Ruvuma: Afikishwa mahakamani kwa kuzaa na binti yake. Alimlaghai kwa kumwambia anamtibu kupitia uume wake

Mkazi wa kijiji cha Luhagala, kata ya Litumbandyosi wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma, Aleyanda Mdendemi (54) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya kwa tuhuma za kufanya mapenzi na watoto wake wawili na kuzaa na mmoja kati yao.

Akisomewa mashtaka hayo na mwendesha mashtaka wa polisi, Inspekta Seilf Kilungwe mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ally Mkama amedai kuwa mbali na kufanya mapenzi na mabinti zake, pia anatuhumiwa kumuachisha masomo binti yake wa shule ya sekondari.

Mshtakiwa huyo ambaye ni baba mzazi wa watoto hao wawili anadaiwa kutenda makosa hayo katika nyakati tofauti ambapo katika faili la kwanza anatuhumiwa kufanya mapenzi na binti yake (17) mwanafunzi wa kidato cha tatu, Desemba mwaka jana shambani kwao Kata ya Amani Makolo akidai anamtibu kupitia uume wake, kwani binti huyo alikuwa mgonjwa.

Aidha, mwendesha mashtaka ameendelea kudai kuwa mshtakiwa aliendelea kumlaghai binti huyo na kuendelea kufanya naye kitendo hicho kwa kipindi chote wakiwa shambani mpaka waliporudi kijiji cha Luhagala tayari binti yake alikuwa mjamzito na kisha kujifungua mtoto.

Credit: Swahili Times
Ushirikina ni uovu
 
Baradhuli huyu ahasiwe... Awe ndafu
 
Kama huyo binti angekuwa mkubwa na amekubali mwenyewe lingekuwa kosa kwa sheria za Jamhuri? Maana hapo naona kosa ni kama ametembea na bint chini ya 18yrs. Au pana kosa lingine kwa mujibu wa sheria zetu?
 
Haya mambo jaman hua najiuliza kuna mangapi mengine kama haya yanaendelea hayajabahatika kujulikana. Mungu endelea kuwaumbua waovu hawa.
 
Huyo mzee adhabu ya kunyongwa itakua nzuri hata kwake pia coz maisha yake hapa Duniani hayana maana tena kwa dhambi na aibu aliyojichagulia,

Anyway Mungu atatoa hukumu yake pia.
 
Haya mambo jaman hua najiuliza kuna mangapi mengine kama haya yanaendelea hayajabahatika kujulikana. Mungu endelea kuwaumbua waovu hawa.
Wanasema zama iliyojaa mahasi ilikuwa ni ya kina luti sodomah na Gomorrah

Sasa kama ya kwetu ina nafuu pata picha huko kulikuaje
 
Back
Top Bottom