Rushwa Bungeni: Mbatia sasa atishia kuwataja wakati wowote

Kwa wabunge waliotajwa ni Akina sendeka, Sarah msafiri, mumbwe na kwa upinzani walisema eti watampa kafulila
 
Rushwa bungeni moto
• Mbatia sasa atishia kuwataja wakati wowote

na Edson Kamukara, Dodoma
Tanzania Daima



SAKATA la wabunge kuhongwa kwa nia ya kuyatetea makampuni ya mafuta na menejimenti ya Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) linazidi kuchukua sura mpya kadiri siku zinavyosonga mbele.

Siku moja baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kuvurumisha makombora dhidi ya wabunge hao pasipo kuwataja kwa majina, Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, ameibuka na jipya kuhusu sekeseke hilo.
Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi amesema wakati wowote kuanzia sasa atawataja kwa majina wabunge wote waliopokea rushwa kwa lengo la kuwalinda viongozi wakuu wa TANESCO wanaokabiliwa na tuhuma za kulihujumu shirika hilo.

Mbali ya hilo, Mbatia amemshutumu Spika wa Bunge, Anne Makinda, kwa kuwalinda wabunge hao aliodai wamehongwa na mafisadi hao wa TANESCO.
Kauli hiyo aliitoa jana mkoani hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Spika Makinda kuridhia kuivunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na kuiagiza Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwachunguza watuhumiwa.

Mbatia alisema Spika anao ushahidi wa kutosha wa majina ya wabunge waliohongwa kwani Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliliambia Bunge kuwa wana ushahidi wote.
Alibainisha kuwa ushahidi huo ndiyo uliomfanya Spika Makinda akaridhia kuivunja kamati husika na kuipa kazi Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwachunguza watuhumiwa.
Kiongozi huyo pia alisema hawana imani na kamati iliyopewa jukumu la kuwachunguza wabunge watuhumiwa wa rushwa kwa sababu inaundwa na baadhi ya watuhumiwa.

“Tunamtaka Spika ajitakase kwanza kwa kuwaengua wajumbe ambao ni watuhumiwa, kinyume na hapo hatuna imani na kamati hiyo,” alisema.
Alisema Bunge ni chombo kitukufu na ili utukufu huo uonekane ni lazima maamuzi yanayofanywa huko yaheshimiwe, hivyo akapendekeza kuwa mbali na Bunge kutumia kanuni zake kuwahukumu wabunge watuhumiwa au linaweza kuiga maamuzi ya baadhi ya mabunge ya Jumuiya ya Madola.

Alitolea mfano mabunge ya Uingereza na India, ambapo Bunge la Uingereza limewahi kuwatimua na kuwavua ubunge wabunge 57 na India imefanya hivyo kwa wabunge 11 kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

“Hivyo basi tunatoa wito kuwa mbunge yeyote wa chama chochote anayeamini kwa dhamira yake kwamba ni mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini na anafanya biashara na TANESCO kwa njia ya maslahi binafsi halafu anatumia rushwa kuwashawishi wabunge wengine au amepokea rushwa kutetea uovu ni bora akajiondoa mwenyewe kwenye ubunge kabla ya kuabishwa na Bunge,” alisema.

Mbatia aliongeza kuwa wanamtaka Spika awe amewataja kwa majina wabunge waliopokea rushwa si zaidi ya wiki moja ili Bunge liwachukulie hatua, huku akiwaomba wabunge wenzake bila kujali itikadi za vyama vyao wafanye azimio la Bunge ili wahusika mbali na kuvuliwa ubunge wafungwe jela miaka mitano.

“Kwa mujibu wa sheria namba 3 kifungu cha 32 ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ya mwaka 1988, mbunge anakatazwa kuzungumza, kuhoji, kupiga kura au kutetea jambo lolote bungeni ambalo litakuwa na ushawishi wa maslahi yake binafsi kutoka nje na kwamba adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka mitano jela,” alisema Mbatia.

Mwenyekiti huyo ambaye alifuatana na mbunge mwingine wa chama hicho wa Kasulu Mjini, Moses Machali, alimtaka Spika kuzitaja kamati nyingine ambazo wajumbe wake wanatuhumiwa kwa rushwa.

Mbali na Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa, kamati nyingine zinazodaiwa baadhi ya wabunge wake kujihusisha na vitendo vya rushwa ni ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) chini ya Zitto Kabwe na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Augustine Mrema.

Nyingine ni ya Miundombinu chini ya Peter Serukamba, Viwanda na Biashara ya Mahmoud Mgimwa na Ardhi, Maliasili na Mazingira chini ya James Lembeli.

“Tatizo la nchi yetu ni kuchelewa kufanya maamuzi wakati muafaka.
Tukilitakasa Bunge kwa kuwashughulikia wabunge waliokula rushwa ni wazi hata serikali itaanza kuwachukulia hatua wale ambao tumekuwa tukiwalalamikia kujihusisha na rushwa,”

Mbatia aliwatahadharisha wabunge wa chama chake kuwa kama kuna yeyote aliyechukua rushwa katika sakata hilo, ajiengue mapema.

Mbatia pia alitumia mwanya huo kuwatia matumaini wabunge waadilifu wenye misimamo mikali ya kuikosoa serikali kuwa wasiogopeshwe na sakata hilo ambalo alidai serikali italitumia kuwanyamazisha wabunge kwa vile walikuwa wakiikosoa.

Ingawa Mbatia hakuwataja kwa majina wabunge hao, habari ambazo Tanzania Daima inazo zinaeleza kuwa wabunge zaidi ya sita wanatajwa kuwa katika kundi la wale wanaotuhumiwa kuwatetea mafisadi wa TANESCO.

Inadaiwa wabunge hao walipewa fedha na kampuni za mafuta ili washinikize kung’olewa kwa Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliakim Maswi wanaodaiwa kuipa zabuni ya kusambaza mafuta kwa TANESCO kampuni ya Puma Energy.

Habari zinaeleza kuwa, wabunge hao wako katika Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Kamati ya Miundombinu, Kamati ya Viwanda na Biashara na Ardhi, Maliasili na Mazingira.

Gazeti hili limedokezwa kwamba wabunge takriban wote isipokuwa mmoja tu, walioko katika orodha hiyo wanatokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).



Tiss wazalendo tuwekeen majina hapa
 
Gazeti hili limedokezwa kwamba wabunge takriban wote isipokuwa mmoja tu, walioko katika orodha hiyo wanatokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Mmmh! Hapo sasa mbona balaa jamani?

Huo sasa unafiki,
Limetokeza wapi? kwa nini halijawataja? Inaoneakna wewe hata hausikilizi bunge, ungewasikiliza akina SELASINI usingeleta mapenzi yako hapa jamvini.
 
Gazeti hili limedokezwa kwamba wabunge takriban wote isipokuwa mmoja tu, walioko katika orodha hiyo wanatokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Mmmh! Hapo sasa mbona balaa jamani?

huyu wa upinzani ni kitu maalumu, atakuwa yule muuza matairi. CHADEMA waonyeshe mfano wakati ni huu kwani haina madhara kwao kwa kuwa ni kitu maalumu. CCM kazi wanayo.
 
Nadhani kamati ya zitto itakuwa inanuka rushwa kubwakubwa si mnaona hammmers
 
Wataje wabunge wote waliowahi kuchukua rushwa toka enzi za ngeleja ndo itakuwa vizuri zaidi
 
Hadithi hadithi,hakuna chochote hapo,nani atathubutu kumnyooshea kidole mwenzake wakati wote wachafu?hapo maigizo tu,mmoja akimwaga ugali mwingine anamwaga mbonga'wa Tz tusijipe matumaini hapo hakuna lolote la maana yaani ukisikia sehem ya wasanii kwa Tz hakuna kama bungeni,tunapoteza muda sana kukaa kusikiliza bunge,hizo pesa za posho zao bora zingefanya kazi nyingine,hawa wabunge hawana history yakusaidia nchi hii na hawa ndio wanaotuongezea umaskini tu,
 
Siku moja baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kuvurumisha makombora dhidi ya wabunge hao pasipo kuwataja kwa majina, Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, ameibuka na jipya kuhusu sekeseke hilo.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi amesema wakati wowote kuanzia sasa atawataja kwa majina wabunge wote waliopokea rushwa kwa lengo la kuwalinda viongozi wakuu wa TANESCO wanaokabiliwa na tuhuma za kulihujumu shirika hilo.
Mbali ya hilo, Mbatia amemshutumu Spika wa Bunge, Anne Makinda, kwa kuwalinda wabunge hao aliodai wamehongwa na mafisadi hao wa TANESCO.

My Take.

Mbunge wa Viti Maalumu naye kwa Mbwembwe
 
hana lolote huyo kibaraka nae,anatishia nini sasa,kama kweli hajapewa zawadi ya hicho kiyi maalum basi ataja mapema.
 
Haya sie tuna kiu yakuwajua majina yao,asijekua anatishia wenzie nyau.
 
Bramo, Humtendei haki mheshimiwa Mbatia kumwiti mbunge wa viti maalumu. Mbatia ni mbunge wa kuteuliwa na rais kwa Misingi ya katiba ya nchi, kama alivyomteua Profesor Muhongo. Naona kila wakati tunadhihaki sana na kumvujia haki yake aliyopewa na rais kama wengine aliowateua.
 
Walishapoteza uzalendo hawa siku nyingi tu ndio maana wanaitwa usalama wa mafisadi...Wangekuwa bado wana uzalendo nchi isingekuwa imejaa madudu ya kutisha. Ufisadi kila kukicha, waheshimiwa kulambishana sumu, na wengine wakiwa na wasiwasi na uhai wao baada ya kupokea vitisho na hata kutekwa kwa Dr Ulimboka kwa kudai haki za Madakatari na kuboresha sekta ya afya nchini kusingetokea. Angalia hadi leo wako kimya kuanika hadharani majina ya mafisadi ndani ya Serikali waliokutwa na $200 millioni kwenyr bank accounts zao kule Switzerland. Wanafanya kazi kwa "weledi" katika kulinda maslahi ya mafisadi.

Tiss wazalendo tuwekeen majina hapa
 
House Ethics team also eating at Tanesco - MP
Monday, 30 July 2012 08:20

By Florence Mugarula, The Citizen Reporter
Dodoma

Who will bell the cat? That must be the big question now in Dodoma, for Parliament is faced with the unenviable task of dealing with the very committee that it had assigned to probe corruption within its ranks. Why, the probe committee has also been accused of corruption.

On Saturday the Speaker of the National Assembly, Ms Anne Makinda, dissolved the Parliamentary Committee on Energy and Minerals and ordered the conduct of some of its members be probed by the committee for Privileges, Ethics, and Powers (PEP).

But yesterday Mr James Mbatia (NCCR-Mageuzi) added a twist to the saga when he claimed that some members of the Privileges, Ethics, and Powers Committee, were also among those who have been taking bribes, the same vice that brought down the Energy committee.

Mr Mbatia said that if the investigation into the Energy committee's alleged vices is to be meaningful, some PEP members should also step down and be subjected to scrutiny as well.
"My party is not ready to see PEP investigate the matter before suspending some of its members who have also been named as corrupt. There is a need for the committee to clean itself first before it embarks on investigating the rot in the Energy and Minerals committee.

"We have evidence that some members of the Parliamentary Committee for Privileges, Ethics and Powers are among lawmakers who have business interests with Tanesco and are linked to the dirt in the power firm and therefore we cannot have faith in its findings until the suspects amongst them are removed," insisted Mr Mbatia.

Commenting on the Speaker's decision to dissolve the Energy committee, Mr Mbatia said he doesn't see why there should be concealment of the names of suspect MPs and other committees that are linked with graft at Tanesco.
Meanwhile, Mr Mbatia said the shake-up should not end with the Energy committee since, he alleged, there were about six others that are accused of teaming with Tanesco and some private oil companies to sabotage the government.

"We are aware that there are more parliamentary committees involved in this scam, we want the Speaker to dissolve them all so that we can have a fresh start," said Mr Mbatia.

Mr Mbatia, who doubles as NCCR-Mageuzi national chairman, said all MPs linked to the rot should not wait to be named in the Parliament.
"They should resign their posts... We have several examples from UK and India where MPs resigned after they were named in certain scams; in this House during Pius Msekwa's tenure as Speaker, four CUF legislators were forced to go after they were found guilty of forging passports and marriage certificates for some Somali women," recalled Mr Mbatia.

The nominated MP wanted the Parliament to take legal measures against the accused lawmakers by using the Parliamentary Powers, Privileges and Immunities Act of 1988, which requires an MP convicted of corruption to be jailed for five years and be removed from his or her post. On the other hand, the former chairman for the dissolved Energy and Minerals Committee, Mr Jumanne Zedi, said he was shocked by the Speaker's move and that his committee would fully cooperate with the investigating committee.

Mr Zedi told The Citizen that the he was confident the investigation would reveal the truth behind the matter.
"I was shocked by the Speaker's decision to dissolve my committee, but we welcome the idea to have the Ethics committee investigate us and publish their findings," said Mr Zedi.

Another committee member, Mr David Silinde (Mbozi West-Chadema) hailed the decision, saying it was for the benefit of the Parliament and the entire country that tainted lawmakers be investigated and penalised if found guilty. He said it was better that the issue has been handed over to the PEP for as there were a number of controversies that need to be cleared.
According to Mr Silinde, the committee's opinion, which was presented last Friday during the tabling of the Energy ministry's budget, was not the same as issues that were discussed and agreed by the MPs when they were debating the budget.

"I support the dissolution of our committee; I think the investigation will clear the air. I was shocked to see the committee's opinion presented in the Parliament with additional comments that had not been discussed during our meetings," said Mr Silinde.

For his part, Mr Moses Machali (Kasulu Urban, NCCR-Mageuzi) said the Speaker's decision to dissolve the Energy committee would go a long way in cleansing the House tainted with graft allegations and other forms of misconduct.

He demanded that the Speaker names the suspects. Failure to that, he charged, after seven days he would move a private member's motion seeking the Parliament to suspend other activities so as to discuss the issue in depth.

On the other hand, Mr Luhaga Mpina (Kisesa - CCM) also commended the Speaker's decision saying the measure would help in regaining the Parliament's tattered image.

He said there was no way the Speaker could avoid taking such a decision given the circumstances. "It is very difficult to supervise people who do not trust your integrity, the committee lost legitimacy after some of its members were accused of pocketing bribes from Tanesco and some businessmen; there was no way it could continue to operate."
after the revelation," said Mr Mpina.

 
Back
Top Bottom