Rutabanzibwa amtunishia msuli Waziri Huvisa

Rutabanzibwa amtunishia msuli Waziri Huvisa

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,331
Rutabanzibwa amtunishia msuli Waziri Huvisa

Na Elias Msuya, Mwananchi

Posted Agosti17 2013

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, amesema tuhuma alizopewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa, za kutetea wahalifu wa mazingira, ni uongo na zinazotokana na moyo wake wa kutetea wanyonge.

Kauli ya Rutabanzibwa imekuja ikiwa ni siku moja tangu Waziri Huvisa kumtaja akimtuhumu kumkingia kifua, Robert Mugishagwe anayemiliki kiwanja Na.2002 eneo la Kawe Beach, Dar es Salaam.

Akijibu madai hayo ofisini kwake Dar es Salaam jana, Rutabanzibwa alisema hakukosea kumwekea dhamana Mugishagwe na kwamba, anazo nyaraka zinazoonyesha uhalali wa kiwanja chake.

“Nimekuwa Katibu mkuu wizara kwa zaidi ya miaka 17, nimekuwa nikizushiwa tuhuma nyingi na nimechunguzwa sana, lakini zote hazina ukweli. Hata tuhuma hizi ndiyo hizohizo za kuzusha,” alisema Rutabanzibwa na kuongeza:

“Waziri aliagiza Mugishagwe akamatwe tangu Januari, nilikwenda Kituo cha Polisi Kawe, nilipowauliza kosa lake wakasema waziri ameagiza akamatwe. Nilimdhamini ili akalale nyumbani siyo mahabusu. Kumdhamini mtu ni kosa? Nilimdhamini ili kama atapotea nikamatwe.”

Huku akionyesha barua ya polisi yenye kumbukumbu Na.KW/K/BI/1/VOL/48, Rutabanzibwa alisema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilipitia jalada la NEMC na kuthibitisha Mugishagwe anamiliki kiwanja hicho kihalali.

“Nilitarajia kwamba baada ya kumkamata, watafungua kesi mahakamani, mbona hawajamfungulii kesi tangu Januari?” alihoji Rutabanzibwa na kuongeza:

“...Hayo ni matumizi mabaya ya madaraka. Ndiyo maana nilimdhamini, siyo kwa sababu yeye ni Mhaya, ila natetea watu wote.”

Huku akiendelea kuchambua nyaraka zake, Rutabanzibwa alionyesha barua iliyotoka Ofisi ya Makamu wa Rais yenye kumbukumbu BA/78/27/01/61 yenye taarifa ya mgogoro wa ardhi na mazingira eneo la Kawe Beach, Dar es Salaam na kwamba taarifa hiyo inathibitisha uhalali wa kiwanja hicho.

“Pale kuna watu wengi walioingilia mto na kuna raia wa kigeni ameuhamisha kabisa wakati hana hata hati ya kumiliki kiwanja hicho, lakini haguswi. Badala yake wanambana tu Mugishagwe. Siwezi kuona mtu anaonewa halafu nikae kando, utakuwa ni unafiki. Lazima nipambane hadi haki ipatikane.”

Alipoulizwa kwa nini asimfuatilie huyo mgeni, aliyedai kuwa ametembeza rushwa kwenye wizara hiyo, alijibu:

“Hapa nina kesi nyingi za rushwa nazifuatilia Takukuru, hata wiki hii nilikuwa shahidi kwenye kesi ya wizi hapa wizarani. Isitoshe hicho kiwanja alipewa kabla sijaingia wizara hii. Lakini kuna rushwa ilitembea hapa wizarani.”
 
Hilo jina km vile la nje ya mpaka kwa magahribi kwa nchi....
 
Katika ile orodha na Mafisadi (List of Shame)ya Dr Slaa iliyotangazwa rasmi pale Mwembeyanga, huyu alishika namba 5. Huwezi kuelewa ameendeleaje kuwa katika utumishi wa serikali🙁

[h=2]5. PATRICK W.R.
RUTABANZIBWA[/h]
ruta.gif

Kwa miaka mingi
Patrick Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini wakati
mikataba mibovu ya madini inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea. Kwa sasa
Bwana Rutabanzibwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na vile vile Mkurugenzi wa
kampuni ya kigeni ya Tangold Limited. Ufisadi unaomhusu umeelezewa kwa kina
katika maelezo yanayomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Hapa pia kuna
mgongano mkubwa kati maslahi yake binafsi kama Mkurugenzi wa kampuni binafsi
iliyopokea mabilioni ya fedha za umma na maslahi ya umma aliyotakiwa kuyalinda
akiwa kama kiongozi wa umma
 
Anakiri kwamba rushwa ipo ofisini kwake?huu ni udhaifu wa kwanza!

Mbona unakimbilia kumhukumu? kasema hivi; alipewa kiwanja kabla yeye hajawa katibu mkuu pale wizarani, inaonekana kuna rushwa ilitembea pale wizarani. wakati huo yeye hakuwepo.kuwa katibu mkuu wa wizara miaka 17 siyo mchezo. lazima ujue yuko imara na anajua kazi yake.
 
....Yes!, miaka 17 ya UFISADI na bado yupo tu!!........ sio mchezo aisee.........hata angekuwa na miaka 30 plus ya Ukatibu Mkuu...lakini hiyo sio hoja ya kuhalalisha au kutetea na kukingia maovu........halafu unajifanya unatetea wanyonge........huyu kweli ametetea wanyonge!!....Mugisha ni mnyonge......au huyu mwenzetu anaishi bongo ipi.........the same Patrick alituingiza Mkenge wa wa IPTL akishirikiana na Rugemarila (mabibo) halafu baadaye akajifanya eti kutetea kupunguza makali........he should be the one in jail right now.........

Wewe Patrick ni bora ukae kimya........maana UMAFIA wako ni mwingi sana pale Ardhi..........
 
Hivi kweli yeye Rutabanzibwa anadhamini wanyonge wote wanaokamatwa?!!! Tangu lini akatetea wanyonge wakati migogoro ya ardhi imezid..ajabu kuu mtu kuwa na kiwanja mtoni halafu anatetewa na Katibu mkuu wa wizara hiyo hiyo iliyogawa kiwanja mtoni...
 
Hii nchi haina adabu ya kazi.katibu mkuu wizara ya Ardhi anasema kuna mtu jirani nhaguswi kwanini yeye asimguse maana ana mamlaka kisheria ya kulinda hifadhi za mito. Na kingne inakuaje Rais anaruhusu wateule wake kujibizana namna hii...
 
BAK, hii yote inaonesha jinsi utendaji serikalini ulivyokuwa at its lowest level ever. Waziri analalamika Katibu mkuu wa wizara anafanya mambo shaghalabagala hachukui hatua ili Katibu mkuu awajibishwe, Katibu mkuu wa wizara hiyohiyo kwa miaka 17 anasema kuna rushwa sana wizarani kwake na bado anaendelea na ukatibu mkuu bila kuchukua hatua yoyote. Sanasana anasema ameenda mahakamani bila kutaja alikuwa anamtetea nanai kwenye kesi iliyofunguliwa na nani. Wizara hii (ardhi) iko ICU sio utani.
 
Sheria si zipo wazi? mimi nashindwa kuwaelewa wote hawa Dr Huvisa na huyo Rutabanzibwa.Kwanini sheria kama inaheshimiwa isifuatwe haki ipatikane?

LINCHI LIGUMU KWELI HILI DUH!!
 
Ongeleeni wote lakini siyo Ruta. Huyu bwana ni mzalendo sana. Alipokuwa KM wa Nishati na Madini alipambana na ufisadi mwingi ukiwepo EPA lakini nguvu za juu zilimwelemea. Waulizeni watumishi wa Ardhi wawasimulie jinsi alivyowadhibiti wezi na wala rushwa.
 
Anakiri kwamba rushwa ipo ofisini kwake?huu ni udhaifu wa kwanza!

You can pick and choose what you want to read or judge, alichosema ni kweli, na udhaifu hauwezi kuwa wake peke yake, ni wa watumishi wote na sisi raia tunaohonga wale watumishi

Patrick is once again right!!!! Siasa kwenye ardhi inaharibu sana migogoro ya ardhi

and they hate him for being straight... sio wa kupindapinda... hata kama ana matatizo yake
 
Hivi inakuwaje huyo mtu anakaa kwenye wizara ya aldhi miaka 17?. Hakuna wengine competent?. Tena wizara hiyo inanuka kwa rushwa za kutoa hati fake za viwanja. Hapo kuna utata. Usalama wachunguze.
 
Ukabila: waziri wa ardhi mhaya katibu mhaya mvamizi mhaya. yamenitokea baraza la ardhi na nyumba kibaha, mvamizi wangu mhaya mwenyekiti wa baraza mhaya wakili wamvamizi mhaya. najua umeshafaham kilichonitokea.
 
....Yes!, miaka 17 ya UFISADI na bado yupo tu!!........ sio mchezo aisee.........hata angekuwa na miaka 30 plus ya Ukatibu Mkuu...lakini hiyo sio hoja ya kuhalalisha au kutetea na kukingia maovu........halafu unajifanya unatetea wanyonge........huyu kweli ametetea wanyonge!!....Mugisha ni mnyonge......au huyu mwenzetu anaishi bongo ipi.........the same Patrick alituingiza Mkenge wa wa IPTL akishirikiana na Rugemarila (mabibo) halafu baadaye akajifanya eti kutetea kupunguza makali........he should be the one in jail right now.........

Wewe Patrick ni bora ukae kimya........maana UMAFIA wako ni mwingi sana pale Ardhi..........

Kweli wewe mgeni huujui vizur mgogoro ulivyokwenda. Jaribu kuwaliza waliokua wizarani kipindi hicho wakwambie kauli za Patric kuhusiana na IPTL, unajua ni kwa nini baadhi ya vikao muhimu kusiana na IPTL vilifanyika bila PS kuwepo?
 
Hapo pana taabu tayari!!!!!

Maadam kamati ya bunge imechukua taarifa na tusubiri tutajua ya kuyajua

Ila hili la kusema huyu anaonewa kwa sababu kuna yule kafanya kosa na hajafanywa kitu hapa ndo hii nchi siilewi kabisa!!!!

Mnaodai huyu yuko straight ,ndio hivi au straight ina maana zaidi ya moja!!!!!
 
...Mkuu hii issue tulianza nayo siku nyingi sana hata kabla huu ukumbi wa JF haujazaliwa.......i.e. tangu bcs...ukifuatilia zile taarifa za kuandikwa tangu wakati ule utapotea......n ya mikataba....na IPTL ni mmojawapo.........
 
Hapo pana taabu tayari!!!!!

Maadam kamati ya bunge imechukua taarifa na tusubiri tutajua ya kuyajua

Ila hili la kusema huyu anaonewa kwa sababu kuna yule kafanya kosa na hajafanywa kitu hapa ndo hii nchi siilewi kabisa!!!!

Mnaodai huyu yuko straight ,ndio hivi au straight ina maana zaidi ya moja!!!!!

...wengine wanasema jamaa huyu ana experience ya miaka 17 kama Katibu Mkuu wa Wizara mbali mbali...na watu wengine wanaona eti ni "point".........damn!.....yaani jitu na akili zake linaanika upuuzi kusema....eti mimi ni Katibu Mkuu kwa miaka 17!.......
 
RUTABANZIBWA....Rutabanzibwa....HUYU NI FISADI KWELI KWELI.... na hata hapa onaona jeuri yake HE DOESN*T CARE ABOUT MINISTER...HE IS PURELY FISADI LONG TIME..

===>> Mama Tibaijuka kashindwa kumtimua kisa MHAYA MWENZAKE...na bado hapa anamkingia kifua mhalifu MHAYA mwenzake....
na huku yeye ni katibu wa Wizara ya ardhi....unategemea nini hapa...???

===>> HUYU NI KUPIGA KELELE KILA KONA KTK MIKUTANO YA MIHADHARA NA MITANDAONI NA MAGAZETINI HADI RAIS AMTUPE NJE NA KUSHTAKIWA....

===>> Fisadi papa huyu Rutabanzibwa amezorotoshe sana maendeleo ya wizara kwa rushwa kubwa kubwa...na mama Tibaijuka kwacha sbb ni UKABILA...

==>> JK mfukuze huyu haraka na umechelewa...plz
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom