Rushwa bado cancer ya taifa letu, hadi NIDA?.

lushalila

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
283
107
Wana jamii forum nimepata taarifa kutoka kwenye zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya taifa mkoani Kagera.

Kama mnavyojua kule ni mpakani na nchi jirani zipatazo tatu hivyo wahamiaji haramu in wengi mno.

Pamoja na taarifa za kuwepo kwa usiri mkubwa kati ya maafsa uhamiaji na watendaji wa serikari, ila habari zilizopo ni kwamba mwenye uraia wa mashaka hakai foleni, ni laki moja tu anamaliza siku moja huku wazawa wakisota kwa zaidi ya Siku tatu kwenye foleni.

Bado haitoshi, anafika mtendaji wa serikari na migambo wanatoza era ili uweze kuandikwa, mfano majuzi wanadai ilikua ni 500 tsh, huna subiri sana.

Zoezi la uandikishaji wa vitambulisho ni zuri mno kwa maendereo ya taifa, ila natumaini ni kwa watanzania tu ndo wawe na vitambulisho kama watanzania , na wageni watambulike kama wageni kama zifanyavyo nchi nyingine.

Pia isiwe sehemu ya kupigia dili kwa maaskari mgambo pamoja na watendaji kwani hii document muhimu sana, ahsante
 
Ubaguzi wa binadamu kwa binadamu unaendelea...bila kitambulisho basi hakna kuvuta hewa yetu...sio? Tuache kubaguana...kwa mambo kama hya
 
Kuna umuhimu gani wakufanya hivyo wakati inafahamika kabisa mimi ni mtu fulani na % Mimi ni mtanzania

Kwanini wasiwaite wakimbizi ndio wawape vitambulisho vya uraia hapa nchini?
 
Kuna umuhimu gani wakufanya hivyo wakati inafahamika kabisa mimi ni mtu fulani na % Mimi ni mtanzania

Kwanini wasiwaite wakimbizi ndio wawape vitambulisho vya uraia hapa nchini?
Kibaya zaidi mkimbizi kisa tu ana elf kumi hakai foreni , mzawa mnachapana makonde kugombea foleni
 
Yani hakuna anayeachwa ilimladi ana era isipokua kamahuna kitu chafoleni unakipata , na bado wanasema muda ukiisha watakakuabado watarudiwa, ilasio wahamiaji wenye mkonomrefu.ni hatari
 
Back
Top Bottom