Ruvuma: Christopha Njako, Tajiri wa mahindi akamatwa kwa utakatishaji fedha

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,803
12,667
Bilionea wa mahindi mkako atiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani

November 13, 2020

Na Stephano Mango, TimesMajira Online, Songea

JESHI la Polisi Mkoani Ruvuma limemkamata Mfanyabiashara wa mazao ya mahindi Christopha Njako (30) maarufu kwa jina la ‘bilionea wa Mkako’ Mkazi wa kijiji cha Mkako Wilayani Mbinga na kumfikisha mahakamani kwa makosa matatu ikiwemo kijipatia zaidi ya Sh. bilioni 1.3 kwa udanganyifu

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma ACP Simon Maigwa amesema, mfanyabiashara huyo amekamatwa jana na amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma kujibu mashtaka matatu yanayomkabili.

Inadaiwa kuwa, kuanzia Agosti mwaka huu mfanyabiashara huyo amekuwa akinunua mahindi kwa bei ya juu ya shilingi 75,000 kwa gunia moja na kuyauza kwa bei ya chini shilingi 45000 kitendo kilichowavutia wakulima wengi pamoja na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Mikoa mbalimbali hapa nchini ambao walifika katika kijiji cha Mkako kwa lengo la kuyauza mahindi yao na wengine kuyanunua mahindi na kuyapeleka kuyauza Mikoa ya Kaskazini na nje ya Nchi.

Ameeleza kuwa, ilipofika mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu, biashara hiyo ilianza kuleta dosari, mashaka na taharuki kubwa kwa wakulima na wafanyabiashara waliokuwa wamepeleka mahindi yao kuyauza kwa mfanyabishara Njako na ndipo malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara na wakulima ambao walimlalamikia Njako kushindwa kuwalipa fedha walizo peleka kuyauza mahindi yao na wengine walilalamika kuwa walimpatia fedha ili awapatie mahindi bila mafanikio.

Kamanda Maigwa amesema, baada ya kupokea na kubaini malalmiko hayo, Jeshi la Polisi lilichukua hatua stahiki ambazo ni pamoja na kufanya uchunguzi wa kina na kuupata ukweli kuwa mfanyabiashara huyo alikuwa akifanya biashara kwa njia ya ujanja na kuwatapeli wakulima na wafanya biashara zaidi ya 1200 ambao wanadai fedha zaidi ya shilingi bilioni 1.3.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, amekuwa akitumia fedha hizo kuanzisha miradi mingine binafsi ambapo amejenga ghala la kuhifadhia mahindi, amejenga nyumba ya kulala wageni, amejenga nyumba ya kuishi na amenunua magari ya kifahari.

Baada ya Jeshi la Polisi kujiridhisha mfanyabiashara huyo amewatapeli idadi kubwa ya wananchi na kusababisha taharuki, kwa kushirikiana na Ofisi ya Mashtaka ya Taifa ilichukuliwa hatua ya kumfikisha mahakamani mshtakiwa kwa makosa matatu na taarifa za ndani zimeonesha kuwa mfanyabiashara huyo amekuwa akifanya matendo hayo ya utapeli akishirikiana na jamaa zake wa karibu na upelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo unaendelea.

Zaidi, soma:

 
Baada ya zile tuhuma nzito za kuwatapeli wananchi.

Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma, linamshikilia Christopher Njako, maarufu kama Bilionea wa Mkako, mkazi wa Kijiji cha Mkako wilayani Mbinga mkoani humo kwa kosa la kutakatisha fedha baada ya kufanya biashara ya mahindi, akinunua mahindi hayo kwa Tsh. 70,000 kwa kila gunia na kisha kuuza kwa Tsh. 42,000 kwa kila gunia.

Chanzo: EAST AFRICA TV
 
Habari za awali nin kwamba Jamaa alinunua mahibdibkwa bei ya juu na kuuza kwa bei ya chini. Lkn Polisi na Serikali kwa ujumla walimpa ulinzi na KUHAKIKISHA vya a sisi zote za Serikali zipo pale mkako wakikusanya kodi zao na miamala inakamilika kupitia mawakala wa benki. Baada ya kuzingua Serikali ileile leo inamgeuka na kumfingulia KESI. Binafsi naona Serikali ilichelewa.

Kimsingi waliofanikiwa ni wachache kuliko waliopotoeza. Nafikiri tujifunzw yanapotokea haya Serikali kuchukua hatua HARAKA. Huenda Siasa za kampeni ziliathiri kutochukua hatua ontime
 
Habari za awali nin kwamba Jamaa alinunua mahibdibkwa bei ya juu na kuuza kwa bei ya chini. Lkn Polisi na Serikali kwa ujumla walimpa ulinzi na KUHAKIKISHA vya a sisi zote za Serikali zipo pale mkako wakikusanya kodi zao na miamala inakamilika kupitia mawakala wa benki. Baada ya kuzingua Serikali ileile leo inamgeuka na kumfingulia KESI. Binafsi naona Serikali ilichelewa.
Kimsibgi waliofanikiwa ni wachache kuliko waliopotoeza. Nafikiri tujifunzw yanapotokea haya Serikali kuchukua hatua HARAKA. Huenda Siasa za kampeni ziliathiri kutochukua hatua ontime
Kazingua Kivip?kwani kuna watu wamelizwa?
 
Kazingua Kivip?kwani kuna watu wamelizwa?
Huyu jamaa yani ni kama alikuwa anfanya biashara isiyo na faida, na kwa siku alikuwa anatoa mzigo wa maana. Ila hata yeye alikuwa hawezi kukwambia ela inatoka wapi.

Hakuna aliyekuwa anadhulumiwa kila mtu analipa na kila siku zaidi ya milion 200 inatoka.
Anakwambia anakula hasara ila bado anaendela kununua na kujenga magodown.

Kulikuwa kuna jambo ambalo halikuwa linamake sense. Ila wakulima wa mahindi wanamshukuru sana kwakweli. Yani unashusha mzigo, anamlipa dereva, analipia gari na mzigo wako anaununua bila kukukata hata cent. kama mkilala mnalala kwa gharama zake.
 
Kazingua Kivip?kwani kuna watu wamelizwa?
Wengi mno tena mzigo wa maana. Kama sikosei taaraifa ya Polisi ilisema ni zaidi ya 1.3 bilioni. Watu wanadai m.7 HD 20 huko. Ilikuwa ni Imani ambayo MTU hata uwe na madigirii unai bia mkenge.

Sokoni Mahindi 100 kg hayafiki 50,000 lkn Jamaa ananunua kwa 75,000 halafu anauza kwa 42,000 HV. So wenye mhindi wote walihamishia huko kutoka sehemu zote za Mkoa wa RUVUMA na hata Njombe pia.

Kijiji kulikuwa kama machimbo mapya ya madini, watu Kibao sana. Mwishowe watu waliamini watalipa tu wanaendelea kupeleka mzigo had wakistuka kuchelweshwa.
 
Ninaowafahamu wamepigwa ni zaidi ya 5 tena zaidi ya gunia 90 akiwemo baba Mwenye nyumba yangu. Nampongeza tu kakubali matokeo lkn wengine bado hawajui what next. Sasa kama amewekwa ndani miujiza sijui kama ataweza tena kule aliko.
 
Ina mana kufanya biashara kwa hasara ndio unaita kufanya biashara? 🤔
Biashara maana yake si unafanya ili upate faida
Kwa hiyo ukipata hasara hiyo ni biiashara.

Ndio maana biashara ina pande ya faida na hasara.

Biashara ni kuuza na kununua.

Biashara inafaida na hasara.
 
Sasa hapo anatakatishaje?
Tafsiri ya kutakatisha fedha ndio jibu ya swali lako.

Kifupi tu, kutakatisha fedha ni kuingiza fedha kwenye mzunguko halali, ikiwa fedha hiyo uliiipata kwa njia ambayo sio halali (kumbuka ili upate fedha unatakiwa kufanya shughuli halali).

Sasa jamaa ananunua mahindi kwa 70,000 gunia anauza 40,000 hapa sio bure, kuna hela kazipata mahala sasa anaamua kuziweka kwenye mzunguko kupitia kununua mahindi.

Any way court itasema kwa undani, mi najua kwa ufupi tu.
 
Kukatisha fedha ni kitendo cha kutumia fedha kihalali kwenye miradi, biaashara nk fedha ambazo zimepatikana kihalamu au kwa kufichwa fichwa chanz chake
ML.gif
 
Kwa hiyo ukipata hasara hiyo ni biiashara.

Ndio maana biashara ina pande ya faida na hasara.

Biashara ni kuuza na kununua.

Biashara inafaida na hasara.
Yeye alikuwa anafanya biashara ya hasara tu na sio faida, ananunua mzigo bei ya juu anauza bei ya chini
 
Back
Top Bottom