji ushauri wetu (anao watu wake wa kufanya hivyo) zaidi ya kutaka tumwombee!

Nisahihishwe kama nimeelewa vibaya.
 
Ruzuku ni Haki ya Vyama vya Kisiasa,Sasa Kwa Sababu Kuna Mtu Mmoja Amewakera Watu,Basi Sie Wote Tuathirike Kwa Ujinga Wake?
Big No!
Mkuu Kilimba, ni kweli ruzuku ni haki ya vyama vya siasa, lakini hata mikutano pia ni haki ya vyama vya siasa, baada ya kuonekana mikutano haina maslahi kwa taifa, imefutwa, why not ruzuku? .
Jee kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa ni jambo jema kuliko hizo fedha zingetumika kwenye shughuli nyingine za maana zaidi.
Pasco
 
Kwasababu CCM wanatumia bajeti ya serikali kuu kujihudumia unadhani hao wapinzani watatumia nini kujiendesha?
Mkuu Bavaria, Tanu ilianzishwa kwa michango ya kujitolea.
Siasa sio ajira ni kazi ya kujitolea.
Ruzuku kwa vyama vya siasa ni ufisadi tuu kama ulivyo ufisadi mwingine wowote.
Pasco
 
Watu wanauwana 7bu yw ruzuku..watu hawatak kutoka kwenye uwenyekiti ukatibu sababu ya ruzuku..mwenzie akitaka kugombania bac kifo au kumundia zengwe na kumfukuza...nmeipenda hili wazo litasaidia sana kwan hivi vita vya ndani ya chama mbona vitapungua kama sio kuisha nawaombeni watanzania sote tungane kupigia upate wazo hili lipite ....kwani yeyote atayendesha chama bac ataendesha kizalendo kabisa maana hata sh.1 ya wananchi hapati....
 
Pasco, Rais aifute ruzuku kwa kutumia sheria gani!?
Mkuu Zero, kwani rais Magufuli alipofuta mikutano ya hadhara ya kisiasa aliifuta kwa sheria gani?.
Rais aliposema atapunguza mishahara, atapunguza kwa sheria gani? .
Au alipotaka Maalim Seif anyimwe mafao, anyimwe kwa sheria gani? .
Ruzuku ni ufisadi, rais akiamua kuifuta hiyo ruzuku anaifuta tuu kwa sababu ni ufisadi tuu kama ulivyo ufisadi mwingine wowote.
Pasco
 
Back
Top Bottom