Rushwa wazi wazi migodi ya Barrick

Rushwa wazi wazi migodi ya Barrick

Sir M.D.Andrew

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2012
Posts
202
Reaction score
37
Ni wawekezaji,ambao waliahidi kutoa fursa sawa za ajira kulingana na fani ya muombaji,lakini hali si shwari migodi ya barrick hasa buzwagi na bulyanhulu... Rushwa iko wazi bila pesa kazi hazipo,wanatangaza magazetini kila kukicha lakini kwa uhalisia barrick wameendekeza rushwa sana.

Tumefika hapo, tumekaa hapo muda mrefu imefikia hatua mtu anakuambia ni kiasi gani cha pesa utatoa ili kupata nafasi fulani,mfano kama kazi ina mshahara wa laki 8 kwa mwezi utatakiwa kutoa rushwa ya million moja,na watakupa mkataba wa miezi sita,ukihitaji kuendelea utatakiwa kulipa millioni tena'

Kwa ujumla migodi ya barrick hasa buzwagi na bulyanhulu imetapakaa rushwa,kazi inayohitaji mtu wa digrii utamkuta form four kigezo ni kwamba alitoa rushwa:Wanao husika hususani TAKUKURU tembeleeni maeneo hayo nendeni kijiji cha kakola,bugarama,ilogi na mwingiro halafu waulizeni wananchi suala hili watawaambia sababu ni jambo ambalo sasa limekuwa ni kama utamaduni..

Kama wapo humu wanaohusika waje wakanushe.
 
hili nalo neno,huenda kuna ukweli ngoja tuone wanaojua mambo watujuze,ila naamini sio barrick peke yao taasisi nyingi ndio mambo yako hivyo
 
Haya tena, ABG na mambo ya mlungula. Ila ni waswahili ndio wafanyayo hayo.Rushwa za ajira za ndani (Waswahili), Rushwa za ajira za ng'ambo (wazungu), Rushwa za miradi midogo (waswahili)Rushwa za miradi mikubwa (wazungu), Rushwa za Miners (Foremen, Superitendants, Dept Manager), Hii ndio African Barrick Gold bana.
 
Ni wawekezaji,ambao waliahidi kutoa fursa sawa za ajira kulingana na fani ya muombaji,lakini hali si shwari migodi ya barrick hasa buzwagi na bulyanhulu...rushwa iko wazi bila pesa kazi hazipo,wanatangaza magazetini kila kukicha lakini kwa uhalisia barrick wameendekeza rushwa sana,tumefika hapo,tumekaa hapo muda mrefu imefikia hatua mtu anakuambia ni kiasi gani cha pesa utatoa ili kupata nafasi fulani,mfano kama kazi ina mshahara wa laki 8 kwa mwezi utatakiwa kutoa rushwa ya million moja,na watakupa mkataba wa miezi sita,ukihitaji kuendelea utatakiwa kulipa millioni tena,kwa ujumla migodi ya barrick hasa buzwagi na bulyanhulu imetapakaa rushwa,kazi inayohitaji mtu wa digrii utamkuta form four kigezo ni kwamba alitoa rushwa:Wanao husika hususani TAKUKURU tembeleeni maeneo hayo nendeni kijiji cha kakola,bugarama,ilogi na mwingiro halafu waulizeni wananchi suala hili watawaambia sababu ni jambo ambalo sasa limekuwa ni kama utamaduni..kama wapo humu wanaohusika waje wakanushe.

Inaonekana wewe umekosa kazi ndio maana umekuja na accusations. Kama una ushahidi sema uliomba nafasi gani na ukakosa kwa sababu hukutoa rushwa, sio kutuaminisha kuwa kuna rushwa bila ushahidi. Unasema tukaulize watu wa Kakola, Ilogi na Bugarama, unafikiri hao wanakijiji wote wanajua mambo ya barrick bila hata wao kuomba kazi?

Kazi kutangazwa gazetini sio lazima wewe upate, hata walio ndani ya shirika nao wanatakiwa kuomba hiyo kazi kama itakuwa ni ya juu kulingana na current position aliyonayo huyo mtu, ikija kwenye interview kuna uwezekano akapewa internal candidate kwanza.

Toa ushahidi ulifanyiwa interview na nani, kazi gani, mlikuwa wangapi na akachaguliwa nani?
Mwisho hiyo mikataba unayosema miezi sitasita, unanifanya niamini kuwa hiyo ni casual labour ambayo ni miezi mitatu mitatu na wanaopewa priority ni wananchi wanaotoka maeneo ya jirani na migodi kupitia chama chao ambacho Barrick huwa haiwachunguzi maana walishakuwa mature enough kujiendesha, ndio maana umesema tuulize vijiji vya jirani na migodi.
 
Heri huko Barrick AFGEM zamani ikijulikana kama SAMAX inayochimba Tanzanite, Kabla hujapata wala nini lazima uandae kama M 5 hv, Wanasema ni ya supu ya wazee.

Hasira zetu tuzihifadhi kwa sasa na tuje tuzionyeshe 2015 coz nchi haitawaliki kwa sasa.
 
Hilo ni kweli kabisa, mi nafanya buly hali ni mbaya sana bila m no job. Ni wa bongo wenzetu hasa idara ya hr na mining training.
 
Inaonekana wewe umekosa kazi ndio maana umekuja na accusations. Kama una ushahidi sema uliomba nafasi gani na ukakosa kwa sababu hukutoa rushwa, sio kutuaminisha kuwa kuna rushwa bila ushahidi. Unasema tukaulize watu wa Kakola, Ilogi na Bugarama, unafikiri hao wanakijiji wote wanajua mambo ya barrick bila hata wao kuomba kazi?Kazi kutangazwa gazetini sio lazima wewe upate, hata walio ndani ya shirika nao wanatakiwa kuomba hiyo kazi kama itakuwa ni ya juu kulingana na current position aliyonayo huyo mtu, ikija kwenye interview kuna uwezekano akapewa internal candidate kwanza.Toa ushahidi ulifanyiwa interview na nani, kazi gani, mlikuwa wangapi na akachaguliwa nani?Mwisho hiyo mikataba unayosema miezi sitasita, unanifanya niamini kuwa hiyo ni casual labour ambayo ni miezi mitatu mitatu na wanaopewa priority ni wananchi wanaotoka maeneo ya jirani na migodi kupitia chama chao ambacho Barrick huwa haiwachunguzi maana walishakuwa mature enough kujiendesha, ndio maana umesema tuulize vijiji vya jirani na migodi.
Rushwa barrick ni ya hadharani hata waajiriwa wa kudumu wanaingia hivyo hivyo,si kweli kwamba mimi nilishaomba nikakosa that is why i have come up with this accusation, no hali ni mbaya barrick kulisema hapa siyo mpaka niwe nimeomba nikakosa,unabisha nini rushwa iko hadharani?vyombo vinavyohusika wafanye uchunguzi wa siri,mi niko tayari kuwasaidia na ninapatikana hapa hapa kahama
 
Nenda kwa human resource manager pale,ana vijana wake hata hujaongea naye lazima uache mzigo kwa vijana hawa,halafu watapeleka jina lako moja kwa moja,wewe ukisikia tangazo la kazi barrick nenda moja kwa moja na milioni waone hao vijana mmoja yupo ilogi halafu ndani ya siku tatu ulishatoka,pale training napo acha pesa mambo yanakwenda...halafu mtu anakuja kubisha hapa...wakazi wanaozunguka mgodi wana ofisi yao ya ibuka cooperative society,pale napo barrick wameshikilia bila laki tano hujapata kazi,msipende kubisha sisi tuna data na kila siku tunawaona tu
 
Huo uchunguzi wa siri ukifanywa anayechunguza akupate vipi? ili utoe ushahidi maana unaingia JF kwa ID, nakushauri kama una moyo wa kweli wa kupingana na udhalimu unaousema kuwa muwawazi, watu tufanye kazi yetu sio allegations sizizokuwa na tija.
Show evidences please!
 
Naijua vizuri Barick.unayoyasema ni ukweli mtupu.halafu kazi zinatolewa kwa ukabila na kujuana.huu ni mfumo umeanzia kwa wazungu wa kampuni hii ambao hupenda ajira zibaki kwa watu wanaowajua na ndugu zao na pia kupendelea cheap labour!
 
Kaka hata email za matangazo yao ya kazi huwa haziendi. Nilishtuma saa nzima cafe mpka jamaa akaniambia hizo email wameziblock hata yeye amempa barua mtu kwa mkono anayefanya kazi humo.this is stupid nadhani vyombo huska vinapaswa kuangalia hili. Wacha watu wapambane gpa plus skilss
 
Nenda kwa human resource manager pale,ana vijana wake hata hujaongea naye lazima uache mzigo kwa vijana hawa,halafu watapeleka jina lako moja kwa moja,wewe ukisikia tangazo la kazi barrick nenda moja kwa moja na milioni waone hao vijana mmoja yupo ilogi halafu ndani ya siku tatu ulishatoka,pale training napo acha pesa mambo yanakwenda...halafu mtu anakuja kubisha hapa...wakazi wanaozunguka mgodi wana ofisi yao ya ibuka cooperative society,pale napo barrick wameshikilia bila laki tano hujapata kazi,msipende kubisha sisi tuna data na kila siku tunawaona tu

I totally disagree with you that HR Manager has his guys, who works for him for malpractices purposes. Ninachoweza kusema ni kuwa kuna vijana wengi pale mitaani Kakola, Bugarama na Ilogi wanao tapeli watu kuwa watawapa kazi kupitia kwao. Hao watu kwa sababu ya kutaka kazi wanaingia mkenge, sasa aliyeliwa pesa yake anajua hiyo ni Barrick, which is not true.

Kuhusu chama cha IBUKA, kama nilivyosema awali ni chama kilichoanzishwa na wanakijiji wanaozunguka maeneo ya mgodi wa Bulyanhulu ili vijana wanao toka eneo hilo wapate ajira. Barrick ilichokifanya ni kuhakikisha kuwa chama kinapata viongozi wanakijiji watakao kiongoza, tokea muda mrefu chama kinajiendesha chenyewe na Barrick wakitaka kuajili kutoka kijijini wanawasiliana na viongozi wa IBUKA na viongozi wa IBUKA ndo wanaoleta watu kulingana na idadi waliyo ambiwa na Barrick. If there is any malpractices katika hicho chama that is not Barrick it is IBUKA, wanakijiji wanaopatwa na matatizo ya kuombwa rushwa watoe taarifa katika uongozi wa mgodi, ili uongozi ujue, maana unakuta mtu ametoa rushwa halafu anakaa kimya na badala yake anakuja kulalamika huku JF.

Lakini pia hiyo IBUKA ni kwa ajili ya wanakijiji wanaozunguka mgodi ila unakuta watu kutoka Kahama, Shinyanga, Mwanza, Kagera, Dar es salaam etc. ambao sio wakazi wa pale wanaenda kuomba kazi na hao ndo wanashawishi viongozi wa IBUKA kupokea rushwa.
 
Shangaa mtu anajiita mndebile humu JF anakana,let you be sometimes impartial kwa vitu vinavyokera watu,ni nani asiyejua uhuni wa barrick hasa human resource na training manager? We unakurupuka hapa sababu umo ndani humo,,ndugu yangu acha bias kwa vitu vinavyokera
 
Kaka hata email za matangazo yao ya kazi huwa haziendi. Nilishtuma saa nzima cafe mpka jamaa akaniambia hizo email wameziblock hata yeye amempa barua mtu kwa mkono anayefanya kazi humo.this is stupid nadhani vyombo huska vinapaswa kuangalia hili. Wacha watu wapambane gpa plus skilss
Kaka you dont have to bother youself sending your CV to barrick e-mails,they dont read emails and they have never taken online application seriousily,have a physical visit to bulyanhulu,there are people you can meet them near,pay a million and you will be sure of being employed:
 
Usihangaike na barricky wakati LUMWANA MINING tunatafuta wafanyakazi kila cku
 
Usihangaike na barricky wakati LUMWANA MINING tunatafuta wafanyakazi kila cku

Don't be silly when you talk of Lumwana Mining and Barrick what is the difference my dear, please let us know, You are really talking of the same thing with different names, like Buzwagi and Bulyanhulu they are mining companies under the same boss BARRICK stop.
 
Thieves
 
Shangaa mtu anajiita mndebile humu JF anakana,let you be sometimes impartial kwa vitu vinavyokera watu,ni nani asiyejua uhuni wa barrick hasa human resource na training manager? We unakurupuka hapa sababu umo ndani humo,,ndugu yangu acha bias kwa vitu vinavyokera

You have the right to speak according to your understanding, but for your information there is no employee at Buly who is holding the position of Training Manager. Therefore from that point I can conclude that you are alleging accusations which you can not prove.
 
Back
Top Bottom