Rushwa: Wanausalama barabarani na Krismass!

kisugujira

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
773
195
WanaJF,

Sasa hivi askari polisi wa usalama barabarani wametawanyika kila kona hapa jijini Dar es Salaam wakikamata magari hovyo kwa lengo la kujikusanyia pesa za Krismass kwa ajili ya matumizi ya familia zao na wakubwa zao! Tena cha kushangaza makundi ya askari hao wa usalama barabarani huongozana na wakaguzi wa magari (Vehicle Inspectors) ili zoezi zima la kukamata magari lionekane kuwa na uzito fulani!

Mfano mzuri wa hiki ninachokieleza katika uzi huu kipo barabara inayoingia Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na Mbagala ambapo kila siku wala rushwa hawa utawaona wakikamata magari na kupokea rushwa hadharani! Kama ni gari ya mauzo imekamatwa, iwe ya maji, sabuni, pipi, nk ikikamatwa na dereva akasema hana pesa, hulazimisha wapewe kitu fulani kati ya vitu vinavyouzwa!

Pia kutoka chanzo cha kuaminika pale Ubungo Bus Terminal, inasemekana wanausalama hawa wa barabarani wanahongwa pesa na wenye mabasi yanayokwenda mikoani ili wayaruhusu magari hayo kwa muda mrefu hasa saa za asubuhi na kusababisha msongamano mkubwa wa magari toka sehemu zingine na kuchangia wanaowahi kwenda maofisini kuchelewa!
 

Dengue

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
1,809
2,000
Wivu wa kike,kama vp nawe kawe Polisi. Kazi wanayofanya ngumu wacha wapate chochote kitu.
 

Makamee

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
2,020
1,250
Wivu wa kike,kama vp nawe kawe Polisi. Kazi wanayofanya ngumu wacha wapate chochote kitu.

Mbona unawaonea wanawake?
Wapate chochote kitu kwani hawalipwi mishahara?
Usihalalishe haramu
 

Gwangambo

JF-Expert Member
Jun 30, 2012
3,641
1,225
Toa rushwa mambo yako yaende, acha ubahili, utachina, nchi hii RUSHWA MBELE KAMA TAI, ndio maana naomba CCM iendelee kabaki madarakani ili mambo yaende. CCM OYEEEEE!!!!!!!
 

Dengue

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
1,809
2,000
Mbona unawaonea wanawake?
Wapate chochote kitu kwani hawalipwi mishahara?
Usihalalishe haramu

Mishahara ni midogo sana wanayoipata ukilinganisha na mazingira ya kazi.

Tanzania ilipofikia ni lazima haramu iwe halali na halali iwe haramu mambo yako yataenda vizuri.
 

Makamee

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
2,020
1,250
Mishahara ni midogo sana wanayoipata ukilinganisha na mazingira ya kazi.

Tanzania ilipofikia ni lazima haramu iwe halali na halali iwe haramu mambo yako yataenda vizuri.
Unavyodhani polisi ana maisha magumu kuliko mwalimu? Mbona walimu hawachukui rushwa?
Polisi ana mshahara pamoja na posho,je mwalimu anayo?
 

abdulazizi kingu

New Member
Jul 6, 2013
4
0
Yaaani mi ndo hata sisemi maana mvua zikiwazinanyesha wao wanaendelea na kazi hebu jiulize trafiki wa ubungo anakula vumbi kilo ngapi kwa siku usinijibu fikiri kisha tafakari chukua hatua ungefanyaje mi binafsi ningechukua maana pesa bhana!!!!!!
 

mpiga domo

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
838
1,000
hii kitu imenitokea pia mimi leo arusha..wanausalama barabaran walikuwa wamemwaga katika kila barabara wanakamata magari kama hawana akili nzuri
 

Mkira

JF-Expert Member
May 10, 2006
425
195
Hebu utaje mshahara
polisi
nesi
tra
mwalimu wa shule ya msingi
mwalimu wa secondary
ili tujue kama ni kweli


Yaani Leo hapo surrender bridge wamekuwa Wakali sana. Cha ajabu wanatisha HATA kulaza mtu ndani Kumbe wanachotaka NI hela! Nimewapatia elfu kumi nikaaondoka kosa lilikuwa dogo cha ajabu wakanitisha kuniweka ndani!!! Hebu Jiulize ikitokea mtu akawa hana hela Si atanyanyaswa na kufungiwa ndani?????? NI bora. Akusimamishe na kukuomba hela in a friendly manner nitampatia!

vitisho vya nini? Shame on you police, acheni ukali na kukuza makosa Kumbe unataka hela!!! Shame on you!!
 

paul milya

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
285
195
Hawa jamaa barabarani tangu mwezi wa kumi na moja katikati wameanza utaratibu wao mbaya sana kana kwamba kama una hasira unaweza ukajikuta umejibizana nao vibaya kbs.
Wanakukagua wanakuta una kila ki2 lakini hawakubali,ni mpaka wahakikishe umewatoa tu.
 

Dengue

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
1,809
2,000
Hebu utaje mshahara
polisi
nesi
tra
mwalimu wa shule ya msingi
mwalimu wa secondary
ili tujue kama ni kweli

Ninapozungumzia polisi sizungumzii ngazi ya akina kova bali ni wale makonstebo na ninapozungumzia mwl sio mwl mkuu ni yule ambaye hana hata kitengo kama cha taaluma
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom