Ruzuku kwa mwezi: CCM milioni 800/-, Chadema 200/-, CUF 117/-

Tofauti na tunavyoona hali ya mambo ndani ya CHADEMA ambacho kipo busy na shughuli za kisiasa nchini kwa kutumia vijipesa kidogo vya ruzuku na michango ya wananchi; chama cha mapinduzi chenye matrioni ya ruzuku kila mwaka hakijulikani kinazitumiaje hizo fedha.

Wadadisi wa mambo wanahoji, kama CHADEMA pamoja na uchanga wake, na karuzuku kadogo inakopata inaweza kufanya mambo mengi na makubwa kiasi hiki yanayoashiria ushiriki wa kweli katika shughuli za siasa, CCM yenye matrioni ya fedha si ilipaswa kufanya zaidi ya hapo?

CCM inatumia ofisi zilizojengwa na watanzania wote nchi nzima, hakilipi kodi ya pango la ofisi; CCM inakusanywa hela kutoka kwenye miradi iliyochangiwa na watanzania wote wakati wa chama kimoja: kama vile viwanja vya mipira, majengo ya kukodisha, pamoja na viwanda, na hivi sasa inajineemesha kutokana na kipato kitokanacho na miradi hiyo.

Kwa haraka haraka kama ukifanya tathimini ya kile ambacho CCM inauwezo wa kukusanya kwa mwaka na matumizi yake, matrioni ya fedha yanabaki mfukoni. Lakini chama hiki hakijishughulishi na jambo lolote linalohusu affairs za watu.

Hakijishughulishi kwenda kusikiliza kero za wananchi na kutoa maelezo juu ya masuala ambayo kiliahidi kutekeleza mwaka 2010 na hakikutekeleza. Hakijishughulishi na ukusanyaji wa maoni ya katiba (taarifa za ndani zinaonyesha kwamba kuna kikosi kazi kinatengeneza hayo maoni, badala ya kuyakusanywa kwa wananchi kama inavyofanya CHADEMA), na zaidi ya yote, chama hiki hakionyeshi kuguswa na matatizo yanayowakabili wananchi hata japo kwa kujaribu kuwa nao na kushirikiana nao kuyatatua.

Mimi najiuliza hapa, hizi ruzuku kubwa ambayo chama hiki kinaipata, inatumika wapi, na inatumikaje? Na pesa zile zinazokusanywa kwenye miradi mbalimbali ambayo ilijengwa na watanzania wote inatumika wapi?

Tunataka majibu yanayojitosheleza siyo longolongo. Kuna taarifa za ndani zinazoonyesha kwamba ruzuku ya chama chenu inawaneemesha baadhi ya vigogo ndani ya chama. Kama mtaleta hadidhi za sungura na paka mimi nitamwaga mboga hapa. Tayari nina data za matawi yenu ambayo yameripoti kutokupata hela yoyote kutoka makao makuu huku kila tawi likipangiwa kiasi cha fedha cha kuchangia makao makuu. Mtueleze ni kwanini huko makao makuu kunahitaji kuongezewa hela tu ilihali hakuna cha maana kinachoendelea katika harakati za kisiasa?

cc. HAMY-D, Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, Ritz, ZeMarcopolo, babayako utaifakwanza, FaizaFoxy, etc.
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahaaaa!!
Budget ya CCM ni kubwa kuliko budget ya nchi. Lakini wanachofanya ni kuua tembo wetu tu.

Mkuu usitegemee jibu kwa hao onyenye hapo juu.
Ni shida na njaa tu zinawasumbua hao
 
Mkuu zinatumika kwa kuwalipa wanaopika maoni juu ya katiba mpya pale lumumba, pia zinaliwa na wachumia tumbo kama mwigulu nchemba, nape nnauye na vile vizee pale lumumba, pia usisahau zingine hutumika kuwahonga mabolizi wa nyumba kumikumi wakati wa uchaguzi!
 
*Kukodisha magari ya kusomba watu kwenye mikutano ili paonekane pamejaa na kuwalipa wanaohudhuria maana wanasombwa bila hiari yao.

*Kutengeneza kura feki wakati wa uchaguzi
 
CCM inatumia gharama kubwa na ya kutisha kila wanapoitisha mkutano mmoja wa hadhara. Kwani kikao kimoja cha CCM gharama yake ni sawa na vikao 30 vya CDM kwani kila mhudhuliaji upewa posho na usafiri na wengi wao husombwa Wilaya jirani na hata mikoa jirani, wasanii pia hulipwa na ukiweka na posho za vbopa utakuta tilioni kadhaa zimetumika.
 
Mkuu Lukolo

Vijana Wa Lumumba Wapo Kwenye Mgomo Baridi, Wanadai Nyongeza Ya Posho Za Post & Thread!

Wanadai Posho Wanayopewa Ni Ndogo Kulinganisha Na Kazi Wanayofanyishwa Ya Kuipinga CHAMA KUBWA CHADEMA..
Ndo Maana Hawapo Jamvini...
 
ccm wanatumia ruzuku kwa: KUWALIPA WALE LB7 PROJECT,ULIPIA MALORI YA KUSOMBA WATU KTK MIKUTANO,KUNUNUA SHAHADA,KUTENGENEZA KOFIA NA TSHIRT WAKATI WA KAMPENI,KUWANUNUA BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI MAKANJANJA,KTENGENEZA VIDEO FAKE,KUGAWA 500,1000,CHUMVI NA SUKARI WAKATI WA CHAGUZI,KUWANUNUA MASHEHE NA WACHUNGAJI UCHWARA WAWAPIGIE DEBE NA.......
 
Unlike other parties, CCM ina ofisi kila mkoa, kila wilaya, kila kata, kila kijiji. Ofisi zote hizi zina makatibu wa chama na wa jumuiya. Shughuli za ofisi hizi zinaendeshwa na ruzuku pamoja na michango ya wanachama.
 
Kijana ishia hapohapo , vinginevyo utakutwa MABWEPANDE ! swali hilo alitakiwa apelekewe MZEE PIUS MSEKWA na wala siyo hao uliowapelekea nakala , ni swali gumu sana .
 
eti vijipesa kidogo vya ruzuku na michango ya wanachama, eti ndio zinatumika kwenye shughuli za kisiasa chadema.

unamdanganya nani?

tangia mwaka 2010 baada ya uchaguzi mkuu hadi leo, chadema imeharibu mabilioni ya pesa.
ambazo kama wangeamua kujenga ofisi labda ubungo plaza kama 13 hivi nchi nzima.
wakati chadema inahoji juu ya ruzuku ya ccm, wao mpaka sasa hawajajibu haya mabilioni ya pesa wanayatoa wapi?
na kwa makubaliano gani?
 
Back
Top Bottom