I totally disagree with you that HR Manager has his guys, who works for him for malpractices purposes. Ninachoweza kusema ni kuwa kuna vijana wengi pale mitaani Kakola, Bugarama na Ilogi wanao tapeli watu kuwa watawapa kazi kupitia kwao. Hao watu kwa sababu ya kutaka kazi wanaingia mkenge, sasa aliyeliwa pesa yake anajua hiyo ni Barrick, which is not true.
Kuhusu chama cha IBUKA, kama nilivyosema awali ni chama kilichoanzishwa na wanakijiji wanaozunguka maeneo ya mgodi wa Bulyanhulu ili vijana wanao toka eneo hilo wapate ajira. Barrick ilichokifanya ni kuhakikisha kuwa chama kinapata viongozi wanakijiji watakao kiongoza, tokea muda mrefu chama kinajiendesha chenyewe na Barrick wakitaka kuajili kutoka kijijini wanawasiliana na viongozi wa IBUKA na viongozi wa IBUKA ndo wanaoleta watu kulingana na idadi waliyo ambiwa na Barrick. If there is any malpractices katika hicho chama that is not Barrick it is IBUKA, wanakijiji wanaopatwa na matatizo ya kuombwa rushwa watoe taarifa katika uongozi wa mgodi, ili uongozi ujue, maana unakuta mtu ametoa rushwa halafu anakaa kimya na badala yake anakuja kulalamika huku JF.
Lakini pia hiyo IBUKA ni kwa ajili ya wanakijiji wanaozunguka mgodi ila unakuta watu kutoka Kahama, Shinyanga, Mwanza, Kagera, Dar es salaam etc. ambao sio wakazi wa pale wanaenda kuomba kazi na hao ndo wanashawishi viongozi wa IBUKA kupokea rushwa.