Rushwa Bungeni: Mbatia sasa atishia kuwataja wakati wowote

Mimi mwenyewe natamani hiyo list ibandikwe hapa jamvini ili watu tuandae magereza ya hawa waheshimiwa! Naimani hapa ndiyo itakuwa turning point ya rushwa kama spika atakuwa makini kutusaidia watanzania. Lakini akiendekeza uchama na ubabe wake pamoja na kutumia remote controller ya Lukuvi basi tutegemee hakuna jipya. lakini cha mhimu ni kujipanga kujenga hoja hadi hao wabunge watimuliwe na kuingizwa jela. May GOD help this time to provide a demo!!

Taarifa zinaonesha wawili kati yao ni wa cdm. Napendekeza chama kiwataje hao wawili ili kijisafishe na sisi wakereketwa tuondoe fikra au gueswork kuwa huenda ni Mnyika.....au Zitto......Selasini......nk.
 
Nlipata kuskia kuwa Kafulila naye ametajwa. Isije ikawa Mbatia anataka kutumia mwanya huo kumfukuzisha Kafulila mjengoni.

Huku ni kudogodesha hoja ambayo ni ya msingi sana. Kafulila alikuwa ni mlalamikaji wa jinsi kamati yake ya Serikali za Mitaa ilivyokuwa inahongwa na wakurugenzi wa halamashauri za wilaya, manispaa na majiji.

Kwa ujumla wabunge hawa ni mawakala wa mafisadi ambao waligawana Kamati hizi kwa ajili ya kuwashughulikia mawaziri wanaowaona kwamba ni tishio katika mustakabali wao wa kifisadi. Wamejipanga kuwashughulikia mawaziri wa Nishati, Mawasiliano, Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Maliasili na Utalii na Maji.

Wabunge hawa sasa wanajipanga kuzua uongo wakati bajeti ya Mambo ya Nje itakapowasilisha bajeti yake tarehe 6 August. Ndiyo hawa hawa ambao walifanya misafara ya nje ya nchi na kuchonga madili na kuwatishia mabalozi wakitaka nyaraka ambazo watazitumia kujenga hoja za kuipiga chini bajeti hiyo. Wengine ni wale walikwenda kujiuza Morocco.
 
Back
Top Bottom