Russia quits International Criminal Court

Russia quits International Criminal Court

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
Rais wa Urusi Vladmiri Putin ametia saini maagizo ya kumuamuru Waziri wa Mambo ya Nje kumpa taarifa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa Urusi inajisitisha kuwa mjumbe wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita(ICC).

Mahakama inayoendesha na Mkataba wa Rome(Rome Statute) unaungwa mkono na wajumbe ambao ni jumla ya nchi 123.

===========================
Putin_Signs.jpg

Vladimir Putin signed a directive instructing Ministry of Foreign Affairs to inform the UN Secretary General that Russia no longer intend to become a state party to the Rome Statute of the International Criminal Court.

The Rome Statute which established the court has been ratified by 123 countries.

Russia signed the documents in 2000 but did not ratify it. Despite not falling under jurisdiction of the court Russia continued to cooperate with it and participated in its work as an observer.

Israel, Sudan and the United States were the first to inform the UN Secretary General that they no longer intend to become states parties to the Rome Statute.

This year South Africa, Gambia and Burundi also took actions to quit the International Criminal Court. Uganda and Kenya are reportedly on their way out.

Source: rapsinews.com
 
hiyo ni msg mwanaume anatuma kwa NATO kuwa anajiandaa kufanya unyama ambao hata shetani mkuu akipata nafasi kushudia nahis ataenda kuomba hifadhi mbinguni!!!!
 
Serikali ya Urusi imetangaza kuidhinisha uamuzi wa kutaka kujitenga na mahakama kuu ya kimataifa.

582c74ff61dc8.jpg

Kulingana na maelezo yaliyotolewa na ikulu ya Kremlin, iliarifiwa kwamba rais Vladimir Putin ametia saini rasimu ya uamuzi huo wa kutaka kujitenga na mahakama kuu ya kimataifa kufuatia pendekezo la wizara ya sheria na masuala ya nje.

Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Putin pia alitoa agizo la kuwasilishwa kwa uamuzi huo kwa ofisi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitriy Peskov alifahamisha kuchukuliwa kwa uamuzi huo kutokana na vizuizi vya sheria vilivyopo kwa taifa la Urusi.

Wizara ya masuala ya nje ya Urusi pia ilikahsifu mahakama kuu ya kimataifa kwa ukosefu wa haki na uadilifu katika sheria kutokana na kushindwa kujitegemea.

Mahakama hiyo pia inadaiwa kuangazia mzozo wa Georgia wa mwaka 2008 kwa upande mmoja na kughadhabisha Urusi.
 
Huwezi kupitisha manowari kama zile Warusi walizopitisha jirani na Uingereza kwenda Syria halafu ukaendelea kuwa mwanachama wa ICC. Ni lazima ujitoe kwanza ili uweze kuvitumia vifaa vyako vizuri na kwa uhuru. Putin sio mjinga; anajua sana hilo.
 
Ngoja tuone Wamagharibi watakuja na hila gani mpya baada ya hii ICC kukimbiwa na kupoteza uzito wake. ICC ilikuwa na mazuri yake na mabaya. wapo waiohukumiwa na wapo waliotishwa. Kubwa ni kuwa hakikuwa chombo huru bali kiliwekwa kwa lengo la kuwatisha vibaraka wao na kuwatia adabu au kuwashurutisha watii matakwa yao. Nafikiri hilo ndilo lilimnusuru Uhuru kenyatta. Mahakama hii upande mwingine imekuwa na mtazamaji wa mauaji tuuu. Tanzania tujitoe
 
koh koh koh... tukijitoa akina maalim seif watakwenda kushtaki wapi sasa???
 
Serikali ya Urusi imetangaza kuidhinisha uamuzi wa kutaka kujitenga na mahakama kuu ya kimataifa.

582c74ff61dc8.jpg

Kulingana na maelezo yaliyotolewa na ikulu ya Kremlin, iliarifiwa kwamba rais Vladimir Putin ametia saini rasimu ya uamuzi huo wa kutaka kujitenga na mahakama kuu ya kimataifa kufuatia pendekezo la wizara ya sheria na masuala ya nje.

Maelezo zaidi yanaarifu kwamba Putin pia alitoa agizo la kuwasilishwa kwa uamuzi huo kwa ofisi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitriy Peskov alifahamisha kuchukuliwa kwa uamuzi huo kutokana na vizuizi vya sheria vilivyopo kwa taifa la Urusi.

Wizara ya masuala ya nje ya Urusi pia ilikahsifu mahakama kuu ya kimataifa kwa ukosefu wa haki na uadilifu katika sheria kutokana na kushindwa kujitegemea.

Mahakama hiyo pia inadaiwa kuangazia mzozo wa Georgia wa mwaka 2008 kwa upande mmoja na kughadhabisha Urusi.
Kimeshanuka sasa, naiona vita baridi ikiwa kwenye mwendo kasi
 
Hili vuguvugu la nchi wanachama wa ICC kujitoa unachama kwangu mimi nina mtazamo hasi wa nchi hizi kujitoa.

NINI MAANA YAKE

watawala wengi hawatakuwa na hofu juu ya tawala zao kwa kujua hakuna sehemu ya kuwashitaki, tawala nyingi duniani hasa Afrika zitakuwa za kidharimu. Pamoja na matatizo ya ICC tena hii mahakama ina matatizo mengi, Nchi za Afrika wanaiona hii mahakama kama ilianzishwa kwa ajili ya viongozi wa Afrika na ukiangalia hii ina ukwel ndani yake, kesi nyingi za ICC ni za Afrika na haina maana viongozi wa nchi zingine wahajafanya makosa ya kuweza kushitakiwa na mahakama hiyo ukizingatia nchi tano za baraza la usalama ndiyo zenye maamuzi ya nani ashitakiwe na nani asishitakiwe ila katika hizo nchi tatu siyo mwanachama wa mahakama hiyo. Pamoja na mapungufu ya mahakama hiyo ila inasaidia sana viongozi kutofanya maovu kwa kujua kuna mahakama na ipo siku watafikishwa mbele ya ICC kidogo wanakuwa na uwoga
 
Back
Top Bottom