Rushwa imekithiri kwa Trafiki eneo la St. Peters Oysterbay

Bururu

JF-Expert Member
May 21, 2016
877
584
Jaman Watanzania TRAFIC WA PALE SANT PETER CHURCH wanataka Rushwa kwa lazima na chini ya elfu 20 wanakataa,Wanalazimisha makosa hasa Trafic Salom.Ni kero na ni mradi kwa hawa watu tunaomba wachunguzwe.WAMEJIFICHA NYUMA YYA MITI.Wanakuvizia na ujisimamishwa Utalazimishwa josa lolote kwenye gari.
 
Kwani mkuu ungetulia tu vizuri ukaandika uzi wako vizuri ungekuwaje?

Au washakupa ka twenty na wewe?

pole mkuu hii ndo bongo dsm
 
Wahusika tengenezeni mtego ,muwakamate hawa watu wanazidi xana utazani hawalipwi mishahara,
 
Hakuna watu wametiwa viburi na Magufuri km Traffic kiukweli siwapendi wanalazimisha makosa
 
Labda niseme ukweli tu.. Traffic Police wanapunguza sana kura za ccm..yaani sasa hivi wanalazimisha makosa ambayo hayapo
 
Na kwanini mnawapatia hizo pesa na kuja kulalamika hapa.

Mnajua mnamakosa na ndio maana mnawapa pesa zenu, nyie ndio mjilaumu.

Wanachi kwenye mengi nyie ndio vyanzo vya kuendeleza hayo ya rushwa, wengi nyie ndio mnawabembeleza wachukue pesa ili wasiwapeleke mbali na makosa mnayofanya hata kushtakiwa.

Muanze kwa kuacha kutoa hizo pesa.

Kama wamewaomba wao kwanza basi nendeni mkaripoti kituo cha polisi au kupiga namba zilizotolewa za wakubwa wao. Utakuwa umejisimamia kwa kuonewa bila kuwa na wasiwasi wowote.
 
Baba yao alisema muwape hela ya kubrashi viatu mlijua kamaanisha nini ile ni zaidi ya TRA sikuizi wanakusanya kodi.
Mkuu kachukue hela za Takukuru uwachome nazo
 
Mimi hua nashangaa sana Watu wanaosema Magufuli amepunza rushwa. Rushwa ndio imeongezeka hasa Trafiki.
Trafiki wa Kahama wanakusanya rushwa hakuna mfano wake.
 
Trafic Salom! hahahaha , uwe mwangalifu, usiwe na sababu ya kuwafanya wakuombe rushwa!
 
Sheria Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa Namba 11 Ya 2007 Kupokea/Kutoa Rushwa Ni Kosa Ila Sasa Kwa Ndg Sizonje Kaja Kuitegua Kwa Maneno Kuwa 5000/- Pesa Ya Kubrash Viatu Hapo Ndiyo Alipokosea Sana

Alisema Anataka Kuhakikisha Anapambana Na Rushwa Kubwa Sana Ila Said Lugumi Kateleza Yaani Kaangukia Kwenye 5000/-
 
Hao trafiki wapunguzwe huko barabarani, hakuna cha maana wanachofanya zaidi ya kujikusanyia rushwa. Waongezwe kwenye doria, wasifurahie rushwa za barabarani wakati wenzao wanapoteza maisha kwenye majukumu ya msingi ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
 
Jaman Watanzania TRAFIC WA PALE SANT PETER CHURCH wanataka Rushwa kwa lazima na chini ya elfu 20 wanakataa,Wanalazimisha makosa hasa Trafic Salom.Ni kero na ni mradi kwa hawa watu tunaomba wachunguzwe.WAMEJIFICHA NYUMA YYA MITI.Wanakuvizia na ujisimamishwa Utalazimishwa josa lolote kwenye gari.
Hii issue ni Tanzania nzima
Ukitaka kujua rushwa ilivyo rohoni mwa Trafic fika Arusha. Wakikuomba kadi ya gari hapo hapo wanakutishia nakuandikia makosa mawili bila kukagua gari wala leseni. Hii ni janja ili utoe rushwa haraka.
Cha kushangaza viongozi wa juu wa polisi wanafahamu hii hali lakini wameziba masikio. Polisi trafiki wamekuwa kero.
 
Na kwanini mnawapatia hizo pesa na kuja kulalamika hapa.

Mnajua mnamakosa na ndio maana mnawapa pesa zenu, nyie ndio mjilaumu.

Wanachi kwenye mengi nyie ndio vyanzo vya kuendeleza hayo ya rushwa, wengi nyie ndio mnawabembeleza wachukue pesa ili wasiwapeleke mbali na makosa mnayofanya hata kushtakiwa.

Muanze kwa kuacha kutoa hizo pesa.

Kama wamewaomba wao kwanza basi nendeni mkaripoti kituo cha polisi au kupiga namba zilizotolewa za wakubwa wao. Utakuwa umejisimamia kwa kuonewa bila kuwa na wasiwasi wowote.
ungekuwa hata na bodaboda usingeandika hili povu,kaa kimya wanaume wenye magari wachangie
 
Na kwanini mnawapatia hizo pesa na kuja kulalamika hapa.

Mnajua mnamakosa na ndio maana mnawapa pesa zenu, nyie ndio mjilaumu.

Wanachi kwenye mengi nyie ndio vyanzo vya kuendeleza hayo ya rushwa, wengi nyie ndio mnawabembeleza wachukue pesa ili wasiwapeleke mbali na makosa mnayofanya hata kushtakiwa.

Muanze kwa kuacha kutoa hizo pesa.

Kama wamewaomba wao kwanza basi nendeni mkaripoti kituo cha polisi au kupiga namba zilizotolewa za wakubwa wao. Utakuwa umejisimamia kwa kuonewa bila kuwa na wasiwasi wowote.
Kwa mara ya kwanza nakuunga mkono uko sahihi.
 
Back
Top Bottom