Amiliki
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 2,085
- 1,004
Nimemsikiliza kwa makini Mh. Waziri Mkuu Mstaafu kwa heshima (si kwa kashfa ya kutuibia wananchi), Mh. Fredrick Sumaye akieleza kwamba rushwa ndani ya chaguzi za CCM si tatizo jipya ispokuwa la sasa limekuwa la aina yake kidogo kwani ni rushwa ya "Kimtandao" ambapo mtu anaweza akawa sehemu nyingine lakini aka-influence uchaguzi wa watu anaowataka toka sehemu nyingine ya nchi so long kwamba watakaochaguliwa atakuja kuwatumia huko mbeleni.
Swali ninalojiuliza, kama hivi vitu vipo dhahiri kihivi mpaka akina Sumaye wanavizungumza hadharani na hatujasikia mtu yeyote amekamatwa na rushwa na kuhukumiwa kwenye chaguzi za CCM, je kweli kuna haja gani ya kuwa na chombo kama Takukuru ambacho kinaendeshwa kwa kodi zetu?
Naomba kuwasilisha.