Rushwa Bungeni: Mbatia sasa atishia kuwataja wakati wowote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rushwa Bungeni: Mbatia sasa atishia kuwataja wakati wowote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 30, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,701
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Rushwa bungeni moto
  • Mbatia sasa atishia kuwataja wakati wowote

  na Edson Kamukara, Dodoma
  Tanzania Daima  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]SAKATA la wabunge kuhongwa kwa nia ya kuyatetea makampuni ya mafuta na menejimenti ya Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO) linazidi kuchukua sura mpya kadiri siku zinavyosonga mbele.

  Siku moja baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kuvurumisha makombora dhidi ya wabunge hao pasipo kuwataja kwa majina, Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, ameibuka na jipya kuhusu sekeseke hilo.
  Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi amesema wakati wowote kuanzia sasa atawataja kwa majina wabunge wote waliopokea rushwa kwa lengo la kuwalinda viongozi wakuu wa TANESCO wanaokabiliwa na tuhuma za kulihujumu shirika hilo.

  Mbali ya hilo, Mbatia amemshutumu Spika wa Bunge, Anne Makinda, kwa kuwalinda wabunge hao aliodai wamehongwa na mafisadi hao wa TANESCO.
  Kauli hiyo aliitoa jana mkoani hapa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Spika Makinda kuridhia kuivunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na kuiagiza Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwachunguza watuhumiwa.

  Mbatia alisema Spika anao ushahidi wa kutosha wa majina ya wabunge waliohongwa kwani Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliliambia Bunge kuwa wana ushahidi wote.
  Alibainisha kuwa ushahidi huo ndiyo uliomfanya Spika Makinda akaridhia kuivunja kamati husika na kuipa kazi Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge kuwachunguza watuhumiwa.
  Kiongozi huyo pia alisema hawana imani na kamati iliyopewa jukumu la kuwachunguza wabunge watuhumiwa wa rushwa kwa sababu inaundwa na baadhi ya watuhumiwa.

  “Tunamtaka Spika ajitakase kwanza kwa kuwaengua wajumbe ambao ni watuhumiwa, kinyume na hapo hatuna imani na kamati hiyo,” alisema.
  Alisema Bunge ni chombo kitukufu na ili utukufu huo uonekane ni lazima maamuzi yanayofanywa huko yaheshimiwe, hivyo akapendekeza kuwa mbali na Bunge kutumia kanuni zake kuwahukumu wabunge watuhumiwa au linaweza kuiga maamuzi ya baadhi ya mabunge ya Jumuiya ya Madola.

  Alitolea mfano mabunge ya Uingereza na India, ambapo Bunge la Uingereza limewahi kuwatimua na kuwavua ubunge wabunge 57 na India imefanya hivyo kwa wabunge 11 kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

  “Hivyo basi tunatoa wito kuwa mbunge yeyote wa chama chochote anayeamini kwa dhamira yake kwamba ni mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini na anafanya biashara na TANESCO kwa njia ya maslahi binafsi halafu anatumia rushwa kuwashawishi wabunge wengine au amepokea rushwa kutetea uovu ni bora akajiondoa mwenyewe kwenye ubunge kabla ya kuabishwa na Bunge,” alisema.

  Mbatia aliongeza kuwa wanamtaka Spika awe amewataja kwa majina wabunge waliopokea rushwa si zaidi ya wiki moja ili Bunge liwachukulie hatua, huku akiwaomba wabunge wenzake bila kujali itikadi za vyama vyao wafanye azimio la Bunge ili wahusika mbali na kuvuliwa ubunge wafungwe jela miaka mitano.

  “Kwa mujibu wa sheria namba 3 kifungu cha 32 ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ya mwaka 1988, mbunge anakatazwa kuzungumza, kuhoji, kupiga kura au kutetea jambo lolote bungeni ambalo litakuwa na ushawishi wa maslahi yake binafsi kutoka nje na kwamba adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka mitano jela,” alisema Mbatia.

  Mwenyekiti huyo ambaye alifuatana na mbunge mwingine wa chama hicho wa Kasulu Mjini, Moses Machali, alimtaka Spika kuzitaja kamati nyingine ambazo wajumbe wake wanatuhumiwa kwa rushwa.

  Mbali na Kamati ya Nishati na Madini iliyovunjwa, kamati nyingine zinazodaiwa baadhi ya wabunge wake kujihusisha na vitendo vya rushwa ni ile ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) chini ya Zitto Kabwe na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) inayoongozwa na Augustine Mrema.

  Nyingine ni ya Miundombinu chini ya Peter Serukamba, Viwanda na Biashara ya Mahmoud Mgimwa na Ardhi, Maliasili na Mazingira chini ya James Lembeli.

  “Tatizo la nchi yetu ni kuchelewa kufanya maamuzi wakati muafaka.
  Tukilitakasa Bunge kwa kuwashughulikia wabunge waliokula rushwa ni wazi hata serikali itaanza kuwachukulia hatua wale ambao tumekuwa tukiwalalamikia kujihusisha na rushwa,”

  Mbatia aliwatahadharisha wabunge wa chama chake kuwa kama kuna yeyote aliyechukua rushwa katika sakata hilo, ajiengue mapema.

  Mbatia pia alitumia mwanya huo kuwatia matumaini wabunge waadilifu wenye misimamo mikali ya kuikosoa serikali kuwa wasiogopeshwe na sakata hilo ambalo alidai serikali italitumia kuwanyamazisha wabunge kwa vile walikuwa wakiikosoa.

  Ingawa Mbatia hakuwataja kwa majina wabunge hao, habari ambazo Tanzania Daima inazo zinaeleza kuwa wabunge zaidi ya sita wanatajwa kuwa katika kundi la wale wanaotuhumiwa kuwatetea mafisadi wa TANESCO.

  Inadaiwa wabunge hao walipewa fedha na kampuni za mafuta ili washinikize kung’olewa kwa Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliakim Maswi wanaodaiwa kuipa zabuni ya kusambaza mafuta kwa TANESCO kampuni ya Puma Energy.

  Habari zinaeleza kuwa, wabunge hao wako katika Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Kamati ya Miundombinu, Kamati ya Viwanda na Biashara na Ardhi, Maliasili na Mazingira.

  Gazeti hili limedokezwa kwamba wabunge takriban wote isipokuwa mmoja tu, walioko katika orodha hiyo wanatokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ngoma inogile. i hope this time somo la uwajibikaji watakuwa wamelielewa vyema na kilichobaki ni utekelezaji tu
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,701
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  Watu matumbo joto na wale waliochukuwa rushwa mwaka jana katika kikao cha bajeti ya 2011/2012 na kusababisha katibu mkuu wa Nishati na Madini Jairo kumwaga unga pia majina yao yaanikwe hadharani. Hawa hawastahili kuingia mjengoni kwa kuwa walichoweka mbele ni maslahi yao binafsi badala ya yale ya nchi.

   
 4. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Gazeti hili limedokezwa kwamba wabunge takriban wote isipokuwa mmoja tu, walioko katika orodha hiyo wanatokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  Mmmh! Hapo sasa mbona balaa jamani?
   
 5. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Nlipata kuskia kuwa Kafulila naye ametajwa. Isije ikawa Mbatia anataka kutumia mwanya huo kumfukuzisha Kafulila mjengoni.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,701
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  Tusubiri tuone kitakachojiri maana inaelekea ana ushahidi wa uhakika kuhusu hao wapokea rushwa, vinginevyo asingetoa kauli kama hii hadharani.

   
 7. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Asisahau kujitaja yeye mwenyewe na rushwa ya kameruni aliyotoa kwa mkuu wa kaya iliapewe viti maalumu.
   
 8. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Sakata limeiva kisawasawa. Mimi napendekeza uchunguzi urudi mpaka mwaka jana alipoondolewa Jairo kwani inasemekana zile fedha ziligawanywa kwa baadhi ya wabunge.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,701
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  Inabidi iwe hivyo, vinginevyo ni usanii tu. Je, magamba itakuwa tayari kuwapandisha kizimbani Wabunge wa magamba waliohusika na kupokea rushwa? Je, itakuwa tayari kuwatosa ili kukisafisha chama chao?

  Kumbuka swala la kujivua gamba liliwashinda vibaya sana wakaanza kuleta usanii wa hali ya juu. Je, hili la kuwatosa Wabunge wa magamba waliopokea rushwa na hivyo kupoteza hadhi ya kuwepo mjengoni, magamba wataliweza?


   
 10. Mdakuzi

  Mdakuzi JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,748
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Awataje tu kama anawajua...
  Asilete zile kung fu za kupiga upepo badala ya kumfuata adui aliko ampige za kweli!
  Alishatufanyia sana Pinda hizo, halafu tukakaa mkao wa kusubiri, lakini mwisho wake watu wakarudishwa ofisini kwa kusukumwa magari yao!
   
 11. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  alikua wapi siku zote kuwataja hadi leo kama alikua anajua what happened?
   
 12. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Siasa za kuviziana hizo. Wanatafuta kumkaanga mbaya wao baada ya jaribio la awali kugonga mwamba mbele ya mahakama.
   
 13. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mi naona wakati wa kutishia umeisha, Huyo Mbatia ua mtu yeyote anayewajua hao Wabunge wala rushwa angewataja tuu kama hawajui basi anyamaze.
   
 14. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Awataje, asiwataje itasaidia nini? Slaa aliwataja mafisadi miaka ilee, lakini hakuna cha maana kilichofuata, badala yake mafisadi wameongezeka. Bila mapinduzi ufisadi utaendelea kukua
   
 15. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Just go ballistic and name names, Why WAIT?
   
 16. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mbatia analeta zile za "nipige uone!"

  Kwa nini usubiri upigwe ndiyo uonyeshe?

  Zoza!
   
 17. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watajwe tu, kwani kuna woga gani jamani!!

  Wengine mnatuweka roho juu.

  Hofu yangu ni endapo mbunge wa cdm atakuwa kahusika basi patakuwa hapatoshi.

  Kama anajijua bora ajiondoe mapema. Cdm hatukumbatii mafisadi.
   
 18. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mi naona kama huyu jamaa analeta zilee za miaka ilee!!! Kama si za Dogo Asley, "usiponinunulia chips kuku naenda kusema kwa mama". Anatishia ili jamaa "Wakamwone" maana anataka kufidia zile posho zote alizokosa akiwa nje ya bunge kabla ya kuteuliwa Viti maalum.
   
 19. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #19
  Jul 30, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  JF naamini kuna mtu anayo majina yote, hebu tumwagieni hapa hayo majina tuwafahamu ili kauli mbiu ya: Where we dare to talk openly" itimie. Mkiyaficha mtakuwa hamna tofauti na magazeti.
   
 20. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mimi mwenyewe natamani hiyo list ibandikwe hapa jamvini ili watu tuandae magereza ya hawa waheshimiwa! Naimani hapa ndiyo itakuwa turning point ya rushwa kama spika atakuwa makini kutusaidia watanzania. Lakini akiendekeza uchama na ubabe wake pamoja na kutumia remote controller ya Lukuvi basi tutegemee hakuna jipya. lakini cha mhimu ni kujipanga kujenga hoja hadi hao wabunge watimuliwe na kuingizwa jela. May GOD help this time to provide a demo!!
   
Loading...