Rushwa ya ngono St.John's University inatishia usalama wa wanafunzi wa kike

Wana JF
Kwamza naomba MODS iacheni hii mada hapa maana tutapata michango mingi .Chuo cha st.John's pale Dodoma kuna tatizo kubwa la walimu kuwakamata wananfunzi na kuwalazimisha ngono .Nimeshuhudia mwanafunzi last week amekamatwa na mwalimu kamwambia ajisalimishe .Kamtumia sms na calls kum harrass huyu binti na mwisho ametoa matokeo akiwa ameamua mwanagunzi huyu asimalize chuo na inabidi arudie mwaka mzima .Ushahidi uko wazi umekuwa documented hatua imechukuliwa baada mtego kwa kushirikiana na jeshi la polisi , kwa mumwachia mwanafunzi akubali matakwa ya mwalimu , alimpigia simu mbele uongozi wa polisi na kumwambia yuko tayari kwa ngono na bila ajizi mwalimu aliitikia kwa bashasha na aliwahi kituoni akamchukia mwanafunzi na kabla hajaondosha gari alikamatwa baada ya mahojiano ya siku 2 mwalimu kaamua kubadilisha matokeo ya mwanafunzi baada ya supplementary na sasa mwanafunzi ata graduate mwezi ujao .

Naomba msaada toka kwenu juu ya ufumbuzi wa hilli jambo huko vyuoni hali ni mbaya na rushwa ya ngono imeshika kasi .What is the solution to this problem ?

Ina maana St.John's mtu mmoja anajiweke matokeo anavyotaka, hakuna vikao vya kupitisha matokeo? Yaani jamaa kutoka tu Polisi akabadirisha matokeo. Mhu, labda lakini kwa wanaojua taratibu zamitiani ya vyuo vikuu hii haingii akilini
 
Mkuu shida ni moja kwamba Polisi wanampa onyo mwalimu na kumtaka asirudie na kusema muhimu mwanafunzi amalize chuo .Lakini kesi imesha funguliwa na polisi wamekuja na hilo .Huyu mwalimu na wenzake wana wanawatesa sana wananfunzi na kuwanyanyasa ndiyo maana nimekuja hapa nikiwa kwamba kuna wengi wenye mawazo tofauti ila nataka jambo hili liwe wazi kuna mwalimu St.John's ana tabia mbaya mno.Shida kwa wazazi nk .

Kama ni kweli jambo funguka,huna haja ya kuzunguka zunguka,taja jina la mwalimu,sema suala hili limefikishwa kituo gani cha polisi na km una jina la polisi taja tu kwani naamini mtandao huu makini unatembelewa na watu mbalimbali wakiwemo wasimamizi wa sheria ,wanaharakati na viongozi wa chuo chako ili waweze kulifanyia kazi
 
Ni ujinga na kutokuwa siriasi na shule kwa wasichana walio wengi. Huwezi kukamatwa kama unaouwezo darasani. Kwa upande wa waalimu wa kiume ni binaadamu wenye uzaifu mkubwa wa ngono, kikubwa ni kuwa makini tu. Pia upande wa vyama vya wanafunzi vinatakiwa visisitize uwazi ktk usahihishaji wa mitihani.
 
WAKO WAPI TAMWA,TGNP,AMREF na watetezi wengine wa wanawake??????Mbona hawapigi kelele na unyanyasaji huu wa kijinga!!!ZIKO WAPI KAMPENI ZA KUWANUSURU WATOTO WA KIKE,KWENYE LUNINGA?????????TAKUKURU nao wapo kimya na rushwa ya ngono.
HAPA LAZIMA SAUTI IPAZWE NA MITEGO KWA KUSHIRIKIANA IENDESHWE,KAMPENI ZA KUANZA KUPINGA UNYANYASAJI HUU ZIONGEZWE NA WASHIRIKA WANAOTETEA WANAWAKE NA WADAU WENGINE.
 
Yote haya yanatokea kwasababu hakuna utawala wa sheria katika Nchi hii na Culprits wanalifahamu hilo vizuri.Nchi nyingine Walimu wanaogopa kabisa kujihusisha na rushwa za aina yoyote kwasababu wanajua wakikamatwa kwaajili ya makosa ya namna hiyo ni jela tu hakuna mjadala hapo.Kwa wenzetu case za kuwalazimisha Wanafunzi wa kike kutoa rushwa ya ngono ili apewe marks nzuri wanaita sexual abuse or sexual harassment against women na ni case zinazopigwa vita sana huko na makundi ya kijamii (civil organizations) yanayotetea haki za watoto na wanawake.Kwa hiyo ishu hapa ni kwamba kwanza Nchi yenyewe haina utawala wa sheria na ndio maana watu hawaogopi kujihusisha na vitendo vinavyokiuka sheria;Pili,Watanzania tumelala sana linapokuja suala la kujitambua na kufahamu nafasi/umuhimu wetu ni nini hapa Tanzania.Tungejitambua kwa njia kama hizi nina uhakika hivi vitendo vingekuwa vinatokea katika kiwango cha chini sana,Ila kwa jinsi tunavyoliangalia hili tatizo la sexual abuse ni kama vile acceptable practices in Tanzania!
 
St. John ina uongozi wa ajabu sana, nlishapewa malalamiko haya last semister, ngoja nitafute jina la huyo mkufunzi niliweke hapa, imefika muda tuache fumbia macho huu upuuzi.
 
Yaaaani hakuna chuo jina madenu wabayaaaa kama hiki....mxxxxh yaaani huyo mwalimu naye hana choices kabisa....
 
Siku hizi kusoma ni kwingi, ila watu hawaelimiki. Inshu kama hii enzi zetu tulikuwa tunaimaliza sisi wenyewe wanafunzi, sasa nyie mnaenda hadi polisi!! Anyway, inshu kubwa hapo ni wanafunzi wenyewe mnakaa vibaya darasani, hamsoni, mnajilegeza legeza hovyo na Mwl. akiwa strict to the rules mnaanzisha skendo kama hizo. Simtetei huyo Mwl. ila hatujapata maelezo upande wake, hivyo ni ngumu kuanza kumlaumu moja kwa moja.
 
Mwalimu hayuko sahihi hata kidogo ila dada zetu vyuo vyote wanatumia hyo mianya ya kuwastarehesha lectures kurahisha masomo yao.
Dada zetu(si wote)hawapendi kuumia kusoma wakati kuna shortcut,mimi nakumbuka kipindi nasoma chuo kuna wasichana ambao kwenye lecture hawaonekani lakini tuligraduate wote!
Lunyungu una nafasi ya kuwashawishi wenzao kuacha mchezo wa kutegemea miili yao kurahisha masomo,badala ya kutegemea ngono waambie wasome.
 
Mkuu shida ni moja kwamba Polisi wanampa onyo mwalimu na kumtaka asirudie na kusema muhimu mwanafunzi amalize chuo .Lakini kesi imesha funguliwa na polisi wamekuja na hilo .Huyu mwalimu na wenzake wana wanawatesa sana wananfunzi na kuwanyanyasa ndiyo maana nimekuja hapa nikiwa kwamba kuna wengi wenye mawazo tofauti ila nataka jambo hili liwe wazi kuna mwalimu St.John's ana tabia mbaya mno.Shida kwa wazazi nk .

Mkuu Lunyungu asante uzi huu.
Hii kesi taarifa imeenda tamwa, tawla na tgnp? Nadhani hili kwao ni dili na watasaidia kufuatilia ili haki itendeke. Huyo mwanafunzi anastahili 'credit' kwa ujasiri wake.
 
Last edited by a moderator:
St John maana yake ni MTAKATIFU YOHANA!!

Sasa kama watakatifu ndio hivyo!
Na wale wa kawaida je! Si ndio watatumalizia watoto wa kike!!?
Mi nashauri serikali.ikimkamata mwalimu anafanya kitendo hicho basi imfamfanye HASI!
YAANI IUE KABISA NGUVU ZA KIUME!
Awe khanatha!
 
Hapo issue ni walimu wachache mno, ingekuwa wanafunzi wengi wanapenda fani ya ualimu walimu wangekuwa wengi na kama ikitokea tatizo kama hili asingekanywa wangem fire


Sent from my BlackBerry 8900 using JamiiForums
 
Inauma sana,lakini kuna haja ya kuanzisha mfumo/mechanism ambayo itanusuru mambo kama hayo
 
Watoto wa kike hawapendi kusoma siku hizi matokeo yake wanajitia majaribuni wanapofeli
 
nadhani ungewatembelea TGNP(mtandao wa jinsia Tanzania), TAMWA, au chama cha wanasheria wanawake Tz hao wangekusaidia zaidi. Polis wanapoozwa kwa pesa hao. Mwenye mawasiliano ya hizo taasisi amsaidie huyo ndugu.
"Chage begins with me & together we can"
 
Back
Top Bottom