Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,602
- 830,350
Ifike mahali tusionekane wapingaji na wakosoaji wa kila kitu,! Jamani tuna hoja tusikilizwe! Tutapongeza panapostahili, tutakosoa penye mushkeli.... Tunajenga boma moja hatuna haja ya kufanyiana hujuma.
Ukweli mchungu ni kwamba hali ni mbaya taasisi za serikali hasa zile zinazohusika na wananchi moja kwa moja, kuna taasisi zimesahauliwa na nyingine kukumbukwa sana TRA ARDHI na MIUNDOMBINU pengine huku ndio kumewekewa jicho kali sana.
Lakini huku kwengine hali ni mbaya sana. Jeshi la polisi na vitengo vyake vyote , huduma za afya, serikali za mitaa, elimu hakufai hakufai hakufai.... Trafiki barabarani utadhani wamepewa kibali rasmi, huko kwenye vituo vya polisi magereza, idara za mahakama unaambiwa live kabisa ni ama A au B! La usipoambiwa itabidi tu ujiongeze.
Huduma za afya kwenye hospital na vituo vya afya vya serikali huduma zimezidi kuwa mbovu, uzembe ndio usiseme, rushwa ndio kama imezaliwa upya! Yako wapi yale MADUKA YA DAWA YA SERIKALI? Yameishia wapi yale???? wananchi wanaumizwa huko jamani.
Wafanyakazi hawana morali wa kazi tena! Hawana hakika na kesho yao hakuna kupandishwa madaraja, na kila uchao ni uhakiki usiokoma NI VEMA HILI JAMBO LIKAWA NA TIME FRAME ili watu waweze kuwa na uhakika na ajira zao.
Tusidili na mambo makubwa tu huku kwenye msingi mambo yanaharibika na nchi inapata aibu kubwa hasa kwa wageni trafiki wanaongoza hasa tangu road license iondolewe... Shame shame shame on them.. Rushwa ya kulazimisha mpaka buku! Tena anaombwa mgeni.
Vijana wa usalama waluojazwa kwingine wapelekwe na huko nilikotaja na wakafanye kazi kwa weledi, tutaona maajabu lakini kwa sasa hali ni mbaya