Rutabanzibwa amtunishia msuli Waziri Huvisa

Rutabanzibwa amtunishia msuli Waziri Huvisa

...Mkuu hii issue tulianza nayo siku nyingi sana hata kabla huu ukumbi wa JF haujazaliwa.......i.e. tangu bcs...ukifuatilia zile taarifa za kuandikwa tangu wakati ule utapotea......n ya mikataba....na IPTL ni mmojawapo.........

Unakumbuka kauli zilizotolewa na wanahisa wa IPTL dhidi ya huyo bwana kuhusiana na ripoti ya WB.
 
Hivi huyu ndiye anayetajwa tajwa kwenye maskendo mengi ya kifisadi? Hiyo Wizara wamepangana, Waziri Mhaya, Katibu Mhaya mtuhumiwa Mhaya. Hivi hapo NEMC itapeleka tingatinga?
 
Katika ile orodha na Mafisadi (List of Shame)ya Dr Slaa iliyotangazwa rasmi pale Mwembeyanga, huyu alishika namba 5. Huwezi kuelewa ameendeleaje kuwa katika utumishi wa serikali🙁

5. PATRICK W.R.
RUTABANZIBWA



ruta.gif

Kwa miaka mingi
Patrick Rutabanzibwa alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini wakati
mikataba mibovu ya madini inasainiwa na kashfa kubwa ya IPTL inatokea. Kwa sasa
Bwana Rutabanzibwa ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na vile vile Mkurugenzi wa
kampuni ya kigeni ya Tangold Limited. Ufisadi unaomhusu umeelezewa kwa kina
katika maelezo yanayomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Hapa pia kuna
mgongano mkubwa kati maslahi yake binafsi kama Mkurugenzi wa kampuni binafsi
iliyopokea mabilioni ya fedha za umma na maslahi ya umma aliyotakiwa kuyalinda
akiwa kama kiongozi wa umma

nchi hii na ufisadi bado sana
 
Maswali yangu kwa Rutabanzibwa;
1:Kama huyo raia wa kigeni unayedai alipatiwa hati kwa mgongo wa rushwa kwa watumishi wa ofisi yako je huyo Mhaya mwenzio una uhakika gani kuwa hakupata hati kwa mgongo wa rushwa na ukabila kwako mwenyewe na watumishi wako?
2.Tatizo hapa sio kuwa na vibali halali wala feki bali ni kujenga katika maeneo ambayo siyo sahihi kwa mazingira,na vibali vyote vinatoka katika ofisi yako,kwa nini wasibanwe hao waliotoa vibali hivyo?
 
Hutu Katibu Mkuu ni kilaza mkubwa, amenihuzunisha sana kwa maneno yake yasiyoonyesha uwajibikaji
 
Anasema kuna mtu pale jirani haguswi, wakati yeye ndio katibu mkuu wizara yenye dhamana na ardhi anayetakiwa kusimamia matumizi bora ya ardhi, sasa anataka nani amguse?:eek
 
Mkuu Nzi kwenye taratibu za uandishi ukimquote mtu unastahili kumquote hadi mwisho,..nimeandika sentence nzima ukijichukulia kipande ukataka ufafanuzi nadhani sio sahii...ujumbe wangu uko kwenye kipande ulichoacha
 
Last edited by a moderator:
Ni mtizamo wangu kuwa kuna issue nyingi sana zinazohitaji kushughulikiwa kiwizara kama vile kusimamia utekelezaji wa sheria na sera,miji yetu kujengwa kiholela,wananchi kutokulipwa fidia ya kutosha na kwa wakati,kutafsiri sera sahihi hususan pale mamlaka za chini zinaposhindwa kutekeleza sera etc kama hili suala la Mhe.Huvisa-Wizara ya Ardhi ilitakiwa kutoa tafsiri sahihi ya nini kifanyike,cha ajabu Katibu Mkuu anapata muda wa kutoa dhamana na sio kutoa tafsiri nini kifanyike?,hawa ndio viongozi wetu,ana miaka 17 kama Katibu Mkuu kwa kudhamini watu au?
 
....Yes!, miaka 17 ya UFISADI na bado yupo tu!!........ sio mchezo aisee.........hata angekuwa na miaka 30 plus ya Ukatibu Mkuu...lakini hiyo sio hoja ya kuhalalisha au kutetea na kukingia maovu........halafu unajifanya unatetea wanyonge........huyu kweli ametetea wanyonge!!....Mugisha ni mnyonge......au huyu mwenzetu anaishi bongo ipi.........the same Patrick alituingiza Mkenge wa wa IPTL akishirikiana na Rugemarila (mabibo) halafu baadaye akajifanya eti kutetea kupunguza makali........he should be the one in jail right now.........

Wewe Patrick ni bora ukae kimya........maana UMAFIA wako ni mwingi sana pale Ardhi..........

Duh! Miaka 17 same ministry? Huu sasa ni wakati muafaka ahamishiwe wizara nyingine.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ongeleeni wote lakini siyo Ruta. Huyu bwana ni mzalendo sana. Alipokuwa KM wa Nishati na Madini alipambana na ufisadi mwingi ukiwepo EPA lakini nguvu za juu zilimwelemea. Waulizeni watumishi wa Ardhi wawasimulie jinsi alivyowadhibiti wezi na wala rushwa.

Mimi ninashangaa sana nchi hii kuwa huyu bwana bado yumo serikalini; kwanza afya yake ni ya mgogoro licha ya kuhusika na tuhuma nyingi za rushwa!! Sasa huyo anayesema alimuwekea dhanana kwasababu alikuwa anaonewa na sio kwasababu ni muhaya mwenzie; wananchi wangapi wameonewa na yeye hakuenda kuwawekea dhamana? Alikwenda kumuwekea dhamana Mugishagwe kwasababu ni muhaya mwenzie na wanafanya biashara pamoja period!! Wizara hii itazidi kuwatesa wananchi kwasababu ya lack of management prowess ya Mkweree kwa kufanya makosa ya kuwaweka Tibaijuka na Rutabanzibwa wakiwa wote washomile kuongoza wizara moja nyeti kama hiyo!!!
 
Nimesoma comments za watu hapa....kweli watanzania wengine ni vichekesho...

Inatakiwa watanzania tujifunze utawala wa sheria...mimi namtetea huyu katibu mkuu kwa anavyojitahidi kufanya kazi kwenye mazingira magumu....hiyo wizara ni ngumu na ina ufisadi mwingi lakini anajitahidi kuchukua hatua za kuupunguza...shida ya watanzania wanataka mtu anayepiga kelele kwenye vyombo vya habari ndio wajue anafanya kazi...kwa taarifa huyu alikua against IPTL kwa msiofahamu, lakini ikaletwa kwa nguvu za JK....huyu huyu amewahi kushtakiwa mara nyingi na kuna wakati mafisaidi walikua wamfunge jela kama sio jaji mkuu kuingilia hukumu....alichofanya hapa ni kuhakikisha sheria inafuatwa labda alikua anamfahamu anayeonewa....kama mnakumbuka hata lile soo la rose garden na manispaa ya kinondoni walipotaka kukurupuka tu kuvunja ikabidi magufuli aingilie kati akawaambia kavunjeni tu kama hamtalipa mabilioni.....hawa wadau wanaopiga kelele mbona hamuendi kuvunja nyumba ya lwakatare sababu wanaogopa kulipa .....hii wizara imejaa ufisadi wa kufa mtu na ulianza tangu serikali ya awamu ya pili....
 
....Yes!, miaka 17 ya UFISADI na bado yupo tu!!........ sio mchezo aisee.........hata angekuwa na miaka 30 plus ya Ukatibu Mkuu...lakini hiyo sio hoja ya kuhalalisha au kutetea na kukingia maovu........halafu unajifanya unatetea wanyonge........huyu kweli ametetea wanyonge!!....Mugisha ni mnyonge......au huyu mwenzetu anaishi bongo ipi.........the same Patrick alituingiza Mkenge wa wa IPTL akishirikiana na Rugemarila (mabibo) halafu baadaye akajifanya eti kutetea kupunguza makali........he should be the one in jail right now.........

Wewe Patrick ni bora ukae kimya........maana UMAFIA wako ni mwingi sana pale Ardhi..........

mbona huyo mzungu hajashughulikiwa, je kwann alimwekea dhamana mhaya mwenzie, ni nani yake, je kiwanja ni chake au sio chake, kwann yy ana huruma sana kwa huyu mtu, kwani huyu mtu hana ndugu au anashikilia kiwanja chake
 
Sheria si zipo wazi? mimi nashindwa kuwaelewa wote hawa Dr Huvisa na huyo Rutabanzibwa.Kwanini sheria kama inaheshimiwa isifuatwe haki ipatikane?


LINCHI LIGUMU KWELI HILI DUH!!

CCM ni kama JAMBAZI, Ona hali ilivyo




Kwa hali ilivyo ukitaka kufanya compare and contrast juuya CCM na Jambazi, utaona sifa nyingi za jambazi CCM anazo, kama kawaidamifano:
1. Wote wanamiliki Silaha kinyume na sheria (picha yawatoto/greengurad wanasilaha, je waliazima polisi wapigie picha, au ni za CCM?Je polisi wanaruhusiwa kuazimisha silaha?)

2. Wote wanaua (Kombe, Kolimba, Mwaikambo, Rutabago,Mwangosi, Arusha, Mwanza, Pemba etc)

3. Wote hawasemi UKWELI(Richmond hadi leo wanasutana,Mwenyekiti ni kipi nilifanya bila taarifa na maelekezo yako)

4. Wote ni wabishi, hata kama jambo limewashinda watang’ang’aniampaka wauawe

5. Wote wanatumia nguvu kupata kisicho halali

6. Jambazi anaiba mali CCM anaiba Kura na Madaraka

7. Sifa kubwa ya Jambazi hawatajani (Jiulize wauza unga JKanawajua, ametaja?? EPA waliorudisha hela anawajua ametaja??)

8. Wote wanacheka huku wakati wowote wanaweza kukuua,kumbuka yule kijana wa UDSM na laptop yake

9. Wote ni wakimatwa wanakuwa wapole kama bibi harusi,(arusha mjini, mwanza, tarime enzi za chacha wangwe)

10. Lakini cha ajabu wote wakipanwa na kupata kichapo chakweli husema ukweli, tupu.
CCM tuwabane hivi hivi watasema tu UKWELI kama jambaziakipanwa pumb na kucha.
Je kuna mtu anadhani CCM na Jambazi sio kitu chenye sifaza kufanana? Bado tu unataka kutekeleza pointi namba 4 Hapo juu??? Au unatakakuongeza comparison??? Nisaidie mkuu.
 
Rutabanzibwa amtunishia msuli Waziri Huvisa
Na Elias Msuya, Mwananchi
Posted Agosti17 2013 saa 23:15 PM
Kwa ufupi

Kauli ya Rutabanzibwa imekuja ikiwa ni siku moja tangu Waziri Huvisa kumtaja akimtuhumu kumkingia kifua, Robert Mugishagwe anayemiliki kiwanja Na.2002 eneo la Kawe Beach, Dar es Salaam.


Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, amesema tuhuma alizopewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa, za kutetea wahalifu wa mazingira, ni uongo na zinazotokana na moyo wake wa kutetea wanyonge.

Kauli ya Rutabanzibwa imekuja ikiwa ni siku moja tangu Waziri Huvisa kumtaja akimtuhumu kumkingia kifua, Robert Mugishagwe anayemiliki kiwanja Na.2002 eneo la Kawe Beach, Dar es Salaam.

Akijibu madai hayo ofisini kwake Dar es Salaam jana, Rutabanzibwa alisema hakukosea kumwekea dhamana Mugishagwe na kwamba, anazo nyaraka zinazoonyesha uhalali wa kiwanja chake.

“Nimekuwa Katibu mkuu wizara kwa zaidi ya miaka 17, nimekuwa nikizushiwa tuhuma nyingi na nimechunguzwa sana, lakini zote hazina ukweli. Hata tuhuma hizi ndiyo hizohizo za kuzusha,” alisema Rutabanzibwa na kuongeza:

“Waziri aliagiza Mugishagwe akamatwe tangu Januari, nilikwenda Kituo cha Polisi Kawe, nilipowauliza kosa lake wakasema waziri ameagiza akamatwe. Nilimdhamini ili akalale nyumbani siyo mahabusu. Kumdhamini mtu ni kosa? Nilimdhamini ili kama atapotea nikamatwe.”

Huku akionyesha barua ya polisi yenye kumbukumbu Na.KW/K/BI/1/VOL/48, Rutabanzibwa alisema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilipitia jalada la NEMC na kuthibitisha Mugishagwe anamiliki kiwanja hicho kihalali.

“Nilitarajia kwamba baada ya kumkamata, watafungua kesi mahakamani, mbona hawajamfungulii kesi tangu Januari?” alihoji Rutabanzibwa na kuongeza:

“...Hayo ni matumizi mabaya ya madaraka. Ndiyo maana nilimdhamini, siyo kwa sababu yeye ni Mhaya, ila natetea watu wote.”

Huku akiendelea kuchambua nyaraka zake, Rutabanzibwa alionyesha barua iliyotoka Ofisi ya Makamu wa Rais yenye kumbukumbu BA/78/27/01/61 yenye taarifa ya mgogoro wa ardhi na mazingira eneo la Kawe Beach, Dar es Salaam na kwamba taarifa hiyo inathibitisha uhalali wa kiwanja hicho.

“Pale kuna watu wengi walioingilia mto na kuna raia wa kigeni ameuhamisha kabisa wakati hana hata hati ya kumiliki kiwanja hicho, lakini haguswi. Badala yake wanambana tu Mugishagwe. Siwezi kuona mtu anaonewa halafu nikae kando, utakuwa ni unafiki. Lazima nipambane hadi haki ipatikane.”

Alipoulizwa kwa nini asimfuatilie huyo mgeni, aliyedai kuwa ametembeza rushwa kwenye wizara hiyo, alijibu:

“Hapa nina kesi nyingi za rushwa nazifuatilia Takukuru, hata wiki hii nilikuwa shahidi kwenye kesi ya wizi hapa wizarani. Isitoshe hicho kiwanja alipewa kabla sijaingia wizara hii. Lakini kuna rushwa ilitembea hapa wizarani.”




Hilo Eneo la Kawe Beach Lina vionja vingi hasa Eneo la kiwanda cha Tanganyika pekas kumegwa na wajanja na Kama huyo katibu Mkuu amekuwa Wizarani kwa Miaka 17 Nadhani umefika mda ahamishiwe wizara ingine akapumzike
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom