Rushwa yatawala ugawaji viwanja Mbeya! RIZ-1 KUPEWA TENA???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rushwa yatawala ugawaji viwanja Mbeya! RIZ-1 KUPEWA TENA????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 21, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,343
  Likes Received: 3,230
  Trophy Points: 280
  Rushwa yatawala ugawaji viwanja Mbeya


  na Moses Ng'wat, Mbeya


  [​IMG]
  ZOEZI la ugawaji wa maeneo ya kujenga vibanda vya biashara kwa wafanyabiashara waliounguliwa na Soko la Uhindini, jijini Mbeya, limeanza kukumbwa na vitendo vya rushwa.
  Hatua hiyo imetokana na baadhi ya watendaji wa halmashauri ya jiji hilo kudaiwa kupokea rushwa kutoka kwa watu ambao si wahanga wa tukio hilo ili wapewe upendeleo.
  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima na kuthibistishwa na viongozi wa Soko la zamani la Uhindi lililoungua moto Desemba mosi mwaka jana, umebaini kuwa watendaji wa Jiji la Mbeya wanaodaiwa kupewa mlungula ni wale ambao wanahusika katika mchakato wa kugawa maeneo hayo.
  Taarifa zaidi zinaeleza kuwa watendaji hao, wamepewa rushwa ya kuanzia sh 200,000 hadi 300,000 na kuwagawia maeneo ya kujenga vibanda hivyo.
  Wakizungumza kwa masharti ya majina yao kutoandikwa gazetini, baadhi ya wafanyabiashara hao ambao baadhi yao wamekiri kubadilishiwa maeneo tofauti na yale walioonyeshwa awali, walidai kuwa baadhi ya wafanyabiashara wenzao wenye mitaji mikubwa wametoa fedha na kupewa maeneo hayo.
  Walisema wafanyabiashara hao wanaojiita G8, awali waliyakataa maeneo waliyopangiwa kwa madai kuwa hayakuwa na hadhi ya kuweka biashara zao hali iliyosababisha kutumia uwezo wao wa fedha kuwahonga maofisa wa jiji hilo. Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo lililoungua, Emily Mwaituka, alipotakiwa kutolea ufafanuzi malamiko hayo alikiri kuwepo na kwamba suala la ugawaji wa nafasi kwa ajili ya ujenzi wa vibanda katika eneo hilo jipya ulisimamiwa zaidi na jiji na wao walihusika kuthibitisha uhalali wa wafanyabiashara. Lakini pia alisema kuwa katika zoezi hilo zaidi ya wafanyabiashara 200 wamekosa nafasi na kwamba hali hiyo ilitokana na mkanganyiko uliojitokeza kati ya wafanyabiashara na uongozi wa jiji.
   
Loading...